Tuesday, March 30, 2010

SHEIN RANGERS " THE HAMMER"

Shein Rangers Sports Club is a Football club which started its operations in 1998, formerly known as Liverpool Football Club, it changed its name and came to be known as SHEIN RANGERS FOOTBALL CLUB in 2001 as soon when Dr. ALLY MOHAMED SHEIN was appointed as a vice President of Tanzania as a means of appreciating his appointment. Shein Rangers as a football club has its short and long term plans, in short term plans it aims to introduce variety of sports and games apart from football. And long term plans is to be the centre of youth talent promotion and improvement for various sports as we do believe that sports goes together with education, no education, no sports and vise versa, thus neither education nor sports will run away from each other that’s why we place our priority to education. Any youth, who is not interested in education, no matter how good he is, strictly will not be considered to our centre. Shein Rangers goes hand in hand with the Government of Tanzania to be against Illiteracy and Diseases especially AIDS, and YOUTH DRUG ADICTION. GOD BLESS SHEIN RANGERS SPORTS CLUB.

PAUL SCHOLES AONGOZA KWA KADI ZA NJANO


Mchezaji wa Manchester United Paul Scholes anashikilia rekodi ya kupata kadi nyingi za njano katika ligi ya mabingwa ulaya. Mpaka sasa ameshaonyeshwa kadi za njano 26 katika michuano hiyo.

Monday, March 29, 2010

BLOG MPYA

Wapenzi na wadau wa Blog hii ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB
Tunapenda kuwatangazia blog mpya inayozungumzia mambo ya Kijamii, Elimu na Burudani.
Blog hii inajulikana kwa jina la NAJUA WAJUA.
Blog hii pia inatoa nafasi kwa wadau wote kama, kuna jambo lolote unahisi ni busara kuwafahamisha ama kuwakumbusha na kuwaelimisha wadau usisite kulituma kupitia anuani iliyo katika blog hiyo.

Ili kuingia katika Blog hiyo Bofya www.unajuahii.blogspot.com

Sunday, March 28, 2010

NYOTA WETU WIKI HII


Nyota wetu wiki hii imeangukia kwa beki mwenye nguvu na aliyejengeka kimwili, si mwengine ila ni Mrisho Juma Mussa. Mchezaji huyo aliyejiunga SHEIN RANGERS SPORTS CLUB mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 8 mpaka sasa ni mmoja ya wachezaji tengemeo hasa katika ukuta wa timu hiyo. Pamoja na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira pia mchezaji huyo amebahatika kuwa na nguvu za ziada kiasi wachezaji wenzake kumpachika jina la FUSO kutokana na kasi na nguvu uwanjani wakimfananisha na beki wa Taifa Stars na Yanga Shedrak Nsajigwa (fuso). Mrisho Juma anamudu kucheza nafasi zote za ulinzi ila mwenyewe upendelea kucheza namba 2,4 na 5.
Huyo ndio Mrisho Juma FUSO wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB (WAPIGA NYUNDO WA SINZA).

MSIMAMO WA KUNDI A

TIMU ZA KUNDI A ..... P W D L F A PTS
SHEIN RANGERS....... 5 4 1 0 22 5 13
STAR RANGERS.......... 5 3 2 0 21 5 11
NEW GUINER.............. 5 2 0 3 14 12 6
EXTRA ACADEMY........ 5 1 3 1 11 10 6
FRIENDS RANGERS... 5 1 1 3 3 18 4
LEBANON..................... 5 0 1 4 4 21 1

Huu ndio msimamo wa kundi "A" baada ya michezo ya awali ya makundi kumalizika.

Saturday, March 27, 2010

SHEIN RANGERS 5 EXTRA ACADEMY 2

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, imeendelea kutoa dozi inayofanana kwa timu zilizo katika kundi lake baada ya leo kuichapa EXTRA ACADEMY magoli 5 - 2. Katika mchezo wa ligi ya vijana Wilaya ya Kinondoni (YOSSO) uliokuwa wa kuvutia kutokana na soka safi iliyoonyeshwa na timu zote mbili hadi mapumziko SHEIN RANGERS walikuwa mbele kwa magoli 2 -1 yaliyofungwa na Jumanne Goa na Victor Wenslaus (figo). Kipindi cha pili Shein waliongeza kasi ya mchezo na kuweza kupata magoli mengine matatu kupitia kwa wauaji wao wale wale Jumanne Goa tena Magoli mawili na Victor Wenslaus goli moja. Mpaka mwamuzi anamaliza mpambano huo SHEIN RANGERS SPORTS CLUB 5 EXTRA ACADEMY 2.

