Wednesday, May 26, 2010

NIZAR AENDELEA KUIPAISHA TANZANIAMchezaji wa kimataifa wa Tanzania Nizar Alfan anaendelea vizuri kuipaisha Tanzania katika ramani ya soka duniani na ni tegemeo katika club yake ya vancover nchini Canada. (Picha hii kwa hisani ya Oranje Football Academy Zanzibar)

Tuesday, May 25, 2010

KIJUE KITUO CHA MICHEZO CHA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE

Kituo cha michezo cha Kijitonyama Chipukizi Sports Centre (KCSC) kilianzishwa tarehe 13 Mei 2002 kikiwa na vijana 24. Tarehe 31 Oktoba 2006 Kijitonyama Chipukizi ilipata Hati ya Usajili toka kwa Msajili wa Vilabu na Vyama vya Michezo nchini.

Kituo cha Kijitonyama Chipukizi kinaundwa na Watu wenye heshima zao mbele ya Jamii na pia wenye Taaluma zao binafsi na kuongoza Kituo kwa kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya watoto wa kitanzania.

Viongozi wanaunda jopo la viongozi wa KCSC:-

Mwenyekiti: Ahamadi Matunda
Makamu mwenyekiti: Salum Chaurembo
Katibu Mkuu: Abubakari Pongwa
Katibu Msaidizi/Mkuu wa nidhamu na Mratibu mkuu: Chris Fidelis
Mweka Hazina: Twaha Mandwanga
Mweka Hazina msaidizi/Mshauri mkuu: Peter Msuya
Mshauri Msaidizi masuala ya udhamini: Frank Mressa

Walezi wa kituo:-


Mzee Iddi Chaurembo
Japhet Makongo
Bi Lawama Chaurembo

Walimu wa Kituo:-

Omari Amour
Mohamed Malindi
Jastin Ngwaya

VIKOSI VYA KCSCPichani juu ni wachezaji wa timu ya mchanganyiko ya U 12 na U 14 wa timu ya Kijitonyama Chipukizi wakiwa katika moja ya michezo yao na picha ya chini ni vijana wa U 17 wakiwa mazoezini.

WACHEZAJI WA CHIPUKIZI WAKIWASIKILIZA VIONGOZI WAO


Wachezaji wa kituo cha michezo cha KCSC wakiwasikiliza viongozi wao wakati wa mazoezi.

KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C YATOLEWA ROBO FAINALI KI-AINA

Uongozi wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre unasikitika kutolewa katika hatua ya Robo Fainali iliyochezwa tarehe 22 May 2010 katika Uwanja wa Mwl,Nyerere baada kufungwa kwa magoli 6-5 yaani mchezo uliisha kwa suluhu ya goli 1-1 na ndipo hatua ya upigaji wa penati ulipofuata wenzetu timu ya Gardeni wakapata penati zote na sisi kukosa moja iligonga mwamba, Kilichotufanya tusikitike ni kwa Mwamuzi aliyechezesha leo kuombwa palepale uwanjani na wasimamizi wa mchezo wa leo huku wakijua hana taaluma ya uamuzi, Ametunyima penati dhahili ndani ya dk 90 na kutoa penati kwa wapinzani wetu huku mtu aliyesababisha alijiangusha na la mwisho hakuwa na kadi, Hii ni hatua muhimu sana lakini imekuwa kawaida kwa Viongozi wa Chama kutoleta waamuzi,tunajipanga kwa mashindano mengine na hatutakuwa tayari kucheza kwa waamuzi wa bora liende huku wilaya yetu inao waamuzi lukuki na wadhamini wa mashindano walishatoa fedha za kulipia waamuzi.

Chama kinashindwa kuelewa kuwa tunaowalea ni vijana wadogo Kisoka na hawatupi msaada wowote zaidi ya wadau wetu wao wapo ofisini kwa mazoea.tunawashukuru wote waliotupatia kila aina ya msaada na tunawaahidi iko siku uozo wa aina hii utaisha kwa kila wanachama kuangalia viongozi hawa wameifanyia nini kinondoni.

Taarifa hizo zimetumwa kwa njia ya mtandao na uongozi wa KCSC.

