Monday, August 31, 2009

VILABU VYA LIGI KUU (VPL)

Uongozi wa timu ya Shein Rangers unapenda kuzikumbusha timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) ambazo zimevutiwa na wachezaji wa shein rangers kwa ajili ya kuongeza nguvu katika vikosi vyao vya pili, watekeleze makubalino ya awali ili kuweza kuwatumia wachezaji hao, na shein rangers iweze kuandaa wachezaji wapya kwa maendeleo ya soka la vijana na mpira wa miguu Tanzania.

SHEIN KUENDELEA NA LIGI YA VIJANA

Timu ya Shein Rangers inaendelea kucheza ligi ya vijana chini ya miaka 17 katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, mchezo unaofatia utachezwa tarehe 06 Septemba 2009 siku ya Jumapili saa kumi kamili jioni katika uwanja wa Bubu Mburahati jijini Dar es salaam. Wapenzi wote wa soka mnakaribishwa kupata burudani ya soka toka Shein Rangers Sports Club.

Wednesday, August 19, 2009

KUTANA NA BEKI MWENYE NGUVU


Nassoro Udulele beki mwenye nguvu na uwezo wa kucheza namba zote za nyuma na kiungo ni kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha shein rangers.

Sunday, August 16, 2009

LIGI YA VIJANA MBURAHATI

Timu ya Shein Rangers imetoka sare ya goli 1 - 1 na timu ya Young Boys ya mburahati katika mchezo wa ligi ya vijana chini ya miaka 17. Mchezo ulikuwa wa kasi na kuvutia kwa muda wote. Goli la shein lilifungwa na mshambuliaji wake mwenye uchu wa magoli Victor Wenslaus dakika ya 29 kipindi cha kwanza na young boys walisawazisha dakika za lala salama.

Thursday, August 13, 2009

BEKI MWENYE UWEZO WA KUFUNGA


Beki kisiki wa shein rangers Amme Mohamed mwenye uwezo wa kupanda na kufunga pia.

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO ALIYOYAKUTA YANGA
Naibu waziri wa Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alipokuwa kweye ziara katika klabu ya yanga.(picha kwa hisani ya Global Publishers)

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO ALIYOYAKUTA SIMBANaibu Waziri wa Utamaduni na Michezo, Joel Bendera akiwa ndani ya klabu ya simba alipofanya ziara kwenye klabu hiyo kongwe nchini.(Picha kwa hisani ya Global Publishers)

Wednesday, August 12, 2009

PONGEZI

Timu ya shein rangers imepokea pongezi toka kwa wadau mbalimbali wa soka toka maeneo ya Mburahati na Manzese kutokana na kucheza mchezo wa kuvutia uliofurahisha wapenzi wengi wa soka, kocha wa shein Rashid Said amepokea simu za pongezi leo tarehe 12 Agost 2009 kufuatia shein kuichapa MB Market 3 - 1 na kucheza soka la hali ya juu, mchezo huo ulifanyika jana tarehe 11 Agost 2009 ligi ya vijana chini ya miaka 17.

Tuesday, August 11, 2009

MCHEZAJI MPYA


Mchezaji mpya shein rangers Salum Abdallah a.k.a Salu T aongoza ngome ya shein rangers katika mchezo wa kwanza wa ligi ya vijana chini ya miaka 17. Shein ilicheza mchezo mzuri wa kuvutia uliofurahisha wakazi wa Mburahati.

SHEIN YAANZA KWA KISHINDO MASHINDANO


Timu ya shein rangers (jezi za njano na bluu) leo tarehe 11 Agost 2009 imeanza kwa kishindo mashindano ya vijana chini ya miaka 17 MAMA HIDAYA CUP 2009 kwa kuifunga timu ya MB Market magoli 3 - 1. Magoli ya shein rangers yalifungwa na Lukinga goli la kwanza, Ibrahimu Juma la pili na Maharaji Lal Bulu goli la tatu. Mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Bubu Mburahati jijini Dar es salaam.

MAWAIDHA


Kocha wa shein rangers Rashid Said a.k.a Sir Mokake, akiwapa mawaidha wachezaji wake wakati wa maandalizi ya mechi ya ligi ya vijana chini ya miaka 17 MAMA HIDAYA CUP 2009. Matokeo ya mchezo huo ni Shein Rangers 3 MB Market 1.

Monday, August 10, 2009

SINZA STARS YALALA

Timu ya sinza stars chini ya kocha mzalendo Zagalo imekubali kipigo cha goli 2 - 0 toka kwa shein rangers siku ya tarehe 09 Agost 2009 katika uwanja wa TP Africa sinza, Magoli ya shein yalifungwa na Maharaji Bulu na Amme Mohamedi.

Saturday, August 8, 2009

HENRY JOSEPH NA TIMU MPYA


Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Henry Joseph ameanza kucheza soka ya kulipwa katika timu yake mpya ya Kongsvinger FC ya nchini Norway.

Friday, August 7, 2009

SHEIN WAKIJIANDAA NA MASHINDANO YA VIJANA


Wachezaji wa shein rangers sports club wakiwa katika mazoezi makali ya kujiandaa na ligi soka ya vijana chini ya miaka 17 (U 17) MAMA HIDAYA CUP.

KIJITONYAMA CHIPUKIZI YAIPONGEZA SHEIN


Timu ya Kijitonyama Chipukizi Sports Club (KCSC) ya Kijitonyama imetuma pongezi rasmi kwa timu ya shein rangers kwa kuwa mabingwa wa SINZA CUP 2009.

MAMA HIDAYA CUP U - 17

Timu ya shein rangers imethibitisha kushiriki mashindano ya soka ya vijana chini ya miaka 17, yaliyopangwa kufunguliwa jumapili tarehe 09 Agost 2009 na Mwenyekiti wa chama cha soka Kinondoni (KIFA) ndugu Michael Lupyana kwenye uwanja wa Bubu Mburahati, Dar es salaam. Michuano hiyo itashirikisha timu 22 kutoka kata tofauti za wilaya ya Kinondoni.

Sunday, August 2, 2009

Said Suleiman


Mchezaji mpya wa shein rangers Said Suleiman.

Shein Rangers Vs Shekilango Boys


Timu ya shein rangers leo tarehe 02 Agost 2009 imecheza mchezo wake wa pili kupima wachezaji wake wapya na kuifunga Shekilango Boys goli 3 - 2, mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa sinza stars wafungaji kwa upande wa shein ni Amme Mohamedi goli la kwanza, Juma Mwalami (mchezaji mpya pichani juu)na goli la tatu lilitumbukizwa kimiani na Michael Philipo (mchezaji mpya).

Saturday, August 1, 2009

Shein Vs Sinza Stars

Timu ya shein rangers ikiwatumia wachezaji wake wapya watano imecheza mchezo wa kirafiki leo tarehe 01 Agost 2009 na timu ya sinza stars, matokeo ni sare ya goli 1 - 1 mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa sinza stars. Goli la shein lilifungwa na mchezaji mpya aitwaye Juma Mwalami. Mchezo huo ulikuwa maalumu kwa ajili ya kujaribu wachezaji wapya wa shein rangers.