Thursday, March 25, 2010

UNAKUMBUKA HII


Unakumbuka hii? hii ilikuwa beach ya Kigamboni February 2009 wakati timu ya SHEIN RANGERS ilipoenda kwa mapumziko na mchezo wa kirafiki na VILIPE FC, mchezo huo mkali SHEIN RANGERS ilishinda bao 1 - 0.

Wednesday, March 24, 2010

JITANGAZE NA SHEIN BURE


Blog ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, ilitoa nafasi ya kujitangaza bure kupitia blog hii ikiwa kwa jambo la kijamii ama la kibiashara. Leo REGENT BARBER SHOP waliopo Mikocheni (Regent Estate) wamechukua nafasi hii kujitangaza.

REGENT BARBER SHOP
ni Salooni ya kiume iliyopo Mikocheni Regent Estate barabara ya kwenda Chuo kikuu cha Kairuki.

HUDUMA WATOAZO:
Kuweka Super Black, Wave, Mask, Scrub na Magic pia wanatoa huduma ya kusafisha na kukarabati viatu.

REGENT BARBER SHOP KWA HUDUMA BORA!

Wahudumu wa saloon wakiwa kazini


Tuesday, March 23, 2010

NYOTA WETU WIKI HII


Nyota wetu wiki hii ni beki kisiki wa SHEIN RANGERS SC, Shabani Masenga. Sifa yake kuwa awapo uwanjani ni matumizi sahihi ya nguvu na akili kwa wakati mmoja kiasi kufanya washambuliajia wengi kuogopa kupambana nae, Shabani Masenga ni mmoja ya wachezaji waandamizi wa SHEIN RANGERS anamudu kucheza nafasi zote za ulinzi watu hupenda kumwita JEMBE ila kocha wake Rashid Said a.k.a Sir Mokake hupendelea kumwita GERMAN TYPE, humfananisha na wachezaji wa kijerumani ambao hutumia nguvu zaidi. Mchezaji huyo kwa sasa ameazimwa na timu ya MANYEMA RANGERS (kikosi cha pili) na yupo nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.

Monday, March 22, 2010

SHEIN RANGERS YAENDELEZA UBABE

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, imeendeleza ubabe katika ligi ya YOSSO wilaya ya Kinondoni baada ya kutoa kipigo kikali cha tatu mfululizo katika ligi hiyo. Siku ya tarehe 21 March 2010 SHEIN RANGERS iliichapa NEW GUINER bao 5 - 2. Mabao ya Shein Rangers katika mchezo huo yalifungwa na Jumanne Goa 3 na Victor Wenslaus 2.

WAFUNGAJI WANAOONGOZA KWA MAGOLI KATIKA LIGI HIYO

Jumanne Goa wa SHEIN RANGERS Magoli 6
Victor Wenslaus wa SHEIN RANGERS Magoli 5
Festo Moyo wa STAR RANGERS Magoli 5

Wednesday, March 17, 2010

TUNAKUMBUSHIA AHADI MH MBUNGE


Mbunge wa kinondoni Mh Iddi Azan (kushoto) akiwa na diwani wa sinza na mdhamini wa mashindano ya SINZA CUP Mh Salim Mwaking'inda akitoa nasaa zake baada ya fainali, pia mbunge huyo amejitolea kudhamini makocha wawili wa shein rangers katika kozi za ukocha wa soka. Hii ilikuwa ahadi ya mbunge baada ya kutwaa Sinza Cup 2009.

Monday, March 15, 2010

SIMBA BINGWA 2009 - 2010


Timu ya SIMBA SC imetwaa ubingwa wa soka Tanzania bara baada ya kuichapa AZAM FC bao 2 - 0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

SHEIN YALALA TENA KWA AZAM FCTimu ya SHEIN RANGERS imekubali kipigo kwa mara ya pili toka kwa AZAM FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, mchezo huo ulikuwa wa utangulizi kabla ya pambano la ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya SIMBA SC na AZAM FC. Katika mchezo huo SHEIN RANGERS ililala bao 4 - 1, bao la Shein lilifungwa na Ibrahimu Juma Kombo.

Saturday, March 13, 2010

Friday, March 12, 2010

KOCHA MKUU AZAM AVUTIWA NA SHEIN


Aliyekuwa kocha wa viungo wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars, mbrazil Itamar Amorn ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa AZAM FC, amevutiwa na soka la SHEIN RANGERS. Pichani kocha huyo akiongea na mchezaji wa SHEIN mara baada ya mchezo na AZAM FC.

