Friday, October 30, 2009

SHEIN RANGERS KUSAKA NYOTA WAPYA

Timu ya Shein Rangers imeamua kuwagawa watoto waliojitokeza katika usaili katika makundi manne (timu nne), na kuzishindanisha kupata timu bingwa na pia kutafuta wachezaji nyota watakaounda kikosi cha pili (U - 14) cha Shein Rangers Sports Club.
Mashindano hayo ya siku mbili yatafanyika kwa mtindo wa ligi na kila timu itacheza mechi tatu, timu mbili za juu zitacheza fainali ili kupata bingwa. Mechi zitaanza siku ya tarehe 31 Oktoba 2009 saa nne asubuhi katika uwanja wa T.P. Africa Sinza.

Wapenzi wote wa soka la vijana wanakaribishwa!

Taarifa hii imetolewa,
Na Rashi Said (Kocha mkuu)
Shein Rangers Sports Club " THE HAMMER "

Sunday, October 25, 2009

SHEIN RANGER YAMALIZA WIKI KWA RAHA

Timu ya Shein Rangers imemaliza wiki kwa raha ya aina yake baada ya timu zake za wakubwa na watoto kufanya vizuri katika michezo yao ya kirafiki. Siku ya tarehe 24 Oktoba 2009 timu ya Shein Rangers chini ya miaka 17 ilicheza na timu ya FC Milan ya Kigogo na matokeo kuwa 3 - 3. Na siku ya tarehe 25 Oktoba 2009 timu ya Shein Ranger chini ya miaka 17 ilifunga Sinza Stars goli 2 - 0 vile vile timu ya Shein Rangers chini ya miaka 14 ilifundisha soka timu ya Sinza Stars chini ya miaka 14 kwa kuichapa bao 2 - 0 pia, michezo yote ilichezwa uwanja wa T.P. Africa Sinza.

KUNDI LA KWANZA LAANZA VIZURI MAJARIBIOKundi la kwanza la watoto waliokuwa katika majaribio ya kujiunga na timu ya Shein Rangers chini ya miaka 14 wameanza vizuri mchezo wao wa kwanza wa majaribio baada ya kuifunga timu ya watoto ya Sinza Star chini ya Kocha Zagalo bao 2 - 0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa T.P. Africa Sinza.

Friday, October 23, 2009

MICHEZO YA KIRAFIKI

Timu ya Shein Rangers itakuwa na michezo miwili ya kirafiki mwishoni mwa wiki hii siku ya tarehe 24 Oktoba 2009 na 25 Oktoba 2009.Michezo hiyo itafanyika katika uwanja wa T.P. Africa Sinza.

Monday, October 19, 2009

MWENYEKITI KIFA AIPONGEZA SHEIN RANGERS


Mwenyekiti wa chama cha soka Wilaya ya Kinondoni (KIFA) Ndugu Michael Rupiana akitoa pongezi kwa timu ya Shein Rangers kwa kutwaa ubigwa wa mashindano ya soka ya vijana, pamoja na pongezi hizo alikabidhi seti moja ya jezi kama zawadi kwa mshindi.

Sunday, October 18, 2009

MTANZANIA HENRY JOSEPH APEPERUSHA VIZURI BENDERA YA TAIFA

Mtanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Norway Henry Joseph anapeperusha vizuri bendera ya taifa baada ya kupata namba katika kikosi cha kwanza katika timu yake ya Kongsvinger FC. (Picha kwa hisani ya Salum Omary wa Orange Fooball Academy Uholanzi/Zanzibar)

CHIPUKIZI KUSHIRIKI BONANZA LA SOKA


Timu ya kikosi cha pili ya kituo cha michezo cha KIJITONYAMA CHIPUKIZI (KCSC)ipo katika maandalizi ya bonanza kubwa la soka litakalofanyika tarehe 31 Oktoba 2009 katika viwanja vya kawe.

BONANZA LA SOKA


Kocha wa timu ya Sinza Star Zagalo akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa bonanza la watoto linaloendelea kila mwisho wa wiki sinza.

Tuesday, October 13, 2009

USAILI SHEIN RANGERS UNAENDELEA


Pichani kocha mkuu wa Shein Rangers Rashid Said akiwaeleza watoto nini anataka kuona toka kwao wakati wa usaili wa timu ya watoto wa Shein Rangers Sports Club.

Monday, October 12, 2009

WATOTO WAZIDI KUJITOKEZA KATIKA USAILI


Watoto wazidi kujitokeza katika usaili Shein Rangers kutafuta watoto wenye vipaji kwa ajili ya kucheza timu ya watoto chini ya miaka 14 (U - 14), usaili huo utaendelea mpaka tarehe 21 Oktoba 2009.

Saturday, October 10, 2009

SHEIN RANGERS Vs MIDIZINI FC


Kikosi cha timu ya Shein Rangers kilichopambana na Midizini FC inayonolewa na kocha maarufu wilaya ya Kinondoni mzee Mwinyimadi Tambaza na kufungana 2 - 2. Magoli yote ya Shein yalifungwa na Murshid Ally. Mchezo huo wa kirafiki ulifanyika katika uwanja wa Kinesi urafiki jijini Dar es salaam leo tarehe 10 Oktoba 2009.

