Sunday, January 31, 2010

MICHEZO YA MWISHO WA WIKI

SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 30 JANUARY 2010
Shein Rangers ilicheza na African People ya Mwananyamala katika uwanja wa shule ya msingi Mwananyamala B na Shein Rangers kushinda magoli 4 - 3. Wafungaji kwa upande wa Shein ni Maharaji Bulu magoli 2, Ibrahimu Juma 1 na Yohana 1.

SIKU YA JUMAPILI TAREHE 31 JANUARY 2010

Shein Rangers ilicheza na Friends Rangers ya Magomeni katika uwanja wa shule ya msingi Mwalimu Nyerere Magomeni na Shein Rangers kushinda magoli 3 - 2. Wafungaji kwa upande wa Shein ni Maharaji Bulu 1, Godgrey Mwita 1 na Victor Wenslaus (figo)1.

Pamoja na ushindi huo timu ya Shein Rangers ilionyesha kiwango kikubwa cha soka.Timu zote hizo zinashiriki ligi ya TFF Wilaya ya Kinondoni.

KOCHA SHEIN RANGERS NA VIJANA WAKE


Kocha wa Shein Rangers Sports Club Rashid Said (wa kwanza kulia) akiwa na wachezaji wake katika moja ya Hotel kubwa jijini Dar (kutoka kushoto) ni Godfrey Mwita na Maharaji Lal Bulu.

Thursday, January 28, 2010

NYUMBANI NI NYUMBANI


Hayo ndio mambo ya nyumbani hakuna kinachoshindikana, we amini usiamini.

MWISHO WA WIKI ULIVYOKUWA SHEIN RANGERS

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB mwishoni mwa wiki iliyoisha iliishushia kichapo timu inayoshiriki ligi ya TFF Wilaya ya Kinondoni Kimara Rangers bao 6 - 1. Mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kimara.

PATA HII YA FEKI ZA WACHINA

Wanariadha wapatao 30 kati ya mamia waliojitokeza katika mashindano ya mbio kusaka wanariadha 100 wa mwanzo watakaojiunga na chuo kikuu cha michezo nchini China wamebainika kufanya udanganyifu kwa kupita njia za panya. Miongoni mwa mbinu walizotumia ni kupanda lifti za magari na kukodi wakimbiaji wa kasi, shirikisho la mchezo huo nchini humo lilisema baadhi ya watu wanaoshiriki mashindano hayo maarufu kama Xiamen International Marathon katika jimbo la kusini mashariki mwa Fuji kuwa watu hao walifanya udanganyifu huo kwa ajili ya kuwa katika nafasi za mwanzo ili wachukuliwe na chuo hicho. China wamekuwa maarufu sana duniani kwa kuingiza bidhaa zisizo na ubora sokoni (bidhaa feki).

Saturday, January 23, 2010

KIVAZI


Mpenzi mmoja wa bendi kongwe nchini akisakata dansi la kibongo na kivazi cha aina yake.

Wednesday, January 20, 2010

SANGOMA ATAKA UJIRA WAKE KOMBE LA DUNIA

Mganga mmoja wa kienyeni nchini Afrika Kusini aitwaye Anna Samalo ametoa kali ya mwaka baada ya kuilaumu kamati ya maandalizi ya Kombe la dunia la soka na chama cha soka cha nchi hiyo (SAFA) kwa kumkwepa kumlipa ujira wake, baada ya kufanya kazi yake ya kichawi ili nchi hiyo ishinde kura za kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Soka (FIFA World Cup 2010).
Lawama hizo zimekuja baada ya nchi hiyo kuzawadia kamati ya maandalizi ya kombe hilo fedha za nchi hiyo rand milioni 7.5, kama zawadi kwa kuweza kuwa wenyeji wa kombe la dunia na kamati hiyo kumsahau Sangoma huyo.

