Thursday, July 30, 2009

Shein Rangers Sports Club


Kocha mkuu wa shein rangers Rashid Said akiwapa mbinu za soka wachezaji wake kabla ya kuanza kwa moja ya michezo ya ligi ya SINZA CUP 2009.

Sunday, July 26, 2009

Itamar


Mchezaji wa shein rangers Murshid Ally akiwa katika picha ya kumbukumbu na kocha mkuu wa Azam FC Itamar Amorn katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Shein Rangers Sports Club


Kocha mkuu wa shein rangers Rashid Said wa kwanza kutoka kulia mstari wa nyuma akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wake.

Saturday, July 25, 2009

Mazoezi


Mwalimu wa magolikipa wa shein rangers Godfrey a.k.a Loya akimpa mazoezi kipa wa shein Mfaume.

Wednesday, July 22, 2009

Rashid Said a.k.a Sir Mokake


Kocha mkuu wa shein rangers Rashid Said mwenye nguo nyeupe kulia akitoa maelekezo kwa wachezaji wake katika moja ya mechi za shein rangers 2009. Rashid ni moja ya makocha wanaoheshimika sana maeneo ya sinza,kijitonyama,manzese na maeneo ya jirani pia yeye ndio muasisi wa timu ya shein rangers miaka 11 iliyopita.

Tuesday, July 21, 2009

Kocha Mkuu wa Shein Rangers


Pichani ni kocha mkuu wa shein rangers Rashid Said maalufu kwa Sir Mokake akiwa mapunzikoni jijini Dar es salaam. Kocha huyo ana sifa ya kuvumbua na kukuza vipaji vya soka kwa vijana.

Sunday, July 19, 2009

Taarifa kutakiwa wachezaji

Baadhi ya timu za ligi kuu ya VODACOM Tanzania (hasa timu kubwa) zimevutiwa na baadhi ya wachezaji wa Shein Rangers kwa ajili ya kuongeza nguvu katika vikosi vyao vya pili ikiwa ni kutekeleza maagizo ya TFF ya kuwa na timu za vijana (timu B).

Uongozi wa shein rangers unazitaka timu ambazo zinaitaji wachezaji toka shein rangers kufika kwa uongozi kwa ajili ya hatua za uhamisho wa wachezaji na sio kuwarubuni wachezaji wetu kama moja ya timu kubwa nchini inavyofanya kwa baadhi ya wachezaji wetu. Shein rangers imekuwa na ikiwaandaa wachezaji hao toka wakiwa chini ya miaka 12 mpaka sasa wana miaka 16 na kuendelea.

IMEANDALIWA NA UONGOZI WA SHEIN RANGERS

Friday, July 17, 2009

THE MOST WANTED


Timu ya shein rangers katika picha ya pamoja na timu ya THE MOST WANTED baada ya mchezo wa kirafiki.

Thursday, July 16, 2009

Uwanjwa wa Karume


Wachezaji wa akiba wa shein rangers wakifatilia kwa makini moja mechi zao za kujipima nguvu katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.

Wednesday, July 15, 2009

Kutoka uongozi wa shein rangers

Siku ya tarehe 15 July 2009 timu ya soka ya shein rangers ya sinza ilikuwa icheze mchezo wa kirafiki na ndugu zao wa VODACOM TANZANIA nyakati za usiku katika uwanja wa Al - muntazil upanga jijini Dar es salaam.

Uongozi wa shein unapenda kuchukua nafasi hii kuomba radhi kwa kutofanyika mchezo huo kutokana na wachezaji wao kuchelewa kutoka katika usaili wa timu ya Simba SC, kwani karibu timu nzima ilikuwa katika usaili kwa ajili ya kikosi cha pili cha Simba.

Mchezo huo ulikuwa ni marudiano baada ya timu hizo kukutana katika mchezo wa awali siku ya tarehe 09 July 2009 katika uwanja huo huo.

Uongozi wa shein rangers unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa kutofanyika mchezo huo.

IMEANDALIWA NA UONGOZI WA SHEIN RANGERS

Monday, July 13, 2009

Mdau awaasa wachezaji


Mmoja wa maafisa wa VODACOM TANZANIA Bro Viduka kitoa nasaa zake kwa wachezaji wa shein rangers mara baada ya mchezo wa mazoezi uliochezwa usiku kati ya shein na staff wa VODACOM, pamoja na kuisifia shein kwa kucheza mchezo mzuri na wa kuvutia pia alisifia nidhamu na uwezo wa wachezaji wote wa shein rangers na kuwataka kuwa wasikivu kwa walimu na viongozi wao.

Shein na Vodacom


Wachezaji wa timu ya shein rangers wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya soka ya STAFF wa kampuni ya simu za mkononi ya VODACOM TANZANIA mara baada ya mchezo wa mazoezi uliofanyika usiku katika viwanja vya al muntazil upanga jijini Dar es salaam.

