Friday, April 30, 2010

SHEIN KATIKA UKAGUZI


Wachezaji wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, wakiwa katika ukaguzi wakati wa michezo ya pasaka ya mwaka huu 2010 na timu hiyo kuwa mabingwa.

Tuesday, April 27, 2010

SHEIN YAIPIGA SHEKILANGO FC 7 - 1

Timu ya SHEIN RANGERS SC, imeichapa timu ngumu ya SHEKILANGO FC iliyomchezesha mchezaji wa mabingwa wa TUSKER CUP Yanga Ally Msigwa, bao 7 - 1 siku ya tarehe 25 April 2010. Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Shekilango timu ya Shein ilionyesha kiwango cha juu sana cha soka kilichoshangaza wapenzi wa soka wa Shekilango na maeneo ya jirani. Magoli ya Shein yalifungwa na Maharaji bulu mawili, Franco Peter (zola) mawili, Victor Wenslaus moja, Jumanne Goa moja na Abdalah Kiumbo moja. Timu ya Shekilango FC inanolewa na kocha mwenye makeke mengi Katabazi.

MIKAKATI YA USHINDI


Kocha wa SHEIN RANGERS SC, akitoa mikakati ya ushindi kwa wachezaji wake kabla ya kuanza mchezo.

SIMBA BINGWA 2009 - 2010


Wachezaji na wapenzi wa timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam wakisheherekea ubingwa wa soka wa Tanzania bara.

Thursday, April 22, 2010

MECHI MBILI GOLI NNE


Huyu ndiye Victor Wenslaus a.k.a figo, mchezaji wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, ambaye katika mechi mbili alizocheza ndani ya wiki moja ametupia nyavuni bao nne. Aliwafunga mwenge Shooting bao tatu peke yake na mechi iliyofuata alifunga bao moja dhidi ya Ponta FC.

SHEIN YAICHAPA PONTA NYUMBANI

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, imeichapa timu ya PONTA FC bao 2 - 1, katika mchezo huo mkali uliofanyika katika uwanja wa PONTA maarufu kwa jina la Sun Siro mabao ya Shein yaliwekwa kimiani na wafumania nyavu wake maarufu Victor Wenslaus (figo) na Maharaji Bulu.

Friday, April 16, 2010

TIMU YA TAIFA YA VIJANA TANZANIA KUCHEZA NA MALAWI

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (U - 20) ya Tanzania NGORONGORO HEROES kucheza na wenzao wa Malawi siku ya Jumapili tarehe 18 April 2010 nchini humo. Iwapo timu ya Tanzania itafanya vizuri katika mchezo huo na wa marudiano utakaofanyika nchini itakuwa imejiwekea mazingira mazuri kucheza fainali za Afrika kwa vijana nchini Libya mwakani na michezo ya Olimpiki ya London, Uingereza.

KOMBE LA PASAKA LILIPOTUA SHEIN

KOMBE LA PASAKA


Mchezaji wa Shein Rangers, Murshid Ally (mwenye jezi za bluu) akiwa na wachezaji wa timu ya Kombaini ya Zanzibar wakisheherekea timu ya Shein kuchukua kombe la Pasaka 2010.

Tuesday, April 13, 2010

KIJITONYAMA CHIPUKIZI YAANZA VIZURI COPA COCA COLA


Timu ya kituo cha michezo cha Kijitonyama Chipukizi (KCSC) imeanza vizuri mashindano ya soka ya Copa Coca Cola baada ya kushinda michezo yake ya awali, katika mchezo wa kwanza timu hiyo (jezi za bluu pichani) ilitoa ovyo kwa timu nyingine baada ya kuichapa Lebanon FC bao 8 - 0 katika uwanja wa Bora Kijitonyama. KCSC iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa timu ya Villa Squad bao 1 - 0 katika mchezo wake wa pili.

MWENGE SHOOTING YALALA NYUMBANI

Timu ya MWENGE SHOOTING ya mwenge imekubali kichapo cha bao 3 - 0 kutoka kwa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, mchezo huo maalum wa kuzipima timu zote mbili ambazo zinajiandaa na michezo yao ya ligi tofauti. Timu ya Mwenge Shooting inajiandaa na mchezo wa ligi ya copa coca cola na Timu ya Shein Rangers inajiandaa na mchezo wa nusu fainali ligi ya YOSSO Wilaya ya Kinondoni.
Katika mchezo huo mkali uliochezwa katika uwanja wa Mwenge Shooting, Mchezaji wa Shein Rangers Victor Wenslaus (figo) aliibuka shujaa baada ya kupiga bao zote tatu peke yake na kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani hapo.

