Saturday, February 27, 2010

SHEIN RANGERS SC YAFANYA MAUAJI

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB leo tarehe 27 Februari 2010 imefanya mauaji baada ya kuichapa bila huruma timu ya LEBANON bao 5 - 0 katika mchezo wa ligi ya YOSSO Wilaya ya Kinondoni. Mchezo huo mkali ulifanyika katika uwanja wa Kinesi urafiki, timu ya SHEIN RANGERS ikicheza kwa kasi na uelewano mkubwa ilitawala sana sehemu ya Kiungo iliyokuwa chini ya Miza Abdalah na Lukinga Abdul. Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Shein ilikuwa ikongoza kwa magoli mawili kwa bila yaliyofungwa na Yohana Elias (Yogo) na Lukinga Abdul mabao mengine matatu yalipatikana kipindi cha pili wafungaji ni Jumanne Goa, Richard Frank (Adebayor) na Victor Wenslaus (figo).

Kabla ya mchezo huo kulifanyika mchezo kati ya New Guinea na Friends Rangers na matokeo New Guine ilishinda bao 2 - 1.

MCHEZAJI SHEIN RANGERS SPORTS CLUB AWA MWANAMICHEZO WA WIKI 5 SPORTS


Mchezaji wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB Murshid Ally ndio mwanamichezo nyota wa wiki hii kupitia kipindi cha michezo cha 5 SPORTS kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV. Akiongea katika kipindi hicho alielezea maisha yake ya soka kwa wakati uliopita na ya wakati ujao pia alisema nusu ya maisha yake ya soka yapo katika timu yake iliyomkuza ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB na pia anathamini sana mchango wa wachezaji wenzake na mwalimu wake toka utotoni Kocha mkuu wa Shein Rangers, Rashid Said a.k.a Sir Mokake.

RIO FERDINAND KUCHEZA MECHI CHACHE


Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson amesema mchezaji wake mahili wa nafasi ya ulinzi Rio Ferdinand anatakiwa kucheza mechi chache ili awe fiti kabisa, mchezaji huyo amekuwa akiandamwa na maumivu mara kwa mara katika siku za hivi karibuni.

WENGER: WALCOTT YUPO TAYARI KWA KOMBE LA DUNIAKocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mshambuliaji wake chipukizi Theo Walcott amekomaa na anaweza kucheza kombe la dunia mwaka huu nchini Afrika Kusini. Walcott ni mchezaji wa kwanza chipukizi nchini Uingereza kufunga mabao matatu katika mechi moja dhidi ya Croatia mwaka 2008.

Friday, February 26, 2010

LIGI YA YOSSO KUENDELEA

Ligi ya YOSSO wilaya ya Kinondoni kuendelea mwishoni mwa wiki hii kwa mchezo kati ya timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB na LEBANON. Mchezo huo utachezwa siku ya terehe 27 Februari 2010 katika uwanja wa Kinesi Urafiki jijini Dar es salaam.

Tuesday, February 23, 2010

SARE YATAWALA LIGI YA YOSSO

Ligi ya soka ya YOSSO Wilaya ya kinondoni inayoendelea kutimua vumbi katika uwanja wa Kinesi jiji Dar, bado inaendelea kutawaliwa na mdudu wa sare baada ya timu ya Extra Academy na Lebanon nazo kutoka sare ya mabao 2 - 2. Mchezo huo uliochezwa tarehe 21 Februari 2010 ulikuwa na ushindani wa aina yake.

Saturday, February 20, 2010

SHEIN YAANZALI LIGI KWA SARETimu ya SHEIN RANGERS SC imecheza mchezo wa ufunguzi wa ligi YOSSO Wilaya ya Kinondoni na kutoka sare ya goli 1 - 1 na timu ya STAR RANGERS ya Kimara. Goli la SHEIN RANGERS lilifungwa na Abdalah Dastan katika kipindi cha kwanza na STAR RANGERS walipata bao la kuwasazisha kipindi hicho hicho cha kwanza. Mchezo ulikuwa mkali na kuvutia na SHEIN RANGERS walipoteza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha pili.