Wachezaji wakipasha


Wachezaji wa shein rangers wakipasha misuli joto wakati wa maandalizi ya moja ya michezo yake jiji Dar es salaam.

Naodha akipokea zawadi


Mchezaji mwandamizi na naodha wa shein rangers Godfrey Inocent akipokea zawadi ya jezi seti mbili toka kwa mgeni rasmi mbunge wa kinondoni mheshimiwa Iddi Azan baada ya shein kutwaa ubigwa wa SINZA CUP 2009. Godfrey amejiunga na shein rangers mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 13 na ajawahi kuchezea timu yoyote mpaka sasa ni mchezaji/naodha anayeheshimika sana ndani ya timu.

Godfrey chuoni


Naodha wa shein rangers Godfrey Inocent akipokea zawadi ya mchezaji bora wa mashindano, baada ya kumalizika mashindano ya soka chuoni DIT.

Godfrey akiwa TangaPicha tofauti za naodha wa shein rangers Godfrey Inocent wakati wa michezo ya vyuo iliyofanyika Jijini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani. Godfrey ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha ufundi (DIT) jiji Dar es salaam.

Friday, July 10, 2009

Shein ndani ya TANZANIA SPORTS ACADEMY


Wachezaji wa shein rangers (wenye jezi za bluu bahari)wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa chuo cha kukuza vipaji cha TFF TANZANIA SPORTS ACADEMY (TSA) baada ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu katika uwanja wa karume.

TSA


Kocha mkuu wa shein rangers Rashid Said (watatu kutoka kusho) akiwa katika picha ya pamoja na meneja wa TANZANIA SPORTS ACADEMY (TSA) Jason Barry anayemfatia, baada ya mchezo wa kirafiki kati ya shein rangers na TSA katika uwanja wa karume, wa kwanza kulia ni kocha mkongwe nchini Kaijage.

Thursday, July 9, 2009

Kinara wa magoli shein rangers


Mchezaji wa shein rangers Maharaj Lal Bulu ndiye anaongoza kwa kufunga magoli mengi toka mwezi January mpaka June 2009 amefunga magoli 20 katika michezo 19 aliyocheza.

Wasouth wamfata mchezaji shein dar


Skauti wa kusaka vipaji vya wachezaji wa soka kutoka nchini Afrika Kusini Damian Armstrong wa pili kulia atua jijini dar kumfata mchezaji nyota wa shein rangers Murshid Ally aliyeng'ara katika michuano ya soka kwa vijana duniani maarufu copa coca cola. Pichani kutoka kulia ni mwalimu wa soka wa Murshid toka akiwa na umri wa miaka 9 mpaka sasa anayefuata Damian, Murshid na cameraman wa Damian naye toka Afrika kusini. Damian amesema hakutengemea kukuta vipaji vya soka vya hali ya juu ndani ya shein rangers.

Akutana na wachezaji shein


Skauti wa soka Damian kutoka Afrika Kusini akiongea na wachezaji wa kikosi cha kwanza cha shein rangers, pamoja na kusaka vipaji pia anatengeneza Profile ya mchezji wa shein Murshid Ally itakayokuwa katika mfumo wa DVD. Picha za chini ni picha mbali mbali wakati walipokuwa kazini kutengeneza video hiyo.


Utambulisho


Damin Armstrong kutoka South Africa akijitambulisha kwa mmoja wa wakurugenzi wa shein rangers ndugu Amani (kulia) walipofika kusaka vipaji vingine ndani ya shein rangers baada ya kuvutiwa na mchezaji wa shein Murshid Ally walipomuona katika mashindano ya Copa Coca Cola nchini Afrika ya Kusini.

Mwenyekiti


Mwenyekiti wa shein rangers S.A Mkwana akisalimiana na mmoja wa wageni wake waliotua katika timu ya shein kusaka nyota wengine.

Naodha wa kikosi cha kwanza


Naodha wa kikosi cha kwanza cha shein rangers Godfrey Innocent (kushoto) akisalimiana na skauti wa kusaka wachezaji toka South Africa Damian Armstong, katikati ni kocha mkuu wa shein rangers Rashid Said (Sir Mokake)akishuhudia.

Naodha wa kikosi cha pili


Skauti wa kusaka vipaji vya soka Damian Armstong kutoka South Africa akipeana mikono na naodha wa timu ya watoto ya shein Adriano Selestino baada ya kufurahishwa na kipaji chake.

Friday, July 3, 2009

Shein yatoa mchezaji mdogo SINZA CUP 2009


Mchezaji wa shein rangers sports club Adriano Selestine (banka) ndio mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote walioshiriki mashindano ya SINZA CUP 2009 na shein kuwa wafalme wa soka sinza, Adriano amezaliwa mwaka 1997. Pichani Adriano akipokea zawadi ya mchezaji mdogo kuliko wote kutoka kwa mbunge wa kinondoni mheshimiwa Iddi Azan.