Baada ya mchezo huo kiongozi wa timu ya Mwenge Shooting ndugu Andrew Tupa aliisifia timu ya Shein kwa kuwa na vijana wadogo walioonyesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu na mchezo wa kuvutia ambao ulikuwa ni burudani tosha kwa wakazi wa maeneo ya mwenge.

Friday, April 9, 2010

SHEIN YATWAA UBINGWA WA PASAKA


Timu ya SHEIN RANGERS SC, imetwaa ubingwa wa michezo ya ujirani mwema ya Pasaka 2010 iliyoshirikisha timu za Kombaini ya Kinondoni, Kombaini ya Zanzibar, Tegeta United na Shein Rangers. Timu ya Shein ilishinda mechi zake zote kwa kuichapa Kombaini ya Zanzibar bao 2 - 1, Kombaini ya Kinondoni bao 3 - 2 na Timu ya Tegeta United iliingia mitini. Pamoja na kutwaa ubingwa huo timu ya Shein Rangers ilikabidhiwa zawadi ya kikombe na kupata tiketi ya kwenda kutetea ubingwa huo Zanzibar wakati wa michezo ya Pasaka mwakani.

UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU, SHEIN RANGERS MSHIKAMANO DAIMA

NAHODHA AKIPOKEA KOMBE


Nahodha wa SHEIN RANGERS katika michezo huo, Murshid Rashid akipokea kikombe cha ubingwa wa michezo ya PASAKA 2010 kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha michezo kwa vijana Wilaya ya Kinondoni (KIDIYOSA).

SIKU YA KUFUNGA MICHEZO


Watu wengi walijitokeza siku ya kufunga michezo ya PASAKA 2010 na SHEIN RANGERS SC kuwa Mabingwa.

SHEIN RANGERS YAPONGEZWA KWA KUWA NA BLOG


Katibu msaidizi wa chama cha soka cha Zanzibar (ZFA)na mkuu mkuu wa msafara wa timu ya Kombaini ya ZNZ iliyoshika nafasi ya tatu katika michezo KOMBE LA UJIRAJI MWEMA PASAKA 2010 ndugu Masoud akitoa pongezi kwa kumalizika michezo hiyo salama na kwa timu ya Shein Rangers kwa hatua waolipiga kwa kuwa na blog ambayo aliitembelea na kuisifia sana.

NYOTA YETU WIKI HII


Nyota yetu wiki hii imeangukia kwa mchezaji mwenye kipaji cha soka na utundu wa kuuchezea mpira pamoja na chenga, si mungine ila ni MBWANA ELIASA ama ROBINHO, jina la Robinho amepewa na wapenzi wa soka kutokana na utundu wake na ufundi wa kuuchezea mpira awapo mchezoni wakimfananisha na nyota wa Brazil Robinho.
Mbwana alizaliwa mwaka 1996 jijini Dar es salaam na ni mwanafunzi wa shule ya sekondari. Amejiunga na timu ya Shein Rangers mwaka 2009 na pia ni mpenzi mkubwa wa Manchester United. Mchezaji huyo mkimya na mwenye umbo dogo ila mwenye mambo makubwa uwanjani anamudu vilivyo kucheza namba 7 na 11. Yeye mwenyewe anasema anahusudu sana uchezaji wa mchezaji nyota wa Brazil Robinho na ndoto zake ni kucheza soka barani ulaya.

Huyo ndio Mbwana Eliasa ROBINHO WA SHEIN RANGERS SPORTS CLUB.

SHEIN WAFANYA MAZOEZI NA ABAJALO


Kutokana na uwanja unaotumiwa na timu ya SHEIN RANGERS kujaa maji timu hiyo kwa sasa inafanya mazoezi yake kwa ushirikiano na timu ya ABAJALO ya sinza katika uwanja wa Abajalo, kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ligi ya YOSSO Wilaya Kinondoni.

Monday, April 5, 2010

KOMBAINI YA ZNZ NA SHEIN ZATOA VIPIGOTimu ya Kombaini ya Zanzibar, UNGUJA KASKAZINI 'A' (jezi za bluu) pichani juu (picha ya kwanza juu) ilipotoa kipigo kikali cha 6 - 1 kwa timu ya TEGETA UNITED (jezi njano na nyeusi).
Picha ya chini timu ya SHEIN RANGERS (jezi nyekundu na nyeupe) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya KOMBAINI YA KINONDONI (jezi za bluu)mara baada ya mechi yao. Katika mechi hiyo SHEIN RANGERS SC ilishinda bao 3 - 2.

