Monday, November 30, 2009

HENRY JOSEPH MAJUU


Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Henry Joseph Shindika anaendelea vyema kupeperusha bendera ya Tanzania na Timu yake imefanikiwa kupanda ligi kuu.

UHAI CUP 2009 YAANZA KWA KISHINDO


Mashindano ya soka kwa timu za vijana chini ya miaka 20 za ligi kuu Tanzania bara yameanza kwa kishindo baada ya timu ya Moro United kuicha JKT Ruvu ya Pwani bao 7 - 1. Timu ya vijana ya Azam ndio bingwa mtetezi.

TANZANIA YALALA 2 - 0


Tanzania bara yaanza vibaya kwa kukubali kipigo cha bao 2 - 0 toka kwa Uganda katika mashindano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kwa Chalenji Cup.

TANZANIA NA GHANA


Tanzania (Taifa Star) siku ilipokutana na Ghana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa kirafiki mapema mwaka huu na matokeo yalikuwa 1 - 1.

TAMASHA LA WATOTO YATIMA LAFANA


Tamasha la michezo mbalimbali lililoshirikisha vituo tofauti vya watoto yatima lafana jijini Arusha, tamasha hilo liliandaliwa na wafanyakazi wa Vodacom Arusha.

PONGEZI KWA HADIJA MALOYA


Uongozi wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB unatoa pongezi kwa dada yetu Hadija Maloya kwa kuifatilia blog hii kwa karibu pamoja na kutoa ushauri na comment kila mara anajulikana zaidi kwa jina la "MKWE"

WAKUSHI WALALA KWA SINZA STARS

Timu ya Wakushi FC ya Sinza Palestina imekubali kipigo cha bao 1 - 0 toka kwa sinza stars katika mchezo wa ligi ya TFF wilaya ya Kinondoni siku ya tarehe 29 Novemba 2009 katika uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam.

IDD AL HAJI

Timu ya Shein Rangers wakati wote wa sikukuu ya iddi al haji ilitoa mapumziko kwa wachezaji wake, hakukua na mechi wala mazoezi na tunashukuru mungu mazoezi yameanza leo tarehe 30 Novemba 2009 wachezaji na viongozi wote wapo salama.

Monday, November 23, 2009

JUHUDI FC YAVUNJA MWIKO WA SHEIN

JUMAPILI TEREHE 22 NOVEMBA 2009
Timu ya Shein Rangers imepoteza mchezo wa pili toka mwaka huu uanze na mchezo wa kwanza kupoteza nyumbani toka mwaka huu uanze. Timu ya Shein Rangers ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Juhudi FC na kufungwa 3 - 2 katika uwanja wake wa nyumbani.
Juhudi FC ndio timu ya kwanza kuifunga Shein Rangers nyumbani mwaka huu 2009.

JUMAMOSI TAREHE 21 NOVEMBA 2009
Timu ya Shein ilicheza na Vijana ya Tandika na Shein ilishinda 4 - 1 katika uwanja wa T.P Afrika Sinza.

IJUMAA TEREHE 20 NOVEMBA 2009
Shein ilikuwa icheze mechi ya ligi ya KANUNI CUP na Sinza Stars, sinza star hawakutokea uwanjani na shein kupata point tatu za chee na mabao mawili.
Hata hivyo shein ilicheza mchezo wa kirafiki na Wazwazwa ya Mburahati na shein kushinda bao 2 - 1.

Friday, November 20, 2009

KOMBE LA DUNIA LATUA TENA TANZANIAKombe la FIFA la Soka la Dunia limetua nchini Tanzania kwa mara ya pili katika historia yake hapa duniani,juu ni picha tofauti za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete alipolizindua katika uwanja mpya wa Taifa na pia alitumia nafasi hiyo kuwafumbua macho viongozi wa TFF kuacha kukombatia timu kubwa na badala yake kuwekeza katika soka la vijana na watoto.