Thursday, October 8, 2009

TIMU YA SHEIN KUFANYA USAILI WA WACHEZAJI CHINI YA MIAKA 14

Timu ya soka ya Shein Rangers itafanya usaili kutafuta wachezaji wapya chini ya miaka 14 kwa ajili ya kujenga upya kikosi cha pili cha Shein Rangers. Usaili huo na mchujo utafanyika kwa kipindi cha wiki mbili katika uwanja wa TP Africa Sinza. Usaili Utafanyika kuanzia tarehe 07 Oktoba 2009 mpaka 21 Oktoba 2009. Mzazi ama mtu yoyote kama utapenda mwanao acheze soka la kisasa usisite kumleta mtoto wako katika uwanja wa TP sinza.

Kwa Mawasiliano zaidi.
E.mail:- shein.rangersfc@yahoo.com
Mob Number:- 0717 294876 (Kocha Mkuu Shein Rangers Sports Club)

WATOTO WAKUTANA NA MCHEZAJI WA KIMATAIFA WA SHEIN


Mchezaji wa timu ya Taifa ya soka ya vijana ya Tanzania (Serengeti Boys) na Shein Rangers Murshid Ally akiwapa moyo wachezaji wa umri chini ya miaka 14 waliojitokeza katika usaili kwa ajili ya timu ya watoto ya Shein Rangers.

Wednesday, October 7, 2009

PONGEZI ZAMIMINIKA SHEIN RANGERS

Baada ya timu ya Shein Rangers ambao ndio mabingwa wa soka kata ya Sinza 2009 kutwaa ubingwa wa soka vijana kata ya Mburahati MAMA HIDAYA CUP 2009 pongezi toka kwa wadau mbalimbali wa soka zimeendelea kumiminika,kwa njia ya simu, barua pepe na comments kupitia blog ya Shein Rangers.

Asanteni Sana kwa kutuunga mkono.
SHEIN RANGERS SPORTS CLUB

Monday, October 5, 2009

SHEIN BINGWA NA MBEGU NYOTA WA MCHEZO
Timu ya Shein Rangers imetwaa ubingwa wa MAMA HIDAYA CUP 2009 kwa kuichapa Young Boys goli 2 - 1. Mashindano ya vijana yalishilikisha timu kumi na mbili na Shein kutwaa ubingwa bila ya kupoteza mchezo wowote.
Katika mchezo huo wa fainali golikipa namba moja wa Shein Rangers Said Mbegu pichani kulia alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuokoa michomo mikali.

SAFARI YA UBINGWA ILIANZIA HAPA


Safari ya timu ya Shein Rangers kwenda kucheza fainali na kutwaa ubingwa wa MAMA HIDAYA CUP 2009 ilianzia hapa, pichani hapo juu ni wachezaji wa Shein Rangers wakiwa katika maandalizi ya mchezo huo wakiwa klabuni kwao.

SHEIN IKIINGIA UWANJANI


Wachezaji wa Shein Rangers wakishuka kwenye Basi maalum lililowapeleka uwanjani.

WACHEZAJI WAKIPASHA JOTO MIILI YAO


Wachezaji wa Shein Rangers wakipasha joto miili yao kabla ya kuanza mchezo wa fainali na timu ya Young Boys ya Mburahati katika mashindano ya vijana MAMA HIDAYA CUP 2009.

UKAGUZI


Timu ya Young Boys jezi nyekundu na Shein jezi za bluu bahari zikikaguliwa kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali.

SHAMBULIZI


Mshambuliaji wa Shein Rangers Ibrahim Juma Kombo (jezi namba 9) akipeleka mashambulizi langoni kwa Young Boys, Shein Rangers Sports Club ilishinda 2 - 1 na kuwa mabingwa wa MAMA HIDAYA CUP 2009.

WACHEZAJI WA AKIBA WAKIFATILIA MCHEZO


Wachezaji wa akiba wa Shein Rangers wakifatilia mchezo wa faina kwa makini.

WACHEZAJI WAKIFURAHIA UBINGWA


Wachezaji wa Shein Rangers wakifurahia ubingwa baada ya kuichapa timu ya Young Boys ya Mburahati goli 2 - 1 katika mchezo mkali wa fainali magoli ya Shein Rangers yalifungwa na Kiungo wake mahili Mussa Chubwi na Mshambuliaji wake mkali Michael Philipo.

NAODHA WA MABINGWA AKIPOKEZA ZAWADI


Naodha wa mabingwa wapya wa MAMA HIDAYA CUP 2009 timu ya Shein Rangers Amme Mohamed akipokea zawadi ya ushindi wa kwanza (jezi seti moja).

MGENI RASMI AKIWAPONGEZA MABINGWA


Mgeni rasmi katika fainali hiyo mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya kinondoni (KIFA) ndugu Michael Rupiana akitoa pongezi kwa Shein Rangers pamoja na kutoa zawadi kwa timu zote zilizofanya vizuri, kulia kwake ni Mjumbe wa SHINA No 22 KATA YA MBURAHATI mama Hidaya ambaye ndio muandaaji wa mashindano hayo ya MAMA HIDAYA CUP 2009.

Friday, October 2, 2009

MAANDALIZI YA FAINALI YANAENDA VIZURI

Timu ya Shein Rangers inaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo wake wa fainali na timu ya Young Boys ya Mburahati,mchezo huo utachezwa jumapili ya tarehe 04 Oktoba 2009. Wachezaji waliokuwa majeruhi wanaendelea vizuri na mwalimu anaweza kuwatumia siku ya fainali, majeruni ni Maharaji Lal Bulu, Nassoro Udulele na Munir.