SIKU SHEIN ILIPOFANYA USAJILI KIDIYOSA


Kocha mkuu wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB Rashid Said akisimamia kwa umakini zoezi la usajili lililosimamiwa na KIDIYOSA.

USAJILI ULIVYOKUWA
Wachezaji wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB wakiwa katika usaili kwa ajili ya usajili wa kucheza ligi ya YOSSO Wilaya ya Kinondoni. Kushoto ni katibu mkuu wa KIDIYOSA ndugu Mwiyimadi Tambaza akisimamia zoezi zima la usajili.

Friday, February 19, 2010

LIGI YA YOSSO WILAYA YA KINONDONI YAANZA

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB ya Sinza imethibitisha kushiriki ligi ya soka inayoandaliwa na chama cha kuendeleza michezo kwa vijana wadogo wilaya ya Kinondoni (KINONDONI DISTRICT YOUTH ASSOCIATION) KIDIYOSA. Na inatarajia kucheza mchezo wa ufunguzi siku ya Tarehe 20 Februari 2010.

Akiongea kupitia blog hii mwalimu mkuu wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB Kocha Chid a.k.a Mokake amejinasibu kuibuka na ushindi mnono baada ya kuiandaa vizuri timu yake katika mazoezi na michezo ya majaribio. Wakati huo huo mshambuliajia hatari wa SHEIN RANGERS Victor Wenslaus (Figo) ametamba kuwa yeye ndio atakuwa kinara wa mabao katika ligi hiyo.

Wachezaji wote wapo fiti kwa mtanange huo isipokuwa majeruhi wanne ambao ni Mrisho Juma (Fuso), Isihaka Said, Said Issa na Juma Kizairo (Manucho).

MUNGU IBARIKI SHEIN RANGERS "THE HAMMER "

RATIBA YA LIGI YA YOSSO

Ratiba ya awali iliyotolewa na KIDIYOSA na kusainiwa na katibu mkuu wake Mwinyimadi Tambaza inaonyesha timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB itafungua dimba kwa kucheza na timu ya STAR RANGERS KIDS ya Kimara. Mchezo huo utafanyika siku ya tarehe 20 Februari 2010 katika uwanja wa Kinesi uliopo Urafiki saa 3 : 00 asubuhi. Ratiba hiyo inaonyesha siku ya tarehe 21 Februari 2010 kutakuwa na mchezo kati ya Extra Academy na Lebanon katika uwanja huo huo.

Tuesday, February 16, 2010

SHEIN WAPOKEA ZAWADITimu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB ya sinza jijini Dar es salaam imepokea zawadi za mipira na soksi toka kwa familia ya marehemu Kanali Seif wa mikocheni Regent Estate, zawadi hizo zilitolewa na wawakilishi wafamilia kwa siku hiyo ambaoni wajukuu wa marehemu Kanali Seif.

PICHA YA PAMOJA NA WACHEZAJI WA SHEIN


Wawakilishi wa familia ya marehemu Kanali Seif wa mikocheni wakipiga picha ya kumbukumbu na wachezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB chini ya miaka 14 baada ya kutoa zawadi.

WAWAKILISHI WA FAMILIA


Wawakilishi wa familia ya Marehemu Kanali Seif wa Regent Estate wakijipongeza baada ya kutoa zawadi kwa timu ya watoto wenzao wa SHEIN RANGERS, wa mbele toka kushoto ni Salum Kassim na Mussa Kassim,wa nyuma toka kushotoni Anual Abdy na Ashraf Abdy.

