Thursday, January 29, 2009

Shein mazoezini


Walinda mlango wa shein rangers wakiwa mazoezini, wakiongozwa na said mbegu aliyesimama na walio chini kutoka kushoto ni salum Abdalah na mfaume. Shein rangers hufanya mazoezi yake kila siku katika uwanja wa TP sinza.

Monday, January 19, 2009

Said Mbegu na IbraSaidi Mbegu (picha ya chini) na Ibrahim Kombo wakiwa mazoezini SHEIN RANGERS SPORTS CLUB.

Thabit Abdalah (Mbabu)


Mchezaji wa shein rangers Thabiti Abdalah

Murshid


Mchezaji wa shein rangers Murshid Ally aliyeko timu ya taifa ya vijana wa tatu kutoka kulia (waliosimama) katika picha ya kumbukumbu na kocha wake Marcos Tinoco wa pili kutoka kulia na mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la mpira wa miguu tanzania (TFF) Sunday Kayuni wanne kutoka kulia. picha ilipigwa katika uwanja wa karume jijini dar es salaam wakati wa mazoezi ya timu ya taifa ya vijana (serengeti boys).

Ramadhan Issa Yarok (Dizana)Mchezaji Ramadhani Issa amezaliwa mwaka 1992, mpira alinza kucheza mwaka 2001 na mwaka 2005 amejiunga na shein rangers.

Malengo yake kucheza mpira wa kulipwa nje ya nchi.
Anamudu kucheza beki wa kati na ushambuliaji.
Maoni yake wadhamini wajitokeze kudhamini timu ya shein katika vifaa vya michezo.
Viatu anavaa namba 8-9.

Victor Wenslaus (Figo/Agogo)


Mchezaji Victor Wenslaus amezaliwa mwaka 1994 alijiunga na shein rangers mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 8. Alisoma shule ya Ukombozi Dar es salaam, wachezaji wenzake na wadau wa soka ufananisha uchezaji wake na Luis Figo na wengine Junior Agogo.

Ana imani mungu atamsaidia kufika malengo yake ya kucheza soka ulaya.
Maoni yake wadau wa soka wakiwekeza kwa vijana basi hakuna kinachoshindikana kutimiza ndoto za vijana kucheza soka ya kiwango cha juu.
Nafasi ya uwanjani ni ushambuliaji na kiungo, pia upenda kuvaa jezi namba 7.
Viatu anavaa namba 7.

Ibrahim J Kombo


Mchezaji Ibrahim Kombo amezaliwa mwaka 1992, amemaliza shule ya msingi mwaka 2006 kwa sasa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Turiani mkoani Dar es salaam. Amejiunga na shein rangers mwaka 2007.

Malengo yake ni kuwa mchezaji bora duniani.
Ana uwezo wa kucheza namba 2-7-9-10 ila anapendeleza zaidi kucheza namba 9.
Maoni yake makocha wazidishe juhudi katika mafunzo yao ili ndoto za wachezaji zitimie.
Anavaa viatu namba 7-8.

Said Mbegu


Mchezaji wa shein rangers Said Selemani Mbegu amezaliwa mwaka 1993 mkoani Dar es salaam na amejiunga na shein rangers mwaka 2005. Mwaka 2008 alichaguliwa timu ya mkoa wa kinondoni katika mashindano ya taifa ya copa coca cola.

Malengo yake ni kuwa mchezaji wa kulipwa.
Maoni yake wadau wajitokeze kusaidia timu za vijana.
Nafasi anayocheza ni mlinda mlango na anatumia mguu wa kulia.
Viatu anavaa namba 6 - 7.

Mwaka 2002


Kocha wa shein rangers Rashid Said akimuingiza katika moja ya mechi za kimashindano mchezaji wake Victor Wenslaus (figo). Picha hii ilipigwa mwaka 2002, victor mpaka sasa bado ni mchezaji tegemeo wa shein rangers.

Mwaka 2009


Mchezaji Victor Wenslaus pamoja na kocha wake wa soka toka utoto wake wakiwa katika picha ya pamoja mwaka 2009. Kocha Rashid Said alivumbua kipaji cha mchezaji huyo mwaka 2002, wachezaji wenzake upendelea kumfananisha uchezaji wake na figo na wengine Agogo.

