Tuesday, December 29, 2009

MAANDALIZI YA MCHEZO WA LIGI YAENDELEA
Maandalizi ya mchezo muhimu wa ligi ya KANUNI CUP 2009 yanaendelea vizuri, Shein Rangers inahitaji sare ya aina yoyote ile ili kuweza kuingia robo fainali.

Monday, December 28, 2009

X - MASS IMEISHA SALAMA

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB iliyokuwa katika mapumziko ya sikukuu ya krismasi imeanza mazoezi yake leo katika uwanja wa TP Africa Sinza, kujiandaa na mchezo wake wa ligi ya KANUNI CUP siku ya tarehe 31 Dec 2009.

Tunashukuru tupo salama na tunawatakia wadau wote wa Shein Rangers kufika mwaka mpya 2010 kwa Amani na Upendo.

YANGA WAFALME WA TUSKER 2009Timu ya Yanga imetwaa ubingwa wa TUSKER CUP 2009 kwa kuichapa SOFAPAKA ya kenya bao 2 - 1. Pichani juu Waziri wa Michezo na Utamaduni, George Mkuchika akimkabidhi kombe nahodha wa Yanga Abdi Kassim katikati rais wa TFF Leodegar Tenga akishuhudia.Picha ya chini wachezaji na viongozi wakisheherekea ubingwa.

KIJITONYAMA CHIPUKIZI YATOA POLE KWA SHEIN

Ndugu,
YAH:MSIBA WA MMOJA WA KIONGOZI WENU. Husika na kichwa cha habari hapo juu.

Uongozi wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya Msiba wa Kiongozi aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Utawala wa timu yenu Bw Amani Marwa aliyefariki dunia tarehe 17 mwezi huu,Tumepata habari hizi jana usiku kwa kupitia Blog yenu,Sisi wana Kijitonyama Chipukizi tulimfahamu Bw,Marwa kwa kupitia Bonanza la Vijana wa U-14 lililoandaliwa na KIDIYOSA na kufanyikia katika uwanja wa kinesi na.2 ambapo yeye alikuwa Mgeni rasmi, Tunakumbuka siku ile timu yetu ilipoteza mpira yeye palepale alijitolea Mpira wa kwake, Tutamkumbuka marehemu kwa kuwa alikuwa mpenda Michezo,Mcheshi na alikuwa mtu wa kila mtu . Tunamalizia kwa kusema poleni sana wana Shein Ranger F.C wote. Mungu amlaze Mahali Pema Peponi .

CHRIS FIDELIS.kny UONGOZI NA WACHEZAJI WOTE WA KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C

Viambatisho:-
PICHA ZA BONANZA LA KIDIYOSA.

MAREHEMU AMANI MARWA AKITOA MPIRA KWA KCSC


Pichani Marehemu Amani Marwa akitoa zawadi ya mpira kwa mchezaji wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre wakati wa bonanza la KIDIYOSA, kulia ni katibu wa KIDIYOSA mzee Mwinyimadi Tambaza (Picha hii kwa hisani ya Kijitonyama Chipukizi Sports Centre)

SOFAPAKA


Mabingwa wa soka wa Kenya SOFAPAKA timu iliyoleta msisimko katika jiji la Dar es salaam,ijue maana ya (SOFAPAKA) SOTE (kama) FAMILIA (kwa) PAMOJA KUAFIKIA AZIMIO ndio kirefu cha SOFAPAKA, klabu ya soka iliyoanzishwa kutoka na timu ndogo ya kanisa la M.A.O.S Ministries jijini Nairobi chini ya usimamizi wa Pastor Jimmy Carter Ambajo mwaka 2002.

Wednesday, December 23, 2009

HERI YA KRISMAS

TIMU YA SHEIN RANGERS SPORTS CLUB INAWATAKIA WADAU WAKE WOTE HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA.

Monday, December 21, 2009

Sunday, December 20, 2009

MABINGWA WA UHAI CUP 2009/2010


Timu ya Azam United chini ya miaka 20 imetetea ubingwa wake wa UHAI CUP kwa kuichapa Simba 3 - 1. Katika mashindano ya timu za vijana chini ya miaka 20 kutoka katika timu zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania.

SAFARI YA MWISHO

Mwili wa marehemu Amani Marwa aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi na utawala wa Shein Rangers umesafirishwa leo Asubuhi kwenda mkoani Mara kwa mazishi.

Mungu Iweke Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amen!

Friday, December 18, 2009

TANZIA


Uongozi wa Shein Rangers Sports Club kwa masikitiko makubwa unapenda kutangaza kifo cha mmoja ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo ndugu Amani Marwa kilichotokea ghafla nyumbani kwake Sinza Karibu na uwanja wa TP siku ya tarehe 17 Desemba 2009. Msiba upo nyumbani kwa wazazi wake Sinza Afrika Sana. Picha juu marehemu Amani akisalimiana na Damian wa Afrika Kusini wakati walipokuja kutengeneza video za wachezaji bora wa coca cola Afrika mapema mwaka huu.