TWALIPO YOUTH SOCCER FOUNDATION (TYSF) NDANI YA TOVUTI


Hizi ni picha tofauti za watoto wa Kituo cha kukuza soka cha TWALIPO YOUTH SOCCER FOUNDATION cha Jijini Dar es salaam kinachomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania. Chini ya mwalimu wa soka Maj Bakari.Kituo hicho kimetengeneza tovuti yake kwa habari zaidi tembelea www.twalipoyouthsoccerfoundation.com

Thursday, November 19, 2009

MWALIMU NA VIFAA


Kocha mkuu wa Shein Rangers Rashid Said akiwa katika moja ya maduka ya vifaa vya michezo alipoenda kuchukua vifaa vya michezo.

WALIOPITA USAILI SHEIN WAANZA MAZOEZI


Wachezaji wa umri chini ya miaka 14 waliopita katika usaili wa timu ya Shein Rangers Sports Club wameanza rasmi mazoezi kwa ajili ya kutengeneza timu mpya ya watoto.

Wednesday, November 18, 2009

Player Information For MURSHID ALLY RASHID

Personal Details
Full name Murshid Ally Rashid
Age17 years old
Membership ID46852
Location Yorkshire
Nationality Tanzanian
Current level Semi pro
Wants trials at Premiership

Physical Attributes
Dominant foot Both
Height5' 6''
Weight10 st 1 lbs
Speed More Quick

Preferred Positions
Forward/Left winger/Right winger

Career To Date
I learned to play football in the street in Tanzania aged seven . When Iwas 14 i joined Shein Rangers Sports Club (check on www.sheinrangers.blogspot.com), in Dar es salaam and between 2006 and 2009 I palyed in 109 games, scoring 74 goals. I was selected to play at district and regional levels, then i joined the Tanzania Natonal football team and I have played 13 friendly match and 6 league with Malawi,Nigeria , Kenya, Namibia, Ethopia and Africa Invatations team,in June 2009 I was Selected to play in the Copa Coca Cola intarnational tournarment in South Africa and as a result iwas chosen be one of the eight highly ranked under 17 players in Africa. Our National team got a 3rd place. Right now I am playing for Azam football club in Dar es Salaam.

Trials To Date
I have taken part in five Trials in Tanzania for Shein Rangers Sports Club, the districkt and regional teams,Azam football Club and U 17 National team. I hope to attend my first Trial in the uk, in December

How To Contact This Player
Click here to contact this player via www.footballcv.com

TAARIFA HIZI ZIMENASWA NA BLOG HII TOKA MTANDAO WA www.fooballcv.com WA UINGELEZA.

SHEIN RANGERS YAANZA KWA SALE

Timu ya Shein Rangers imeanza kwa sale ya bila kufungana na timu ya Eagle Fry ya Mburahati katika mchezo mgumu wa mashindano ya KANUNI CUP 2009. Mchezo huo ulichezwa tarehe 16 Novemba 2009 katika uwanja wa Bubu Mburahati, shein itajitupa tena uwanjani tarehe 20 Novemba 2009 na Sinza Star katika uwanja huo huo.

Taarifa hizi na:-
Rashid Said (Kocha mkuu Shein Rangers Sports Club)

ABAJALO YAJITOA LIGI YA TFF

Timu ya soka ya Abajalo ya Sinza imejitoa katika mashindano ya ligi ya TFF Wilaya ya Kinondoni, kujitoa kwao kuizawadia point tatu za chee mahasimu wao Sinza Stars na kushika nafasi ya pili katika kundi lao.

Monday, November 16, 2009

KANUNI CUP 2009

Uongozi wa mashindano ya KANUNI CUP 2009 umeiomba radhi timu ya Shein Rangers kwa kitendo cha kuwakataa baadhi ya wachezaji wao na kuiomba ishiriki mashindano yao kama awali bila ya masharti yoyote.

SHEIN RANGERS UFUKWENI


Timu ya Shein Rangers ilipokuwa mapumzikoni katika pwani ya bahari ya hindi mapema mwaka huu.

KUTANA NA "KIDUME" SHEIN RANGERSMtoto Ramadhani Kilindo mwenye umri wa miaka 6 amekuwa kivutio katika mazoezi ya timu ya watoto chini ya miaka 14 ya Shein Rangers,Ramadhani maarufu kwa jina la " Kidume" katika picha zake tofauti akiwa mazoezini, moja ya sifa zake ni mbio na kutokata tamaa na kila jambo anata kujaribu na kuweza. Mambo yake ni kivutio tosha mazoezini, huyo ndio KIDUME kama wenzake wanavyomwita.

