Wednesday, September 30, 2009

TOFAUTI YA SOKA AFRIKA NA ULAYA INAANZIA HAPA
Hata ustaarabu wa wachezaji wa Afrika tofauti na wa Ulaya, tazama kwa makini mchezaji wa kiafrika anachokifanya uwanjani.

VIWANJA VYA SOKA AFRIKA
Hii ndio hali halisi kwa viwanja vya soka Afrika na ndipo wanapotoka wachezaji nyota waotamba ulaya. Hapa ndio mwanzo wa tofauti ya soka la Afrika na Ulaya.

Monday, September 28, 2009

SHEIN RANGERS NA KIJITONYAMA CHIPUKIZI


Timu za KIJITONYAMA CHIPUKIZI na SHEIN RANGERS SC (katika picha ya pamoja shein rangers jezi za bluu) terehe 27 Septemba zilicheza mchezo wa soka wa kirafiki ikiwa ni kuziweka sawa timu hizo zilizo katika maandalizi ya michezo yao, Kijitonyama Chipukizi inajiandaa na mchezo wake wa ligi ya TTF (W)Kinondoni na Shein Rangers inajiandaa na mchezo wake wa fainali MAMA HIDAYA CUP siku ya terehe 04 Oktoba 2009 siku ya Jumapili.

Wachezaji wa timu ya Kijitonyama Chipukizi(Jezi za kijani) wakisalimiana na wachezaji wa Shein Rangers kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya timu hizo zenye wachezaji wenye vipaji vya soka.

Wapenzi wa soka Sinza na Kijitonyama wakifatilia kwa makini pambano la kusisimua kati ya Shein Rangers na Kijitonyama Chipukizi. Katika mchezo huo Shein Rangers ilishinda bao 2 - 1 magoli yote ya Shein Rangers yalifungwa na mchezaji wake nyota na Timu ya Taifa ya vijana (Serengeti Boys) Murshid Ally moja kila kipindi.

Wednesday, September 23, 2009

MCHEZO WA NUSU FAINALI WAVUNJIKA
Picha tofauti za wadau wa soka Mburahati na Baadhi ya wachezaji na wapenzi wa Shein Rangers baada ya mchezo wa nusu fainali kati ya Shein na Kasuru FC kuvunjika kutokana na fujo zilizoanzishwa na wachezaji wa timu ya Kasuru FC baada ya kuzidiwa sana katika mechi iliyochezwa leo tarehe 23 Septemba 2009. Kutokana na fujo hizo timu ya Kasuru FC imeondolewa katika mashindano (kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo timu inayoanzisha fujo inaondolewa katika kashindano)na Shein Rangers imeingia moja kwa moja fainali na kukutana na Young Boys.Mpaka mchezo unavunjia dakika 26 kipindi cha kwanza matokeo yalikuwa 0 - 0.

Saturday, September 19, 2009

IDD NJEMA

SHEIN RANGERS INAWATAKIA WADAU WAKE WOTE AMANI FURAHA NA UPENDO KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA IDD.

EID MUBARAK!

KUTANA NA TOTO FC YA MIKOCHENI


Kamera ya Shein Rangers ilikutana uso kwa uso na timu ya watoto chini ya miaka 14 ya TOTO FOOTBALL CLUB YA MIKOCHENI "A", timu hii yenye maskani yake mitaa ya Mikocheni shule ya msingi inaomba misaada ya vifaa vya michezo kama mipira, jezi na viatu. Kama utapenda kuwasidia watoto hawa unaweza kuwasiliana na Blog hii moja kwa moja na utakutanishwa nao.

Friday, September 18, 2009

KOMBE LA KIFA LAENDELEA TEGETA

Wakazi wa Tegeta siku ya tarehe 15 Septemba 2009 walipata burudani safi katika mchezo mkali wa soka kombe la chama cha soka wilaya ya Kinondoni (KIFA)uliozikutanisha timu za Africana United na Vijana FC na kufunga na bao 1 - 1. Goli la Africana United lilifungwa na Magid Kwembe na la Vijana FC lilifungwa na Bakari Kalembo, mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa shule ya Sekondari Tegeta jijini Dar es salaam.