Tuesday, January 19, 2010

TOVUTI YA ISWiT YAZINDULIWA DAR


Tovuti ya wiki ya Kimataifa ya wanafunzi Tanzania yazinduliwa jijini Dar es Salaaam. Kuingia tembelea www.iswit.org

Saturday, January 16, 2010

TEMEKE KUHAMASISHA MATUMIZI YA BAISKELI


Klabu ya mchezo wa Baiskeli iliyopo Wilayani Temeke jiji Dar es salaam imeandaa mbio za baiskeli za kilometa 60 kwa ajili ya kuhamasisha usafiri wa baiskeli wilayani humo. Mbio hizo zitafanyika tarehe 23 January 2010 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Wilaya ya Temeke ni wilaya ya pekee yenye muamko wa kimichezo katika Jiji la Dar.

Thursday, January 14, 2010

TANZIA: NAHODHA TP AFRIKA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Nahodha wa timu kongwe ya TP AFRIKA SPORTS CLUB ya Uzuri Sinza Thomas Chiwiko amefariki dunia siku ya tarehe 12 January 2010 saa nne asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. Na mazishi yake yalifanyika tarehe 14 January 2010.

Kutokana na msiba huo, Uongozi na wachezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB unatuma salamu za rambirambi kwa Uongozi na wachezaji wa timu ya TP AFRIKA SPORTS CLUB na FAMILIA YA MAREHEMU.

MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN!

MAMIA WAMZIKA THOMAS CHIWIKO


Mamia ya wakazi wa Uzuri na wanamichezo walijitokeza kwa wingi katika mazishi ya aliyekuwa nahodha wa timu ya TP AFRICA SPORTS CLUB marehemu Thomas Chiwiko licha ya mvua kunyesha. Mazishi hayo yalifanyika leo tarehe 14 January 2010 saa nane mchana katika makaburi ya Uzuri.

Wednesday, January 13, 2010

SHEIN YAZINDUA JEZI KWA MSIMU 2010/2011

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB imezindua jezi mpya itakazotumia katika mashindano mbali mbali katika msimu huu wa mwaka 2010/2011. Jezi hizo zina nembo (logo) ya SHEIN RANGERS upande wa kushoto na anuani ya tovuti ya timu hiyo kwa kifuani.

KUOGELEA WAIPAISHA TANZANIA

Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa kuogelea imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Three Zone na Four Zone yaliyofanyika nchini Kenya na kushirikisha nchi za Afrika Mashariki, na timu ya kuogelea ya Tanzania ilijikusanyia medali tisa na kuweza kushika nafasi hiyo.

SHEIN RANGERS SPORTS CLUB INATOA PONGEZI KWA WACHEZAJI WOTE NA CHAMA CHA MCHEZO WA KUOGELEA NCHINI (TSA) KWA KUSHIKA NAFASI YA PILI KATIKA MASHINDANO HAYO YA KIMATAIFA.

Tuesday, January 12, 2010

JITANGAZE NA SHEIN BURE

Blog ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB inapenda kuwatangazia wadau wake wote kuwa kuanzia tarehe 15 Januari 2010 blog yako inakupa nafasi ya kujitangaza bure kupitia blog hii.

Unaweza kutangaza kupitia blog hii kwa mambo yafuatayo:-
- Mambo yote ya kimichezo
- Burudani
- Biashara
- Kutafuta marafiki, mchumba
- Siku ya kuzaliwa kwako/mtoto n.k

Unaweza kutuma e.mail yako kupitia shein.rangersfc@yahoo.com au kwa kupiga simu no 0713251001
ni bora zaidi ukituma na picha ya matukio yako kama utapenda.

WATEMA MATE OVYO KUKIONA


Wakazi wa China wanaoishi katika nyumba za Serikali Jimbo la Kusini mwa nchi hiyo. Watafukuzwa katika makazi hayo iwapo watabainika kuwa na tabia ya kutema mate hadharani, taarifa hizi ni kwa mujibu wa mtandao wa www.laho.gov.ch. Pia imejumuisha makosa mengine 20 ikiwepo utupaji wa taka ovyo na upigaji kelele kupita kiasi. Kutema mate hadharani ni kitu kilichozoeleka nchini China licha ya kampeni za mara kwa mara za kuondoa tatizo hilo hatari kwa afya.