SHEIN MAZOEZINI


Timu ya Shein Rangers ikiwa katika mazoezi yake ya kawaida katika uwanja wa TP Sinza.

Wednesday, November 11, 2009

MAZOEZI YAENDELEA SHEIN RANGERS

Timu ya Shein Rangers baada ya kujitoa katika mashindano ya KANUNI CUP 2009 kutokana na mizengwe, inaendelea na mazoezi yake ya kawaida kila siku jioni katika uwanja wa T.P. Africa Sinza.

Taarifa hii kutoka Uongozi wa Shein Rangers Sports Club.

Sunday, November 8, 2009

KOMBE LA BARCLAYS LAVUTIA WENGI DAR


Kombe la Barclays Premier League (Ligi kuu nchini Uingereza) lililopo hapa nchini kwa ziara maalum limevutia wapenzi wengi wa soka Jijini Dar es salaam.

SHEIN RANGERS YAJITOA KANUNI CUP

Timu ya Shein Rangers Sports Club leo tarehe 08 Novemba 2009 imeamua kujitoa katika mashindano ya soka ya KANUNI CUP 2009 baada ya wachezaji wake watano kukataliwa kucheza mashindano hayo kwa hila.

Taarifa hii na:- Uongozi wa Shein Rangers Sports Club

Friday, November 6, 2009

VIDEO YA NYOTA WA SHEIN YATAMBA AFRIKA

Video iliyoshirikisha wachezaji nyota katika mashindano ya copa coca cola Afrika Kusini (mwaka huu) iliyoshirikisha mchezaji wa Shein Rangers na Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania Murshid Ally pamoja na vijana kutoka nchi za Ethiopia, Zambia, Kenya, Uganda, Namibia, Zimbabwe na Afrika Kusini inatarajiwa kuonyeshwa kupitia vipindi vya Televisheni barani Afrika na Ulaya. Meneja wa masoko coca cola Afrika Mashariki na Kati kanda ya Tanzania Rita Tsehai aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Video hiyo ilifanyika sehemu tofauti, kuanzia Afrika kusini yalipokuwa mashindano hayo na kufika mpaka Sinza anapoishi mchezaji huyo pamoja na Zanzibar pia video hiyo ilihusisha timu yake aliyokulia ya Shein Rangers Sports Club pamoja na mwalimu wake toka utoto wake (Rashid Said)na wachezaji wenzake wa Shein Rangers.

MATUKIO TOFAUTIMatukio tofauti ya Murshid Ally alipokuwa Afrika Kusini katika michezo ya coca cola mapema mwaka huu.

WAKATI WA UTENGENEZAJI WA VIDEO HIYOWaandaaji wa video inayoonyesha mashujaa wa Afrika wa mashindano ya vijana wa copa coca cola nchini Afrika Kusini, video hiyo ilishirikisha wachezaji wote wa Shein Rangers.

Wednesday, November 4, 2009

SHEIN RANGERS KUSHIRIKI KANUNI CUP

Timu ya Shein Rangers imethibitisha kushiriki mashindano ya soka KANUNI CUP 2009. Mashindano hayo yanashirikisha timu za soka toka Sinza, Manzese na Mburahati, na Shein Rangers itaanza mechi yake ya kwanza siku ya tarehe 08 Novemba 2009 katika uwanja wa Bubu mburahati. Ratiba kamili ya mashindano hayo itatolewa baadae.

Tuesday, November 3, 2009

ZENGWE BONANZA LA SOKA KAWE

UONGOZI WA KCSC UMEPOKEA TAARIFA ZA KUKATISHA TAMAA KWA BAADHI YA VIONGOZI WA KIFA KUITOA TIMU YETU NA ZINGINE NA KUZIINGIZA TIMU ZA MITAANI WANAZOZITAKA WAO HILI ZICHUKUE ZAWADI NONO ZA AWALI,HIVI NINAVYOKUANDIKIA BONANZA LINAENDELEA KAWE.

