Sunday, March 15, 2009

SHEIN RANGERS SPORTS CLUBUongozi wa shein rangers sports club unapenda kuwatangazia wanamichezo wote nchini hasa wapenzi wa soka kuwa blog hii ni mali ya shein rangers sports club, haina uhusiano na mtu yeyote wala kikundi fulani cha watu. Kwa maana hiyo kila anayeingia katika blog hii anapewa nafasi/uhuru wa kuchangia mawazo na maoni yake (comments)kwa maendeleo ya soka/michezo kwa vijana wa kitanzania.

Shein rangers daima inaamini michezo na elimu ndio ufunguo wa maisha kwa vijana wake, uongozi unapenda kutumia nafasi hii kuomba kwa taasisi binasfi na za umma kuweza kuwapatia nafasi za kujiendeleza kielimu wachezaji wake ikiwa njia ya kuwaendeleza vijana wa kitanzania kwa michezo na elimu.

Shein rangers pia inakaribisha makampuni na watu binafsi kuweza kuja kushirikiana kuwaendeleza watoto wa kitanzania hasa katika upande wa kielimu na vifaa vya michezo!

Imeandaliwa na Uongozi wa shein rangers sports. club

Wednesday, March 11, 2009

Yanga yajinoa kwa wacanada


Mshambuliaji wa wawakilishi wa Tanzania katika ligi ya mabigwa barani Afrika Yanga Ben Mwalala kulia akikokota mpira kuelekea goli la Vancover White Caps ya Canada katika mchezo wa kirafiki wa kujipima kabla ya yanga kukutana na Al Ahly ya Misri ambapo yanga ili iliwafunga mabigwa wa Canada Bao 3 - 1. Mchezo uliochezwa katika uwanja mpya jijini dar.

Friday, March 6, 2009

MSIBA: Afisa Habari Shein Rangers Afariki Dunia


Uongozi wa shein rangers unasikitika kwa kuondokewa na mmoja wa watu muhimu ndani ya timu, Bi Rehema Mwakangale ambaye alikuwa akishikilia cheo cha afisa habari toka 27 October 2008 mpaka kifo chake. Rehema alifariki tarehe 04 March 2009, marehemu alikuwa mmoja wa watu waliofanikisha kuanzishwa kwa blog hii ndani ya timu ya shein rangers na pia alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha timu inapata nafasi katika vipindi vya michezo katika televisheni ya ITV (TAMASHA LA MICHEZO). Sisi shein rangers tunaungana na watanzania wengine pamoja na wanamichezo wote nchini kumuombea mwanamichezo mwenzetu aliyetutoka na kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki kwani mwenzetu ametangulia na sisi tutafata. MUNGU AIWEKE ROHO YA REHEMA MAHALA PEMA PEPONI AMIN!!

Stars wang'ara CHAN


Mchezaji wa timu ya taifa ya tanzania Taifa stars Nizar Halfan akifanya vitu vyake, siku stars ilipoifunga Ivory Coast bao 1 - 0 kwenye uwanja wa Felix Houohouet Boigny mjini Abijan katika michuano ya Mataifa ya Afrika CHAN 2009