Monday, June 29, 2009

Tathmini ya mechi za Shein Rangers toka mwezi Janury mpaka June 2009

MECHI
Mechi zilizochezwa ni 24
Mechi ilizoshinda 19
Mechi ilizopoteza 1
Mechi za suluhu 4

MAGOLI

Magoli ya kufunga 100
Magoli ya kufungwa 45

Mchezaji anayeongoza kwa magoli
Maharaji Lal Bulu magoli 20
Victor Wensleaus magoli 11
Ibrahim Juma magoli 10

Mchezaji aliyecheza mechi nyingi
Maharaji Lal Bulu mechi 19
Victor Wansleaus mechi 18
Nassoro Udulele mechi 17

U 14 Shein yapiga 2 - 0


Timu ya shein rangers U 14 (pichani) imeichapa KIMARA SPORTS ACADEMY bao 2 - 0, mechi hiyo ilichezwa Tarehe 28 June 2009 katika uwanja wa TP sinza

Shein watembelea watoto yatima


Timu ya shein rangers imetembelea na kutoa msaada katika kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo magomeni jijini Dar es salaam, msaada huo ni moja ya sherehe za shein rangers kusheherekea ubigwa wa SINZA CUP 2009. Picha zaidi zinafuata hapo chini.

Thursday, June 25, 2009

Shein Rangers ilipoifunza soka Simba B


Timu ya shein rangers wanye jezi za bluu bahari kulia siku walipoifunga Simba B bao 5 - 3 katika uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaam.

Sherehe za SINZA CUP


Baadhi ya wachezaji wa shein rangers wakisheherekea ubingwa wa SINZA CUP 2009, kutoka kushoto Ibrahim Kombo (Eto'o),Muntasir Abdul (casillas) na Maharaji Bulu (David villa).

Mdau Didi akiwa na wachezaji wa shein


Wachezaji wa shein rangers wakiwa na mmoja wa wadau wa soka ndugu Rajab Didi (wa mwisho kulia)katika duka la vifaa vya michezo la game (mlimani city)kutoka kushoto ni Maharaji Bulu, Ibrahim Kombo (watatu kutoka kushoto)

Sunday, June 21, 2009

Murshid ndani ya Hill Park Joburg


Mchezaji wa Shein Rangers Murshid Ally akiwa katika uwanja wa Hill Park jijini Joburg kuangalia mechi ya ufunguzi FIFA comfederation cup 2009 kati ya South Africa na Iraq.

Serengeti Boys ndani ya Ellis Park South Africa


Serengeti Boys


Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana SERENGETI BOYS wakiwa katika mazoezi yao ya kawaida nchini Afrika kusini wakati wa mashindano ya copo coca cola, vijana hao wa Tanzania walishika nafasi ya tatu. Mchezaji wa shein rangers murshid wa pili kutoka kulia.

Safari ya Mchezaji wa shein Afrika Kusini

Mchezaji shein ndani ya Joburg


Mchezaji wa shein rangers Murshid akiwa ndani ya duka maarufu la vifaa vya michezo jijini Joburg South Africa.

Ubingwa Raha


Wachezaji wa Shein Rangers na wapenzi wa timu hiyo wakisheherekea ubingwa wa SINZA CUP 2009.

Monday, June 15, 2009

Mawaidha


Kocha mkuu wa shein rangers Rashidi (Kocha Chid) akitoa mawaidha kwa wachezaji wake katika moja ya michezo ya shein katika uwanja wa karume jijini dar.

Shein Mabigwa SINZA CUP 2009


Timu ya shein rangers (pichani)imetwaa ubigwa wa SINZA CUP 2009 bila ya kupoteza mchezo wowote wala kutoka sare.

Saturday, June 13, 2009

Katibu KIFA aipongeza shein


Katibu wa chama cha soka wilaya ya kinondoni (KIFA) ndugu Frank Mchaki (kushoto), aipongeza shein rangers kwa kutwaa ubigwa wa SINZA CUP 2009 na kwa kuvumbua na kulea vipaji vya soka nchini. Mashindano ya sinza cup yalishirikisha timu za kata zote za kinondoni. Kulia ni mwenyekiti wa CCM sinza mheshimiwa Mbonde.

Mbunge Azan kudhamini mafunzo ya makocha shein


Mbunge wa kinondoni Mh Iddi Azan (kushoto) akiwa na diwani wa sinza na mdhamini wa mashindano ya SINZA CUP Mh Salim Mwaking'inda akitoa nasaa zake baada ya fainali, pia mbunge huyo amejitolea kudhamini makocha wawili wa shein rangers katika kozi za ukocha wa soka.

MABIGWA SINZA CUP 2009


Naodha wa shein rangers GODFREY INOCENT WAMBURA akipokea zawadi ya mshidi wa kwanza seti mbili za jezi toka kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Iddi Azan mbunge wa jimbo la kinondoni. Baada ya kuifunga third word bao moja bila katika fainali ambayo shein rangers ilionyesha kiwango kikubwa cha soka.

Sunday, June 7, 2009

Mchezaji shein rangers ang'aa Afrika Kusini


Murshid (watatu toka kushoto mbele) akiwa na timu yake ya shein rangers, mchezaji huyo ni mmoja ya wachezaji walioonyesha uwezo mkubwa katika mechi dhidi ya Ethiopia ambapo vijana wa tanzania walishinda 5 - 0 na murshid alifunga goli la nne katika michuano ya dunia ya copa coca cola nchini afrika ya kusini.

Tuesday, June 2, 2009

Mchezaji shein rangers apita mchujo timu ya taifa


Mshezaji wa shein rangers murshid ally kulia akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya vijana (Serengeti Boys)ni moja kati ya wachezaji kumi na sita waliopita mchujo wa wachezaji watakaowakilisha taifa nchini Afrika Kusini katika michuano ya Copa Coca Cola.

Murshid apeperusha bendera ya shein na taifa Bondeni


Mchezaji wa shein rangers murshid ally(wa kwanza kushoto)akiwa na wenzake wa timu ya taifa ya vijana katika uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere kuelekea nchini Afrika ya kusini kushiriki michuano ya dunia ya copa coca cola.