Saturday, January 7, 2017

SHEIN YAANZA LIGI VIZURI

Time ya Shein Rangers Sc imeanza vizuri ligi daraja la Pili mkoa wa Dar es salaam kwa kuichapa timu ya Amani Fc bao 4 - 0, mchezo huo uliochezwa Siku ya Ijumaa tarehe 6/1/2017 katika uwanja wa Kinesi ni wa kundi A. Magoli ya Shein yalifungwa na Fedson Deus matatu na moja Hamis Kado

Wednesday, November 9, 2016

KIKOSI CHA SHEIN RANGERS

Kikosi cha timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB kilichocheza mchezo wa kirafiki na timu ya BLACK STARS ya Gongolamboto na kutoka sare ya bao 2 - 2. Katika uwanja wa Sinza E darajani siku ya tarehe 08 November 2016.

Thursday, November 3, 2016

SHEIN RANGERS WAJAZA MAPENGO YA UONGOZI

Siku ya tarehe 30 October 2016 Klabu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUBI ilifanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi ya Mwenyekiti na Makamu wake, aliyechaguliwa Mwenyekiti ni Ndugu Ally Mzee na Makamu wake ni Ndugu Amasha Zein. SHEIN RANGERS SC inawatakia kila la heri katika nafasi zao mpya.

Sunday, October 23, 2016

SHEIN RANGERS YAZAWADIWA VIFAA

Mdau wa michezo Sinza Ndugu Yahaya (kushoto) aizawadia timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB vifaa vya michezo. SHEIN ambao ndiyo mabingwa wa Wilaya ya Kinondoni, pichani juu akikabidhi jezi na mipira kwa mjumbe wa soka la vijana wa SHEIN ndugu Rashid Said hivi karibuni.

Tuesday, October 18, 2016

TAARIFA TOKA SHEIN RANGERS SPORTS CLUB

Uongozi wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB unapenda kutoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kupapamba na kujitoa kwao hadi kufikia lengo tulilojiwekea mwaka huu la kupanda daraja kwa msimu huu. Vilevile uongozi unatoa Shukurani za dhati kabisa kwa wadau na wanamichezo wote walioiunga mkono timu kwa wakati wote wa ligi daraja la tatu Wilaya ya Kinondoni na hatimaye timu kujenga historia mpya kwa kuwa mabingwa wa ligi daraja la tatu Wilaya ya Kinondoni kwa msimu wa 2015/16 uliomalizika hivi karibuni.

Hakuna cha kusema zaidi ya kusema Asante wanakinondoni kwa kutuunga mkono kwa wakati wote.

Kwa sasa timu inaendelea na maandalizi ya ligi ya Mkoa katika uwanja wa Sinza "E" Darajani, pamoja na maandalizi hayo ni kipindi cha kutengeneza Kikosi imara cha ushindani na benchi la ufundi linatumia nafasi hiyo kufanya usaili kwa wachezaji wapya wenye uwezo wa kuitumikia timu. Benchi la ufundi Shein Rangers linapenda kuwataarifu wachezaji wanaojiona wana uwezo wa kuitumikia timu kufika uwanjani hapo kwa ajili ya majaribio. Muda wa majaribio ni saa 10:00 jioni hadi saa 12:30 jioni kila siku ya Jumatatu hadi Jumatano, eneo uwanja wa Sinza "E" Darajani.

Friday, October 14, 2016

SHEIN RANGERS NDIO MABINGWA WA KINONDONITimu ya Shein Rangers Sc leo imedhiilisha kuwa haikuongoza kundi B kwa bahati baada ya kuichapa Ukwamani FC walioongoza kundi A katika mchezo mzuri wa fainali kusaka Klabu bingwa ya Wilaya ya Kinondoni kutamatisha ligi daraja la tatu wilaya. Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Kinesi umeamua nani bingwa wa wilaya kati ya timu mbili zitakazowakilisha Kinondoni katika ligi ya mkoa wa Dar es salaam.

Katika mchezo wa leo magoli yote ya Shein Rangers yalipatikana katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mkongwe Shomari Pengo na Muddy Vidal. Pamoja na ushindi huo Shein ilizawadiwa Kombe na Cheti cha ushiriki wa ligi daraja la tatu kwa msimu wa 2015/16 iliyomalizika hivi karibuni.

FAINALI YA KLABU BINGWA KINONDONI LEO

Ule mchezo wa fainali Klabu Bingwa Wilaya ya Kinondoni uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa kati ya timu ya Shein Rangers na Ukwamani FC utachezwa leo katika uwanja wa Kinesi saa kumi jioni.

Pamoja na mchezo huo vilabu vyote vilivyoshiriki ligi daraja la tatu msimu huu vitakabidhiwa vyeti uwanjani hapo kabla ya mchezo huo.

Wednesday, October 12, 2016

FAINALI UBINGWA WA WILAYA YA KINONDONI

Kesho Ijumaa tarehe 14 October 2016 timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB inatarajia kuandika Historia mpya katika mchezo wa soka kwa kuwania ubingwa wa Wilaya ya Kinondoni baada ya kuibuka kinara wa kundi B katika ligi daraja la tatu Kinondoni. Kwa matokeo hayo itacheza na kinara wa kundi A timu ya Ukwamani FC kutafuta bingwa wa Wilaya.