Wednesday, December 16, 2009

MAZOEZI


Timu ya Shein Rangers Sports Club inaendelea na mazoezi yake ya kawaida kila siku katika uwanja wa TP Sinza.

Monday, December 14, 2009

AZAM BINGWA TENA


Timu ya Azam United chini ya miaka 20 imeichapa Simba Sports Club chini ya miaka 20 bao 3 - 1 na kuwa mabingwa wa UHAI CUP kwa mwaka wa pili mfululizo.

Sunday, December 13, 2009

SINZA STAR YALALA TENA


Timu ya Sinza Star chini ya miaka 14 (jezi za njano) wamelala tena mbele ya watoto wenzao wa Shein Rangers bao 2 - 0, picha hii ilipigwa baada ya mchezo huo wakiwa pamoja na Shein Rangers (jezi bluu bahari).

MECHI YA WATOTO TWALIPO


Timu ya chini ya miaka 17 ya Shein Rangers Sports Club wakifatilia mechi ya wadogo zao chini ya miaka 12 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Twalipo jijini Dar es salaam.

MAZOEZINI


Wachezaji wa timu ya watoto wa Shein Rangers Sports Club wakifatilia mazoezi ya wenzao kwa umakini.

Friday, December 11, 2009

SHEREHE ZA UHURU TANZANIA ZAFANASherehe za miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar zafana. Picha ya juu ni Rais Jakaya Kikwete na mkuu majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa sherehe hizo, na picha ya chini ni kikundi cha sanaa toka Uganda kikitumbuza katika sherehe hizo.

Wednesday, December 9, 2009

MIAKA 48 YA UHURU WA TANZANIA BARA


Bodi ya Wakurugenzi, Uongozi na Wachezaji wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB. Wanatoa pongezi kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete na serikali yake pamoja na watanzania wote kwa ujumla katika sherehe za kutimiza miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika leo tarehe 09 Desemba 2009.

SHEIN RANGERS SPORTS CLUB INAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WANAMICHEZO WOTE ILI KULETA MAENDELEO KATIKA MICHEZO NA KUMPATIA HAKI MTOTO WA KITANZANIA KATIKA KUSHIRIKI MICHEZO.

TANZANIA BARA 4 ERITREA 0


Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara mara baada ya mchezo wa robo fainali dhidi ya Eritrea, bara ili shinda bao 4 - 0 na kuingia nusu fainali.

Tuesday, December 8, 2009

TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST KUJA TANZANIA


Timu ya Taifa ya Ivory Coast inawasili nchini tarehe 2 January 2010 kwa kambi ya wiki moja ikiwa katika maandali ya Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika Angola, pia ikiwa Tanzania itajipima ubavu na Taifa Stars (timu ya taifa ya Tanzania) kwa michezo miwili siku ya tarehe 4 na 7 January 2010 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

MDAHALO


Siku ya terehe 10 Desemba 2009 kutakuwa na mdahalo kuhusu unyanyasaji kijinsia, mdahalo huo utafanyikia Karimjee Hall kuanzia saa nane mchana.

MADA
Je, wanaume ni chanzo cha unyanyasaji kijinsia?

MUONGOZA MADA
Jenerali Ulimwengu

Wanamichezo wote tuungane na watanzania wengine katika mapambano ya unyanyasaji kijinsia.

UJUMBE HUU UNALETWA KWENU NA:-
SHEIN RANGERS SPORTS CLUB

Monday, December 7, 2009

ZIARA YA SHEIN TWALIPO CAMP

Timu ya Shein Rangers siku ya tarehe 06 Desemba 2009 ilifanya ziara ya mafunzo katika kituo cha kukuza soka cha Twalipo Youth Soccer Foundation (TYSF) kinachomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania chini ya mwalimu wa soka Maj Bakari.

Katika ziara hiyo kulifanyika michezo ya kirafiki mitatu kwa kuzingatia umri wa wachezaji wa pande zote mbili na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-
Mechi ya kwanza TYSF 1 - Shein Rangers 0 chini ya miaka 12
Mechi ya pili TYSF 2 - Shein Rangers 0 chini ya miaka 14
Mechi ya Tatu TYSF 1 - Shein Rangers 0 chini ya miaka 17

Uongozi wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB unapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukurani kwa mapokezi mazuri na mchezo mzuri wa amani na upendo, pia tunapenda kuchua nafasi hii kutoa shukurani za dhati kwa zawadi ya mpira maalum wa kuchezea soka kwa watoto na kugharamia usafiri.

SHEIN YAFANYA ZIARA TWALIPO


Mkuu wa kituo cha kukuza soka cha Twalipo Youth Soccer Foundation (TYSF) Major Bakari kushoto katika picha ya pamoja na kocha mkuu wa Shein Rangers ndugu Rashid Said katika kituo cha soka cha Twalipo jijini Dar es Salaam, timu ya Shein ilifanya ziara ya mafunzo katika kituo hicho cha soka kwa timu zake zote tatu kupata kichapo.