Thursday, March 11, 2010

AZAM YAITAMANI TENA SHEIN RANGERS


Hiki ndio kikosi kilichoanza katika mchezo kati ya SHEIN RANGERS SC na AZAM FC katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na SHEIN kulala 3 - 0. Kutokana na kandanda safi iliyoonyeshwa na vijana wa SHEIN RANGERS, timu ya AZAM imeonyesha nia ya kutaka mchezo wa marudiano siku ya Jumapili tarehe 14 March 2010 katika uwanja wa Uhuru, mchezo huo utakuwa wa utangulizi kabla ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya SIMBA SPORTS CLUB na AZAM FC.

SHEIN RANGERS YAKWAA KISIKI


Timu ya SHEIN RANGERS SC imekwaa kisiki baada ya kukubali kipigo cha bao 3 - 0 kutoka kwa AZAM FC, katika mchezo wa kirafiki ambao uliovutia watu wengi kutokana na ufundi wa timu zote mbili, timu ya Shein Rangers itajilaumu yenyewe kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuzitumia vizuri ikiwemo penati iliyopigwa na nahodha wake Godfrey Wambura na kugonga mwamba wa juu kisha kuokolewa na walinzi wa Azam. Sifa za pekee zimuendee kipa wa Azam aliyeokoa michomo mingi toka kwa wachezaji wa Shein Rangers, magoli ya Azam yalifungwa na Albert Sospeter, Khalfan Habib na Awadh Mohamed. Mchezo huo ulishuhudiwa na aliyekuwa kocha wa viungo wa Taifa Stars, mbrazil Itamar Amorn ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa AZAM FC.

KOCHA AZAM AVUTIWA NA SHEIN


Kocha wa AZAM FC Lionardo Ligone raia wa Italia wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko katika mchezo wa timu yake na Shein Rangers Sports Club. Kocha huyo alivutiwa na soka ya Shein Rangers na kuomba mchezo wa marudiano siku ya jumapili tarehe 14 March 2010.

BURUDANIWapenzi wa soka waliojitokeza kufatilia burudani ya soka kati ya SHEIN RANGESR SC na AZAM FC katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

AZAM BAADA YA MCHEZO NA SHEIN RANGERS


Wachezaji wa AZAM FC wakimsikiliza mwalimu wao mara baada ya kumaliza mchezo na SHEIN RANGERS SC.

NYOTA WETU WIKI HII


Nyota wetu wiki hii imeangukia kwa mchezaji wa SHEIN RANGERS SC, Jumanne Goa. Ni mchezajia aliyeonyesha juhudi kubwa mazoezini na katika mechi za kirafiki pamoja na michezo ya ligi ya vijana Wilaya ya kinondoni inayoendelea katika viwanja vya Kinesi na Lugalo Jeshini, Jumanne ambaye kwa sasa kiwango chake cha uchezaji kipo juu, anamudu kucheza nafasi ya ushambuliaji na kiungo wa kati na pembeni, pia hupenda sana utani awapo nje ya uwanja. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 ameanza kuchezea timu hiyo toka akiwa na miaka 8.

Huyo ndio Jumanne Goa maarufu kwa jina la "BOBAN" wapenzi wa soka wakifananisha uchezaji wake na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania anyecheza Swiden, Haruna Moshi.

AZAM IMETOA WACHEZAJI SABA TIMU YA TAIFA YA VIJANA U - 20

Timu ya AZAM FC inayopambana na timu ya SHEIN RANGERS SC ya Sinza leo katika viwanja vya michezo chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), imetoa wachezaji saba katika timu ya taifa ya soka chini ya miaka 20 ambao wataoungana na wengine kutoka timu tofauti za vijana zilizoshiriki mashindano ya UHAI CUP na AZAM FC kuwa mabingwa mara mbili mfurulizo. Timu hiyo inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana na itaanza kwa kucheza na Malawi.

Wachezaji wa AZAM FC waliochagulia timu ya taifa ya vijana (U - 20) ni Sadiki Gawaza, Tumba Swed, Jukumu Joakim, Himid Mao, Joseph Mahundi, Omari Mtaki na Faraji Hussein.

(Habari hizi kwa mujibu wa mtandao wa timu hiyo)

Wednesday, March 10, 2010

SHEIN NA AZAM SASA KUCHEZWA UDSM

Ule mpambano mkali wa soka kati ya timu ya SHEIN RANGERS SC na AZAM FC uliokuwa ufanyike katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, sasa utachezwa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM). Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa kumi jioni na itakuwa burudani tosha kwa wapenzi wa soka.