Sunday, April 4, 2010

MICHEZO YA PASAKA YAENDELEA

SHEIN RANGERS 3 KOMBAIN YA KINONDONI 2Michuano ya soka ya pasaka imeendelea jana kwa timu ya SHEIN RANGERS kuichapa timu ya KOMBAINI YA KINONDONI bao 3 - 2, Magoli ya shein yalifungwa na Ibrahimu Juma, Jafary na Maharaji Bulu.

KOMBAINI YA ZANZIBAR 6 TEGETA UNITED 1
Mchezo uliofuata ulikuwa kati ya TEGETA UNITED na KOMBAINI YA ZANZIBAR, timu ya Zanzibar ikicheza soka ya kuelewana na nguvu iliichapa TEGETA UNITED bao 6 -1.

TIMU YA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE YATHIBITISHA KUSHIRIKI LIGI YA COPACOCACOLA 2010.

Uongozi wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre unayo furaha kuwajulisha wadau wake wa soka popote walipo kuwa timu yetu ya U-17 inashiriki ligi ya COPA COCA COLA U-17 Jimbo la Kinondoni inayoanza tarehe 05-04-2010 katika uwanja wa Bora Kijitonyama karibu na kituo cha polisi,Ukiwa mmoja wa wadau wa soka unakaribishwa kuja kuona soka la vijana siku hiyo tutakapoanza kucheza na timu ya Lebanon F.C na baadae na timu za Villa Sguad na Msako FC. Wote mnakaribishwa.

Taarifa hii na:-
Chris Fidelis.
Kny ya uongozi wa KCSC

PASAKA NJEMA

Viongozi na wachezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, wanawatakiwa wakristo wote nchini na duniani kusheherekea siku kuu ya pasaka kwa Amani na Upendo.

PASAKA NJEMA

Saturday, April 3, 2010

SHEIN RANGERS YAANZA MICHEZO YA PASAKA KWA USHINDI

Timu ya Shein Rangers imeanza michezo ya pasaka kwa ushindi baada ya kuichapa timu ngumu ya Kombaini ya Zanzibar kwa bao 2 - 1. Michezo hiyo iliyoandaliwa na chama cha michezo kwa vijana wilaya Kinondoni (KIDIYOSA) ni maalum kwa kukuza ushirikiano wa kimichezo na Zanzibar na hufanyika kila mwaka wakati wa siku kuu ya Pasaka.
Timu zinazoshiriki michezo hiyo ni, Kombaini ya Wilaya ya Kinondoni,Tegeta United, Kombaini ya Zanzibar na Shein Rangers. Michezo hiyo inafanyika katika uwanja wa shule ya msingi Lion magomeni.

SHEIN RANGERS YAUA WAGENI


Kikosi cha Shein Rangers Sports Club kilichowakaribisha wageni toka Zanzibar kwa kuwachapa bao 2 - 1 katika mchezo uliovutia watu wengi.

TEGETA UNITED


Timu ya Tegeta United kutoka tegeta ilianza michezo ya Pasaka kwa sare na timu ya Wilaya ya Kinondoni ya mabao 3 - 3.

TEGETA UNITED VS TIMU YA WILAYA YA KINONDONI


Mpambano wa kwanza kati ya Tegeta United na Kombaini ya Wilaya ya Kinondoni ambao ulimalizika kwa sare ya bao 3 - 3.

VIONGOZI NA WACHEZAJI WA KOMBAINI YA ZANZIBARPichani juu ni timu ya Kombaini ya Zanzibar inayoshiriki michezo ya pasaka na chini ni viongozi wa timu hiyo ilionyesha mchezo mzuri jana.

SHEIN RANGERS VS KOMBAINI YA ZANZIBAR


Mpambano kati ya Shein Rangers (jezi za njano) na Kombaini ya Zanzibar (jezi nyekundu), mchezo ulisisimua watu wengi na Shein kuibuka kidedea kwa kushinda bao 2 - 1, Magoli yaliyofungwa na nahodha wake Godfrey Wambura na Yusuf Suleiman.

MWAMUZI


Mwamuzi wa michezo hiyo Ndugu Abdalah Mwinyi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania alimudu mchezo kwa kiwango cha juu.

Thursday, April 1, 2010

MICHEZO YA PASAKA

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, itacheza mchezo wa ufunguzi michezo ya Pasaka dhidi ya timu ya Kombaini kutoka Zanzibar. Mchezo huo utachezwa kesho tarehe 02 April 2010 katika uwanja wa Shule ya Lion Magomeni barafu.Saa 9 alasiri.

Taarifa hizi ziwafikie wachezaji wote wa Shein Rangers waliokuwa mapumzikoni kutokana na uwanja wa mazoezi kujaa maji kwa ajili ya mvua.

Pia kwa wapenzi wote wa Shein Rangers na wapenda michezo wote.