Wednesday, September 16, 2009

SHEIN RANGERS YAINGIA NUSU FAINALI

Timu ya shein rangers imeingia nusu fainali ya mashindano ya vijana chini ya miaka 17 MAMA HIDAYA CUP baada ya kuichapa timu ya Milambo FC ya mburahati jumla ya mabao 4 - 3. Dakika 90 za mchezo huo uliotawaliwa na vurungu toka kwa mashabiki wa Milambo zilimalizika kwa kufungana goli 1 - 1 ndipo sheria ya penati ilipotumika ili kupata mshindi atakayeingia nusu fainali. Shein ilipata penati 3 zilizofungwa na Said Issa a.k.a fella, Mrisho Juma na Miza Abdallah. Sifa za pekee kwa kipa namba moja wa shein rangers Saidi Mbegu aliyeokoa penati 3 katika mchezo huo wa robo fainali iliyochezwa tarehe 14 septemba 2009.

WAJUE MSEWE KIDS


Timu ya soka chini ya miaka 14 ya MSEWE KIDS FOOTBALL CLUB ilianzishwa mwaka 2007, maskani yake ni Ubungo Rombo Msewe na hufanya mazoezi yake katika uwanja wa Shule ya msingi Msewe na ipo chini ya kocha Willy.

Kwa mawasiliano:
Katibu Mkuu
0719 701135

WAJUE MAKUMBUSHO TALENTS FC


Timu ya watoto chini ya miaka 14 MAKUMBUSHO TALENTS FOOTBALL CLUB ilianzishwa mwaka 2001 chini ya kocha Khalid Athumani.
Timu hii inaomba misaada wa vifaa vya michezo kama mipira,jezi na madawa.

Kwa mawasiliano:
P.O Box 15759 Dar es salaam (T)
Simu 0754 571848

WAJUE KIJITONYAMA FOUNDATION SPORTS CLUB


Timu ya soka ya watoto chini ya miaka 14 ya KIJITONYAMA FOUNDATION SPORTS CLUB (KFSC) ilianzishwa mwaka 2009. Chini ya Kocha Rashid Omar Masoud.
Vikwazo vikubwa kwao ni uhaba wa vifaa kama jezi,bips,mipira na madawa.

Kwa mawasiliano:
0717 322597/0652 685402

WAJUE NEW VIPAJI FOOTBALL CLUB


Timu ya soka ya watoto chini ya miaka 14 NEW VIPAJI FOOTBALL CLUB nao wanashiriki Bonanza la soka la watoto linalofanyika sinza. Timu hii inapatikana Magomeni Mwembe Chai ikiwa chini ya kocha Athumani na Iddi Lila.

Kwa mawasiliano:
Katibu Mtendaji ndugu Mapambano Sisso
Simu 0717 759053

Sunday, September 13, 2009

MAANDALIZI YA ROBO FAINALI


Kocha mkuu wa Shein Rangers Rashid Said akiwa anaandaa program yake kwa ajili ya mechi ya robo fainali MAMA HIDAYA CUP siku ya tarehe 14 Septemba dhidi ya timu ya Milambo FC katika uwanja wa kwa Bubu Mburahati Jijini Dar es salaam.

NYOTA YA TANZANIA YAWAKA CANADA

Mchezaji nyota wa kimataifa wa Tanzania Nizar Khalfani anayecheza soka ya kulipwa nchini Canada katika timu ya White Caps anaendelea kufanya vizuri katika ligi ya Canada na anaendelea kung'alisha nyota ya Tanzania. Juu ni picha tofauti za Nizar siku walipocheza mechi ya ligi na timu ya Miami picasa nchini Canada (Picha kwa hisani ya Salum Omary wa Orange Football Academy Zanzibar)

SHEIN RANGERS YAITANDIKA MIDIZINI FCLeo tarehe 13 Septemba 2009 timu ya Shein Rangers imeitandika timu ya Midizini toka Manzese Midizini mabao 3 - 0. Magoli yote ya Shein yalifungwa na muuwaji wao mahili Mahalaji Lal Bulu, mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Kinesi Urafiki jijini Dar es salaam. Midizini inajiandaa na ligi ya TFF (W) Kinondoni iliyoanza mapema wiki hii.

BONANZA LA SOKA SINZA
Bonanza la soka kwa watoto chini ya miaka 14 sinza limevutia wadau wengi wa soka wa maeneo ya sinza kutokana na vipaji vya hali ya juu toka kwa watoto.