MANENO YA NAHODHA


Nahodha wa timu ya SHEIN RANGERS SC, Godfrey Wambura (watatu kutoka kushoto) akiongea na wachezaji wa timu hiyo.

KIDUME AIBUKA MAZOEZINIYule mtoto asiyeacha vituko katika mazoezi ya timu ya SHEIN RANGERS SC, maarufu kwa jina la kidume ameibuka tena uwanjani hapo baada ya kutoonekana kwa kipindi kirefu.

Tuesday, March 9, 2010

SHEIN RANGERS KUCHEZA NA AZAM

Timu ya SHEIN RANGERS SC ya Sinza baada ya kuonyesha kiwango kikubwa cha soka imewavutia mabingwa wa Uhai Cup timu ya AZAM FC (timu B) ya jijini Dar es salaam na kuamua kujipima nayo, mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali utafanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya KARUME zilipo ofisi za shirikisho la soka la Tanzania (TFF) siku ya tarehe 11 March 2010, saa kumi jioni.

Sunday, March 7, 2010

SHEIN YAPIGA 6 - 0


Wachezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SC, wakishangilia baada ya mchezo wa leo katika ligi ya YOSSO baada ya kuichapa FRIENDS RANGERS ya Magomeni bao 6 - 0.Magoli ya Shein Rangers yalifungwa na Victor Wenslaus (figo) mawili (wa tatu kutoka kushoto),Jumanne Goa mawili (wa kwanza kulia) ,Miza Abdalah moja na Mrisho Juma (Fuso) moja. Shein Rangers ilicheza mpira mkubwa sana na kutoa burudani kwa wapenzi wa soka waliojitokeza uwanjani hapo.

BENCHI LA SHEIN RANGERS


Wachezaji wa akiba wa SHEIN RANGERS SC wakifatilia mchezo huo uliokuwa wa kasi sana.

ADHABU ALIZOKUTANA NAZO KIPA WA FRIENDS RANGERS


Kipa wa timu ya FRIENDS RANGERS ya Magomeni akiwa hoi baada ya kupokea kipigo cha bao 6 - 0, hapo ni picha tofauti baada ya kufungwa na vijana wa SHEIN RANGERS SC, huu ni ushindi mkubwa wa pili kwa Shein Rangers katika ligi hiyo baada ya kushinda mechi yake iliyopita kwa magoli 5 - 0.

Saturday, March 6, 2010

KOCHA WA SWEDEN ATOA SOMO ZANZIBAR


Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Sweden Mr Bo Nilson alikuwepo nchini hivi karibuni akiwa na vijana oranje football Academy,(pichani) Mr Nilson akiwaelekeza chipukizi wa Oranje Football Academy katika kiwanja cha Mao-tse-tung Zanzibar. (picha kwa hisani ya Oranje football Academy)

NDANI YA UWANJA WA MPYA


Makocha wa timu ya SHEIN RANGERS SC wakiwa wanaelekea katika uwanja wa taifa (uwanja mpya) jijini Dar es salaam kushuhudia moja ya mechi kubwa za kimataifa zinazofanyika katika uwanja huo.

WACHEZAJI SHEIN RANGERS KATIKA KIPINDI


Kocha mkuu wa SHEIN RANGERS SC, Rashid Said akiendesha kipindi maalum kuelimisha wachezaji wake malengo ya timu katika mashindano ya YOSSO na kuwakumbusha kuzingatia kanuni za mashindano hayo.

HAWA NDIO MAKUMBUSHO TALENTS


Timu ya MAKUMBUSHO TALENTS ya makumbusho ambayo mwaka jana ilifika hatua ya fainali katika ligi ya YOSSO wilaya ya Kinondoni.

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO

Ligi ya soka kwa vijana Wilaya ya Konondoni (Yosso) imeendelea leo asubuhi katika uwanja wa kinesi, kwa michezo miwili na matokeo ya michezo hiyo ni kama ifuatavyo:-

STAR RANGERS 3 NEW GUINEA 2
MWENGE SHOOTING 1 MAKUMBUSHO TALENTS 1

KOCHA SHEIN ATAMBA KUSHINDA KESHO


Kocha mkuu wa timu ya SHEIN RANGERS SC, Rashid Said a.k.a Sir Mokake ametamba kuibuka na ushindi mnono siku ya kesho katika mchezo wa ligi ya soka kwa vijana (YOSSO) Wilaya ya Kinondoni. Kesho SHEIN RANGERS inapimana ubavu na FRIEND RANGERS katika uwanja wa Kinesi. Akiongea na Blog hii Kocha huyo alidai kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya.