TAARIFA HII IMETUMWA KWA NJIA YA MTANDAO TOKA
KITUO CHA MICHEZO CHA KIJITONYAMA CHIPUKIZI (KCSC)
SIKU YA TAREHE 31 OKTOBA 2009.

MASHINDANO YA WATOTO YAFANA


Mashindano ya siku mbili ya kusaka wachezaji nyota yafana na kusifiwa na wadau wengi wa soka waliotoa maoni tofauti. Mashindano hayo yalishirikisha timu nne zote za Shein Rangers chini ya miaka 14 na yalikuwa ya siku mbili tarehe 31 na 01 Oktoba 2009.

WADAU WA SOKA


Wadau wa soka wakifatilia mashindano ya watoto ya kusaka wachezaji nyota wa Shein Rangers chini ya umri miaka 14.

UFUNGUZI


Mdau wa Soka toka TAUFIQ COMMISSION AGENT AND TAUFIQ MOTORS AND GENERAL SERVICES waliopo Sinza Moli ndugu Mohamed Seif akipiga penati na kumfunga kipa namba moja wa Shein Rangers Said Mbegu katika ufunguzi mashindano hayo siku ya tarehe 31 Oktobar 2009 katika uwanja wa T.P Africa Sinza.

MGENI RASMI ATOA ZAWADI


Mgeni rasmi aliyefungua mashindano hayo ndugu Mohamed Seif alitoa zawadi ya mpira na alitoa maji ya kunywa kwa wachezaji wote kwa siku mbili za mashindano hayo.

MGENI RASMI AKIKAGUA TIMU SIKU YA UFUNGUZIMgeni rasmi katika mashindano ya kusaka nyota wapya wa Shein Rangers ndugu Mohamed Seif toka kampuni ya uuzaji wa magari ya TAUFIQ COMMISSION AGENT AND TAUFIQ MOTORS AND SERVICES akikagua timu siku ya funguzi wa mashindano.

WASHINDI WA PILI


Timu ya World Stars iliyokuwa ikongozwa na Victor Wenslaus (figo) wa kwanza kushoto waliosimama na Maharaj Lal Bulu (hayupo pichani) ambao wote ni wachezaji wa Shein Rangers ilishika nafasi ya pili katika mashindano hayo.

UKAGUZI


Mgeni rasmi wa mchezo wa pili ndugu Yusuf Tall akikagua timu katika mchezo wa pili siku ya ufunguzi.

NASAA KWA WACHEZAJI


Mgeni rasmi wa mchezo wa pili kati ya Winners na World Stars akitoa nasaha baada ya ukaguzi wa timu zote.

MABINGWA


Timu ya Lyon Star iliyokuwa chini ya Mkude (wa kwanza kulia) ambaye ni mchezaji wa Shein Rangers iliibuka bingwa wa mashindano hayo. Wa kwanza kushoto waliosimama ni mwamuzi wa pambano hilo Miza Abdalah ambaye pia ni mchezaji wa Shein Rangers.

WAFUNGAJI BORA


Wafungaji bora katika mashindano hayo kila mmoja alifunga magoli matatu katika mechi nne walizocheza, kushoto ni Mbaraka Erick kulia ni Mussa wakiwa na kocha Chid.

FURAHA YA UBINGWA


Wachezaji na kiongozi wao wakifurahia ubingwa wa mashindano ya majaribio kwa wachezaji wa Shein Rangers chini ya miaka 14.

NAODHA AKIPOKEA ZAWADI


Naodha wa mabingwa Hussein Rashid akipokea zawadi ya soda toka kwa kocha mkuu, kwa ajili ya mabingwa wa wiki ya kwanza ndani ya Shein Rangers.

Monday, November 2, 2009

KINGS STAR


Timu iliyojiita Kings Star iliyoongozwa na Said Mbegu (wa kwanza kulia aliyesimama) ambaye ni kipa namba moja wa timu ya Shein Rangers, Kings Star haikufanikiwa kufika fainali.

NAODHA BORA


Mchezaji Hussein Rashid ndio aliibuka kuwa naodha bora wa mashindano hayo ya vikosi vinne vya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB chini ya miaka 14 (U - 14), pichani akiwa na kocha mkuu wa Shein Rashid Said.