Monday, January 11, 2010

ZANZIBAR YATIMIZA MIAKA 46 YA MAPINDUZI


Timu ya Shein Rangers Sports Club inaungana na Wazanzibar wote kusheherekea kutimiza miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika tarehe 12 January 1964. Siku ya tarehe 12 January kila mwaka hufanyika sherehe za kumbukumbu ya Mapinduzi hayo.

Friday, January 8, 2010

UMESIKIA HII YA AFRIKA KUSINI?

MAKAHABA WAULA BONDENI

Asasi isiyo ya Kiserikali ya Sweat nchini Afrika Kusini ambayo inatetea haki za wafanya biashara za ngono, imetoa shinikizo kwa Bunge la nchi hiyo na vyombo vya Usalama kuondoa sheria za jinai dhidi ya wafanya biashara haramu za ngono katika kipindi chote cha fainali za kombe la dunia la soka nchini Afrika Kusini. Wanaharakati hao wameomba sheria hizo zisifanye kazi wakati wote wa fainali za kombe la dunia la soka 2010 nchini humo ili kuwapa wageni wao nafasi ya kujinafasi kwa uhuru.

Thursday, January 7, 2010

BLOG YA SHEIN YATIMIZA MWAKA LEO

Leo tarehe 07 January 2010 blog ya SHEIN RANGERS inatimiza mwaka toka ianzishwe January mwaka 2009. Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wadau wote wa Blog hii kwa kutuunga mkono, na pia tunapenda kutoka pongezi za dhati kwa marafiki wote wa blog hii na watu wote waliochangia kwa hali yoyote ile mpaka kufikia leo inatimiza mwaka.

Pia tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wadau wote waliokuwa wanatoa maoni yao kwa njia mbali mbali ili kuboresha blog hii.

Pia tunapenda kuwashukuru watu wote waliotembelea blog hii kwa kipindi cha mwaka mzima, kwa kumbukumbu zetu blog hii imetembelewa zaidi ya watu elfu mbili kwa mwaka 2009 pekee.
ASANTENI SANA

DIDIER DROGBA AWA BALOZI WA STARS


Rais Jakaya Kikwete akimbabidhi nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba jezi ya Tanzania ikiwa ni ishara ya kuwa balozi wa Taifa Stars popote duniani.

STARS ILIYOKIPIGA NA TEMBO


Timu ya Taifa ya Tanzania iliyocheza na Ivory Coast na kuonyesha kiwango cha juu katika uwanja wa taifa jijini Dar.

ZUMA APATA JIKO JIPYA


Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini amefunga ndoa ya kimila na mrembo na Tobeka Madiba nchini humo hivi karibuni, Madiba ni mke wa nne wa rais Zuma

SHEIN KUZINDUA JEZI MPYA

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB yenye maskani yake Sinza Jijini Dar es salaam Tanzania inatarajia kutambulisha jezi zake mpya itakazozitumia katika msimu wa mwaka huu 2010. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika hivi karibuni, pamoja na jezi hizo pia kutakuwa na uzinduzi wa mavazi yenye LOGO ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB.

KAA TAYARI KWA KUVAA MAVAZI YA SHEIN RANGERS!

HATIMAYE TEMBO AJIPIMA NA STARS


Hatimaye Tembo wa Afrika wanaoshika nafasi ya 16 katika viwango vya soka dunia Ivory Coast yajipima ubavu na Tanzania Taifa star na Tembo kushinda kwa bao 1 - 0 katika pambano kali la kuvutia.

Friday, January 1, 2010

HAPPY NEW YEAR

TIMU YA SHEIN RANGERS INAUNGANA NA WATU WOTE DUNIANI KATIKA KUSHEHEREKEA KUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2010.

TUNAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA MWAKA MPYA!

TANZIA: MZEE KAWAWA AFARIKI DUNIAKiongozi na mwanasiasa mkongwe, Rashid Mfaume Kawawa amefariki dunia tarehe 31 Desemba 2009 jijini Dar, Mzee kawawa pia alikuwa ni mwanamichezo hasa mchezo wa soka.