MANAHODHA NA WAAMUZI


Manahodha wa timu ya (TYSF) na Shein Rangers chini ya miaka 12 wakiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo wao, nahodha wa Shein Rangers Moses Leonald (jezi bluu bahari) na nahodha wa (TYSF) Mussa Bakari (jezi yenye mistari ya bluu na nyekundu).

TWALIPO CHINI YA MIAKA 12


Timu ya Soka ya Kituo cha kukuza soka cha Twalipo Youth Soccer Foundation (TYSF) chini ya miaka 12.

TYSF NA SHEIN RANGERS


Timu ya Shein Rangers chini ya miaka 12 (jezi bluu bahari) na timu ya Twalipo Youth Soccer Foundation (TYSF) katika picha ya pamoja kabla ya kucheza mchezo wa kirafiki, (TYSF) ilishinda bao 1 - 0 katika mchezo uliokuwa mzuri.

MAPUMZIKOPicha ya juu ni timu ya Shein Rangers chini ya miaka 12 na picha inayofata ni Shein chini ya miaka 17, wakati wa mapumziko katika mechi zao walizocheza na timu za kituo cha Twalipo na timu zote za Shein Rangers zili lala mbele ya vijana wa (TYSF).

NAHODHA U 12 SHEIN AMFURAHISHA MAJ BAKARI


Nahodha wa timu ya Shein Rangers chini ya miaka 12 (U12) Moses Leonald amfurahisha Maj Bakari kwa uwezo wake wa soka katika nafasi yake ya kiungo mshambuliaji.

TWALIPO WATOA ZAWADI KWA SHEIN RANGERS


Nahodha wa timu ya kituo cha kukuza soka cha Twalipo Youth Soccer Foundation (TYSF)chini ya miaka 12 (U 12) Mussa Bakari (jezi bluu bahari kushoto) akimkabidhi zawadi ya mpira maalum wa kuchezea watoto nahodha mwenzake wa timu ya watoto wa Shein Rangers Moses Leonald.

PICHA YA PAMOJA U 17


Picha ya pamoja ya Shein (chini ya miaka 17) na timu ya kituo cha kukuza soka cha Twalipo baadaya ya mchezo mkali na kuvutia kumalizika baina ya timu hizo, katika mchezo huo Twalipo ilishinda bao 1 - 0 kwa mkwaju wa penati dakika za lala salama.

DUA YA PAMOJA


Timu ya kituo cha soka ya Twalipo na Shein Rangers katika dua ya pamoja kumshukuru mungu baada ya kumaliza mchezo wao salama.

Sunday, December 6, 2009

ZUIA UKATILI KIJINSIA

SHEIN RANGERS SPORTS CLUB INAUNGANA NA KAMPENI ZA KIDUNIA YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI KIJINSIA.

NINAWAJIBIKA KWA VITENDO KATIKA FAMILIA NA JAMII YANGU.
HAUKO PEKE YAKO MWENYE NIA BINAFSI, UTHUBUTU NA UTAYARI WA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA.

MTANZANIA, MWANAMICHEZO ZUIA UKATILI KIJINSIA KATIKA JAMII YAKO!

Saturday, December 5, 2009

U17 SHEIN KATIKA MAANDALIZI YA MECHI NA TWALIPOTimu ya chini ys miaka 17 ya Shein Rangers ikiwa katika maandalizi ya mchezo na timu ya kituo cha Twalipo.

SHEIN KUCHEZA NA TWALIPO

Timu za SHEIN RANGERS na KITUO CHA SOKA CHA TWALIPO kuumana katika michezo ya kirafiki siku ya tarehe 06 Desemba 2009 katika uwanja wa Twalipo jijini Dar es salaam. Mechi zinazotarajiwa kuchezwa ni tatu kwa timu chini ya miaka 12, 14 na 17. Wapenzi wa soka ya vijana wanakaribishwa kupata burudani ya soka.

SHEIN KATIKA PICHA


Picha hii ya pamoja ya timu zote tatu za SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, chini ya miaka 17, 14 na 12.

Tuesday, December 1, 2009

SIKU YA UKIMWI DUNIA


Leo tarehe 01 Desemba 2009 ni siku ya UKIMWI duniani kote, kwa Tanzania kitaifa inafanyitika mkoani Tanga. Shein Rangers ilitumia siku hii kwa kuwakumbusha na kuwaelimisha wachezaji wake jinsi ya kujikinga na kupambana na maradhi hayo, juu pichani wachezaji wakisikiliza kwa makini.

MWENYE KIPAJI


Mtoto Semeni Sadiki ni moja kati ya watoto zaidi ya 60 walijitokeza katika usaili wa kuchezea timu ya watoto wa Shein Rangers na yeye kuwa miongoni mwa watoto wenye kipaji cha soka waliopita katika mchujo.

SEMENI MAZOEZINIMtoto Semeni Sadiki ambaye ana ulemavu wa ngozi akiwa na watoto wenzake(wachezaji wa shein rangers) chini ya miaka 14 katika mazoezi.

KIDUME KAZINI
Mtoto Ramadhani Kilindo maarufu kwa jina la utani "KIDUME" akiwa katika mazoezi ya shein rangers juu ni matukio tofauti ya kidume kikiwa kazini.