SHEIN WAPOKEA MIPIRA TOKA KWA MALOYA


Kushoto pichani ni katibu mkuu wa Shein Rangers Sports Club ndugu R.Sunga na Kocha mkuu wa Shein Rangers wakiwa wameshika mipira iliyotolewa na mdau wa michezo na mdau mkubwa wa Shein Rangers Sports Club Dada Hadija Maloya. Shein Rangers wanasema asante sana!!

HALI HALISI YA HAITI


Hii ndio hali halisi baada ya maafa yaliyowakumba Wahaiti.

MAKALIO NA MAPAJA MAKUBWA NI BORA KWA AFYA


Wanawake wenye makalio makubwa na mapaja makubwa kama vile Beyonce na Jeniffer Lopez wana uwezekano mdogo sana wa kupata magonjwa ya moyo na kisukari kulinganisha na wanawake wenye makalio madogo, matokeo ya utafiti wa wanasayansi nchini Uingereza umeonyesha.

MAJINA MENGINE YA AJABU! TAZAMA HII


Hili ni jina la shule moja ipo nchi fulani, nafasi za masomo zipo.

Friday, February 12, 2010

SHEIN RANGERS YAUNGA MKONO KAMPENI YA ZINDUKA


Bodi ya wakurugenzi, viongozi na wachezaji wa timu ya Shein Rangers Sports Club inaungana na serikali katika kutokomeza ugonjwa wa maralia kupitia kampeni ya ZINDIUKA . Kampeni hiyo ya kutokomeza maralia ambayo itazinduliwa februari 13 kwa onyesho kubwa litakalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kionondoni huku mgeni wa heshima akiwa Rais Jakaya Kikwete, kampeni hiyo itaendeshwa nchi nzima, pia kampeni hii ni kuhamasisha kizazi kipya cha vijana kupambana na ugonjwa wa maralia ili kuifanya jamii iliyo salama dhidi ya ugonjwa wa huo hapa nchini na inaratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii pamoja na mradi wa kutokomeza maralia.

SHEIN RANGERS SPORTS CLUB inawakumbusha wanamichezo wote kutumia kampeni za ZINDUKA kutokomeza mazalia ya mbu na kukumbusha matumizi ya vyandarua kwa familia nzima!!

"ZINDUKA TOKOMEZA MARALIA"

WAJUA KAMA BIA NI DAWA? SIKIA YA WATAFITI HAWA

Watafiti kutoka idara ya Sayansi ya chakula na Teknolojia ya chuo kikuu cha Califonia nchini marekani, wamesema kinywaji cha bia kinafaa kutumiwa mara kwa mara kwa kuwa ndani yake kina Silicon ambayo kitaalam huimarisha mifupa. Kitaalam Silicon huikinga mifupa isipate ugonjwa wa "Osteoporosis", ugonjwa huu ushambulia mifupa na kuifanya iwe myepesi na rahisi kuvunjika. Watafiti hao wameongezea kwa kusema kwa kawaida binadamu anatakiwa kupata miligramu 20 mpaka 50 za silicon kila siku, wakati bia moja ina silicom zipatazo 56.

Hii ni habari njema kwa wanamichezo ili kuimarisha mifupa yao!

Sunday, February 7, 2010

TATHMINI YA MECHI ZA SHEIN RANGERS KWA MWAKA 2009

MECHI:
Mechi zilizochezwa ni 49
Mechi ilizoshinda 36
Mechi ilizopoteza 4
Mechi za suluhu 9

MAGOLI:
Magoli ya kufunga 166
Magoli ya kufungwa 80

Wednesday, February 3, 2010

TWANGA PEPETA SOKA IPO PIA


Timu ya soka ya wasanii wa bendi ya Twanga Pepeta ya jijini dar, siku ilipowafunga wasanii wa maigizo na filamu bao 2 -1.

SHEIN RANGERS YAZINDUA MAVAZITimu ya Shein Rangers imezindua mavazi yenye nembo yake, kwa ajili ya wadau na wapenzi wote wa shein rangers.