BONANZA LA SOKA YA WATOTO SINZA LAFANA


Katibu wa chama cha michezo kwa watoto Wilaya ya Kinondoni (KIDYOSA) Mzee Mwinyi Tambaza akikagua wachezaji wa chini ya miaka 14 wa Timu ya Makumbusho Talent (jezi nyeupe) na Kijitonyama Foundation Sports Club (KFSC) jezi za njano. Katika bonanza la soka la watoto katika uwanja wa SINZA STARS.

Friday, September 11, 2009

KUTANA NA MABINGWA WA UHAI CUP 2009


Timu soka ya vijana chini ya miaka 20 ya Azam ndio mabingwa wa UHAI CUP 2009 kombe lililokuwa linashirikisha vikosi vya pili vya timu za ligi kuu ya soka Tanzania.

Tuesday, September 8, 2009

KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTER (KCSC)


Kituo cha kukuza michezo cha KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTER cha Kijitonyama jijini Dar es Salaam kimeingiza timu yake ya soka katika ligi ya TFF Wilaya ya Kinondoni kwa mara ya kwanza. Kwa sasa timu ipo katika maandalizi kabambe katika uwanja wao wa mazoezi Shule ya Msingi Kijitonyama Kisiwani, KCSC itaanza mchezo wake wa kwanza tarehe 19 Septemba 2009 kwa kuonyeshana ubavu na Mchangani FC katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B.

Taarifa hii
Na: Chris Fidelis
Kwa niaba ya Uongozi wa KCSC

Sunday, September 6, 2009

SHEIN YATINGA ROBO FAINALI

Timu ya Shein Rangers imetinga robo fainali ya mashindano ya vijana chini ya miaka 17 (Mama Hidaya Cup) baada ya wapinzani wao Canon FC kuingia mitini katika mechi iliyokuwa ichezwe leo tarehe 06 Septemba 2009 na Shein kupewa magoli mawili na point tatu na kuongoza kundi lake. Baada ya Canon FC kuingia mitini Shein Rangers ilicheza na wenyeji wa mashindano hayo Young Boys mechi ya kirafiki na matokeo Shein ilishinda 3 - 1 Magoli ya Shein yakifungwa na Nassoro Udulele, Saidi Issa (fela) na Adrian Selestine (banka).

Saturday, September 5, 2009

PONGEZI KWA YASINTA NGONYANI


Shein Rangers inampongeza dada yetu Yasinta Ngonyani pamoja na Blog yake ya MAISHA kwa kuifatilia kwa karibu SHEIN RANGERS. Unataka kujua zaidi kuhusu MAISHA? kutana na MWAFRIKA HALISI ingia www.ruhuwiko.blogspot.com

KUMBUKUMBU


Picha ya kumbukumbu viongozi, makocha, wachezaji na wapenzi wa shein rangers siku walipokipiga na timu ya TSA katika uwanja wa kumbukumbu wa Karume unaomilikiwa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Wednesday, September 2, 2009

SHEIN DRAW AT HOME

It was feisal who make the lead for most wanted.
Mooneyr made a cross and feisal with an easy finish for the ball in to the net before shein equalize 20 minutes later. Shein had a poor performance today and let most wanted dominate the game

PLAYERS RATING FOR MOST WANTED SIDE

Muntasir 8
He was good on the goal

Faza 8
He was absolute good

David 7
He was a little bit tired but good

Said 8
He made a good clearance

Samir 8
he was in his possesion no mistake made by him

Ebraheem 8
He had a good performance today

Medy 7
He had a wonderful second half

Nassor(zinja) 8
Good passes came from him

Feisal(zlatan) 9
He is man of the match with a wonderful goal from him

Suleiman(boga) 8
He is absolutely the best of game

Mooneyr 8
He made a good crosses which introduces a goal for most wanted

SUBSTITUTES
Hamees 7
He was good and dominates the game

MOST WANTED Vs SHEIN RANGERS

There will be a biggest game for most wanted who are depending in their best players

Mooneyr: will have a good start against his home team he is amazing skiper

Feisal: they probaly call him zlatan for his ability of scoring and managing the game

Samir: he play like jammie Carragher the liverpool centre half no doubt about him he is the best

Muntasir: he is the record keeper, this goalkeeper had never being allow a goal in one against one he is the best either

Ebraheem: he is not a player but number one most wanted fan hope he will have a good time today