Mchezo huo wa fainali utachezwa katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam, muda wa saa 10:00 jioni. Vilevile pamoja na mchezo huo Chama Cha Mpira Kinondoni KIFA kinatarajia kutoa vyeti kwa timu zote shiriki ligi daraja la tatu iliyomalizika hivi karibuni, Viongozi wa vilabu mnatakiwa kudhuria tukio hilo litakalofanyika kabla ya mchezo wa fainali.

Mungu Ibariki Shein Rangers, Mshikamano Daima!!

Saturday, October 8, 2016

Wednesday, October 5, 2016

Shein Rangers Yaendelea na Mazoezi

Timu ya Shein Rangers inaendelea na mazoezi kujiandaa na fainali ya kutafuta bingwa wa Wilaya ya Kinondoni

Friday, September 30, 2016

SHEIN YANUSA DARAJA PILI MKOA DAR ES SALAAM

Wachezaji wa Shein Rangers Sports Club wakishangilia kupata nafasi ya kucheza ligi daraja la pili Mkoa wa Dar es salaam.

KOZI YA UKOCHA CHETI CHA AWALI


Mafunzo haya yanaandaliwa na KIFA wakishirikiana na Makocha Wakufunzi.
Kozi hii ni Maalum kwa;
1. Waalimu wa Soka
2. Viongozi wa Soka
3. Wadau wa Soka

Faida ya Cheti hiki:
1. Kuijua kiundani Soka na sheria zake
2. Kuongoza Klabu na Taasisi za Michezo
3. Ajira kufundisha Timu inayoshiriki mashindano yoyote isipokuwa Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Kuu tu

Ada ya Mafunzo ni Tsh 85,000/= tu kwa wiki mbili

KWA WANAOHITAJI:
Fika ujisajiri mapema Ofisi za KIFA

HATIMAYE SHEIN YAPANDA TENA DARAJA

Timu ya Shein Rangers Sports Club imefuzu kucheza ligi ya Mkoa wa Dar es salaam baada ya kumaliza ligi daraja la tatu Wilaya ya Kinondoni kwa kuongoza kundi B. Timu nyingine kutoka kundi A ni Ukwamani FC.

Tuesday, August 9, 2016

KAA TAYARI BACK SOON

Blog ya Shein Rangers ipo mbioni kurudi hewani na mambo mapya kabisa, Kaa Tayari Back Soon

Thursday, February 18, 2016

BLOG YA SHEIN KURUDI HEWANI SOON

Blog ya Timu ya soka ya Shein Rangers iliyokuwa haipo hewani kwa kipindi kirefu ipo katika mchakato wa kurudi upya muda si mrefu. Blog ya Shein kurudi na muonekano mpya na habari moto moto za timu ya Shein Rangers.

Friday, October 10, 2014

SHEIN RANGERS YAPANDA DARAJA


Hatimaye timu ya Shein Rangers Sports Club imetimiza ndoto yake  ya kupanda daraja, toka daraja la nne kwenda la tatu kwa msimu wa 2013/2014 wilaya ya Kinondoni.

Wednesday, October 1, 2014

SHEIN KUMALIZA NA HILL WORRIORS

Shein Rangers Sc kumaliza michezo yake ya kundi B ligi daraja la nne Kinondoni hatua ya 16 bora kwa kupambana na Hill Worriors, tarehe 02 Oct 2014 saa 10:00 jioni katika uwanja wa shule ya msingi Mwananyamala B.

SIKIA ALICHOSEMA KOCHA MKUU WA SHEIN RANGERS

Namshukuru mungu kwa kuniamsha salama nikiwa na furaha amani na upendo hakika alipangalo mungu binadam huwez kulipangua hongereni vijana wa shein rangers kwakupanda daraja la 3 kaz nzuri mmefanya nikiwa mimi mwalimu wenu nawapongeza kwahilo TUNAWEZA

Hayo ni maneno ya kocha mkuu wa Shein Rangers Sports Club RASHID SAID kupitia ukurasa wake wa Facebook

Saturday, September 20, 2014

TAMBAZA YAICHAPA SHEIN RANGERS 1 - 0

Ligi daraja la nne hatua ya 16 bora iliendelea tarehe 19 Sep 2014 katika uwanja wa Kinesi kwa kukutanisha timu ya Shein Rangers na Tambaza. Katika mchezo wa kwanza kwa timu ya Shein hatua 16 bora ilichapwa bao 1 - 0.

Pamoja na kupoteza mchezo huo timu ya Shein Rangers ilicheza chini ya kiwango, kitendo kilichowashangaza wapenzi wa soka.

Tuesday, September 9, 2014

LIGI DARAJA LA NNE KINONDONI

LIGI DARAJA LA NNE WILAYA YA KINONDONI 2012/2013 HATUA YA TIMU 16 BORA, Timu ya Shein Rangers SC imepangwa kundi "B" lenye timu tano, nazo ni:-
1. Fort Eagles
2. Mbezi Beach Utd
3. Tambaza SC
4. Shein Rangers SC
5. Hill Worriors