Thursday, March 4, 2010

SHEIN KUSHUKA DIMBANI TENA


Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB itashuka dimbani tena katika uwanja wa Kinesi siku ya terehe 07 March 2010 kuonyeshana kazi na timu ya FRIENDS RANGERS ya magomeni katika mchezo wa ligi ya vijana (YOSSO) Wilaya ya Kinondoni.

HASHEEM THABEET AONDOLEWA LIGI YA NBA


Mchezaji nyota wa mpira wa Kikapu toka Tanzania anayecheza ligi kubwa duniani (NBA) ya mchezo huo huko Marekani Hasheem Thabeet ameondolewa katika ligi hiyo na kuingizwa katika ligi ndogo ya mchezo huo, ili ni pigo kwa wapenda maendeleo ya michezo na wanamichezo wa kitanzania.

Wednesday, March 3, 2010

CHIPUKIZI ARSENAL AVUNJIKA MGUU


Mchezaji chipukizi wa timu ya Arsenal nchini Uingereza, Aaron Ramsey amevunjika mguu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alipatwa na balaa hilo wakati wa mchezo wa ligi kuu ya nchini humo kati ya timu yake na Stoke City huyo anakuwa mchezaji wa saba kuwa majeruhi katika timu ya Arsenal.

Ramsey gets 50,000 messages in three days


More than 50,000 messages of support for Aaron Ramsey have been sent via Arsenal.com in just three days.

The midfielder's season ended on Saturday when he fractured his tibia and fibula during Arsenal's 3-1 win at Stoke. Aaron had surgery that evening and is expected to be sidelined for some time.

Tuesday, March 2, 2010

BADO SIKU MIA MOJA KUANZA KOMBE LA DUNIA


Zimebakia siku mia moja dunia ishuhudie mashindano ya kombe la dunia la soka la FIFA kufanyika katika aridhi ya Afrika (AFRIKA KUSINI) ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya sayari hii. Wanamichezo wa nchi hiyo wameanza kampeni maalum ya kushangilia kwa siku mia moja mfurulizo mpaka siku ya kuanza mashindano hayo ya soka makubwa duniani.

Monday, March 1, 2010

UMUHIMU WA "MASSAGE"

Ufanyaji wa masaji (Massage) ni miongoni mwa njia zinazotumika kuuweka mwili katika hali nzuri. Kwa kufanya masaji kutaiwezesha mishipa ya damu kuwa katika hali nzuri na hivyo kurahisisha msukumo wa damu katika mwili wako.
Ufanyaji wa masaji husaidia kuondoa baadhi ya matatizo mwilini kama vile uchovu, usongo wa mawazo n.k.
Mara nyingi ufanyaji wa masaji uchukuliwa kama kitu cha ziada sana, ama starehe. Pamoja na faida za kiafya ufanyaji masaji ukufanya uwe mwenye furaha siku zote, imezoeleka kwa wengi masaji lazima ifanyike saluni ama sahemu maalum za kulipia dhana ambayo haina nguvu hata kidogo. Wapo pia wanaoamini masaji lazima ifanyike kwa kutumia mafuta ya gharama kubwa, jambo ambalo limekuwa likiwatisha wengi kufanya huduma hii muhimu katika mwili wa binadamu. Kwa kawaida masaji inaweza kufanywa na mtu yeyote na katika mazingira yoyote, kulingana na hali ya mtoa huduma hiyo.
Ukiwa unataka kufanya masaji ukiwa nyumbani uhitaji kuwa na sehemu maalum kwa ajili ya shughuli hiyo, inaweza kuwa hata kwenye kitanda chako. Kwa upande wa mafuta yanaweza kuwa yoyote yatakayokuwa rahisi katika kuchua mwili bila kusababisha mchubuko. Baadhi ya mafuta ambayo yanaweza kutumika ni mafuta ya nazi, ufuta na alizeti. Hakikisha unachua maeneo yote ya mwili nakuacha sehemu ya tumbo. Fanya kazi hiyo kwa muda wa nusu saa hadi dakika 45, na baada ya hapo pumzika kiasi kisha unaweza kwenda kuoga. Wataalam wanashauri baada ya kuoga utembee kidogo ili kuuweka mwili sawa kabla ya kwenda kulala.