Picha mbali mbali za Victor (Figo) 2009
Picha tofauti za mchezaji Victor Wenslaus (Agogo/Figo) akiwa mazoezini na timu yake ya shein, picha hizi ni za mwaka 2009.

MFAUME (Mlinda Mlango)


Mfaume moja ya magolikipa ambao ni mfano wa kuigwa katika timu ya shein na soka la tanzania, moja ya sababu kubwa ya kupewa jukumu la kulinda milingoti mitatu ya shein ni kujitolea kwake kwa kufanya mazoezi kwa moyo na bidii. Mara kwa mara Kocha wa shein amekuwa akimpa nafasi katika mechi kutokana na bidii yake mazoezini. Huu ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wengine hasa vijana.

Tuesday, January 13, 2009

Mechi ya funga mwaka


Kikosi kamili cha shein rangers wakiwa na walimu wao siku walipoifunga shein ya zamani 3 - 0 katika mechi ya funga mwaka 2008.

Monday, January 12, 2009

Timu ya U14 ndani ya morogoro


Baadhi ya wachezaji na mwalimu wa timu ya soka ya shein U14 wakiwa kambini morogoro baada ya mazoezi ya asubuhi wakati wa mashindano ya NZERU CUP.

Shein yabadili LOGO (nembo)Timu ya shein rangers imebadilisha nembo (logo) ili kwenda na wakati, nembo ya mpya inaonekana juu na ya zamani chini. SHEIN RANGERS SPORTS CLUB "THE HAMMER"

Moja ya Nguzo za shein


Kapteni Amme Mohamed (Gendaeka) mmoja ya nguzo muhimu za shein, ni mmoja ya wachezaji wa mfano kwa nidhamu ndani ya timu. Ndoto zake ni kupiga soka barani ulaya.

Nzeru Cup


Kocha Chid wa kwanza kushoto waliosimama akiwa na kikosi cha shein U14 mjini morogoro katika mashindano ya NZERU CUP. Shein rangers hushiriki mashindano hayo kila mwaka.

KIDYOSA


Katibu wa chama cha michezo kwa vijana wadogo wilaya ya kinondoni KIDYOSA Mwinyimadi Tambaza (mwenye kofia) akisalimiana na wachezaji wa shein rangers katika moja ya mashindano yanayoandaliwa na chama hicho.

Nyota ya shein yang'aa KampalaMchezaji nyota wa shein rangers Maharaji Bulu akiwa na marafiki zake jijini kampala nchini uganda akiwa na zawadi zake mbalimbali alizozawadiwa katika michezo ya mashule ya sekondari nchini humo.

Sunday, January 11, 2009

Copy ya Banka


Mchezaji wa kikosi cha U14 cha shein rangers na Nahodha wa kikosi hicho Adili a.k.a banka kulia akiwa na mkali mwenzake Shafii wakiwa morogoro na kikosi cha shein katika mashindano ya Nzeru Cup 2007. Adili uchezaji wake ufananishwa na mchezaji wa simba Mohamed Banka. Adili (banka) alimvutia kocha Talib Hilal wakiwa morogoro na kuamua kumpa zawadi.

Shein rangers na mwaka mpya


Kila mwisho wa mwaka kumekuwa na mazoea ya kuona shein rangers sports club ikifanya mambo ya burudani, ikiwamo kukutanisha kikosi cha kwanza cha wakati huo na kikosi cha wachezaji wa zamani waliopitia shein kwa miaka tofauti. Kwa mwaka 2008 ilifanyika mechi ya mpira wa miguu na shein ya zamani yanye jezi za rangi ya kijani ililala kwa kuchapwa 3 - 0 na shein ya sasa wenye jezi za bluu bahari katika mchezo mkali na uliovuta hisia za wapenzi wa soka toka maeneo ya sinza, tandale na manzese.

Saturday, January 10, 2009

Stars ya Yemen


Hiki ndio kikosi cha stars kilichocheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Yemen na stars kulala 2 - 1 huko yemen. Wadau wengi hawakupata kuona picha hii.

Shein Rangers yamsikia Maximo


Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania Marcio Maximo amekuwa akisisitiza kutumia wachezaji vijana kwa timu za ligi kuu, Shein Rangers ni moja ya timu za soka ambayo katika mipango yake ya muda mrefu ni kuwa kituo maalumu cha kukuza vipaji vya soka kwa vijana wa kitanzania. Shein ilianzishwa rasmi mwaka 1998 na imeendelea kutoa mchango mkubwa katika kuendeleza soka tanzania kwa kutoa vijana wengi waliopitia timu hiyo ambao wengine wapo katika timu za ligi kuu.

Thursday, January 8, 2009

Murshid ndani ya timu ya taifa


Mchezaji wa shein rangers murshid ally wa kwanza kulia akiwa na kocha wa timu ya taifa ya vijana Tinoco, pamoja na wachezaji wengine wa timu ya taifa wakiwa kambini.

Mchezaji shein amkuna maximo


Mchezaji wa shein rangers na timu ya taifa ya vijana ya tanzania U17 (serengeti boys) Murshid Ally akiwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya tanzania, taifa stars Marcio maximo. Maximo alivutiwa na kiwango cha mchezaji huyo mazoezini.

Kikosi cha pili


Wachezaji wa kikosi cha pili cha shein rangers baada ya mazoezi yao ya kawaida.

Kocha Rashid akiwa mafunzoni


Kocha wa Shein Rashid Said (wapili kutoka kulia) alipokuwa katika mafunzo maalum ya ukocha kwa timu za vijana yaliyoandaliwa na NMB. Wa kwanza kutoka kushoto ni mkufunzi wa makocha na kocha maarufu nchini Suleiman Gwaje.

Maajabu ya shein mechi 4 goli 22


Kikosi cha kwanza cha Shein Rangers kimefanya maajabu ya aina yake katika medani ya soka kwa ukanda wa sinza, kuanzia mwezi December 2008 mpaka January 2009 timu ya shein imecheza mechi nne mfululizo na kufunga magoli 22 na kufungwa magoli 5.Wakwanza kupata kipigo ni Sinza Star chini ya kocha Zagalo 6 - 0, wa pili Makumbusho FC 8 - 2, Kijitonyama chipuki 4 - 2 na Juhudi FC 4 - 1.

Wednesday, January 7, 2009

Shein kufufua mahusiano na Simba


Kwa muda mrefu kumekuwa na mahusiano mazuri kati ya timu ya shein rangers (maarufu the hammer) na timu kongwe nchini Simba SC, timu ya shein imekuwa na utamaduni wa kucheza na kikosi cha pili cha simba mara kwa mara kabla ya kuanza kwa mechi za ligi kuu katika uwanja wa taifa.Uongozi wa shein rangers umeamua kufufua mahusiano hayo kwa nguvu mpya mwaka huu.

Baada ya kazi


Timu ya U14 ya Shein Rangers baada ya mechi katika moja michezo iliandaliwa na KIDYOSO kumuenzi baba wa Taifa mwalimu JK Nyerere (Nyerere Day 2008). Shein Rangers ilishika nafasi ya tatu.

Shein Rangers yapata Afisa Habari


Mtangazaji na mwandishi wa Kituo maarufu cha Televisheni nchini ITV Bi Rehema Mwakangale awa Afisa Habari wa Shein Rangers Sports Club.

Jezi za Shein


Timu ya soka ya shein rangers pamoja na kufundisha soka kwa vijana, pia ufundisha vijana wake maadili na miiko ya mchezaji wa soka. Mfano mdogo ni jinsi vijana hao walivyofundishwa jinsi ya kuifadhi vifaa vya michezo ikiwepo kuandaa jezi kabla ya mchezo na baada ya mchezo.

Wachezaji wapya karibuni


Mwalimu mkuu wa shein rangers yenye maskani yake sinza Rashid a.k.a Mokake ametoa wito kwa vijana wote wanajiona wana kipaji cha soka kufika katika kiwanja cha TP sinza kwa ajili ya majaribio. Vijana wanaotakiwa ni wa chini ya miaka 14 na chini ya miaka 17 (U14 na U17) Vijana wote watakaopenda kufanya majaribio wafike uwanja wa TP sinza saa kumi kamili jioni na wamuulizie kocha Rashid (Teacher Chid) au wapige simu namba 0717294876 kwa maelezo zaidi.

Shein Yatisha!


Timu ya shein rangers imezidi kutisha katika medani ya soka ukanda huu wa sinza baada ya kuikandamiza Chipukizi FC bao 4 - 2.