Sunday, May 23, 2010

NGASA APATA AJIRA MPYA AZAM


Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na Yanga ya Dar es salaam, Mrisho Ngasa amepata ajira mpya katika timu ya Azam FC ya jijini. Ngasa amenunuliwa na timu hiyo kwa Shilingi milioni 58 na amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Thursday, May 20, 2010

WAPIGA PENALTI WAONYWA

Shirikisho la soka la kimataifa FIFA, limepiga marufuku wachezaji ambao watapiga penalt kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia kusita sita kabla ya kupiga adhabu. Kuanzia sasa FIFA imesema kwamba mpiga penalt hataruhusiwa kusita anapohashiria kufanya hivyo kwa lengo la kuwapumbaza makipa. Bodi ya kimataifa ya soka (IFAB) ambayo ni wakala wa FIFA imeeleza kuwa hatua hiyo si ya kiuwanamichezo na muhusika ataonywa kwa kadi ya njano katika fainali zijazo.

Sunday, May 16, 2010

SHEIN YATINGA FAINALI LIGI WILAYA YA KINONDONI


Wachezaji na makocha wa timu ya Shein Rangers Sports Club wakisheherekea baada ya kupata ushindi wa magoli 2 - 0 dhidi ya timu ya Tegeta United. Kwa ushindi huo timu ya Shein itacheza fainali na timu ya Star Rangers ambayo nayo iliichapa timu ya Humbarg FC bao 3 - 1 katka nusu fainali ya pili.

GOLI LA PILI


Wachezaji wa Tegeta United wakiwa wanashangaa baada ya Shein kuandika bao la pili.

VICTOR WENSLAUS AFIKISHA MAGOLI 9 KATIKA LIGI


Mchezaji Victor Wenslaus (figo) katikati akionyesha jezi yake namba 7, katika mchezo wa nusu fainali mchezaji huyo alifunga magoli yote mawili na kufikisha jumla ya magoli 9 aliyofunga katika mashindano hayo.

Saturday, May 15, 2010

KIKOSI KILICHOINGIZA SHEIN FAINALIPicha juu ni kikosi kilichoingiza timu ya SHEIN RANGERS SC, fainali ligi ya YOSSO wilaya ya kinondoni leo tarehe 15 May 2010 katika uwanja wa kinesi, na picha ya chini wachezaji wa Shein wakisalimiana na wachezaji wa Tegeta United kabla ya kuanza kwa mechi hiyo.

TEGETA UNITED


Timu ya Tegeta United iliyochapwa na shein rangers 2 - 0 katika mchezo wa nusu fainali ligi ya YOSSO Wilaya ya Kinondoni.

Thursday, May 13, 2010

SHEIN KATIKA MAANDALIZI NUSU FAINALI


Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa nusu fainali kusaka bingwa wa Mkoa wa kisoka wa Kinondoni. Mchezo huo wa nusu fainali utafanyika mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Kinesi dhidi ya timu ya TEGETA UNITED.

Wednesday, May 12, 2010

SHEIN KUFUNGUA TAWI CANADA

Mtanzania anayeishi nchini Canada Gerald Luzangi ameahidi kuwa balozi wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB nchini Canada na Japani. Aliyasema hayo baada ya kuitembelea timu ya hiyo alipokuja nchini wakati wa likizo yake hivi karibuni. Moja ya mipango iliyopo baina yake na timu ya shein ni kujaribu kuwatafutia nafasi wachezaji wa shein katika vyuo vya michezo nchini Canada na Japani, pia amejitolea kutafuta wahisani wa kuweza kuisaidi timu hiyo mambo mbali mbali hasa vifaa vya michezo. Pamoja na hayo kuna mambo mengi yalizungumzwa mbele ya wachezaji wa timu hiyo hasa kujitanua kupitia teknolojia ya Computer. Wadau wa shein kaeni tayari kupata mambo mapya yanayoendana na wakati ndani ya miezi michache ijayo.

SIKU SHEIN ILIPOPATA UGENI TOKA NJE YA NCHIMdau wa michezo na wanasoka Gerald Luzangi (katikati pichani juu) ni Mtanzania anyeishi Canada na kucheza soka nchini humo akitoa mada kwa wachezaji wa SHEIN RANGERS SC, kuhusu maisha ya soka nje ya nchi na wafanye nini ili waweze kucheza soka nje ya Tanzania. Pia alitaka wajitambue kama wao ni vijana wanapaswa kuwa na malengo, hivyo wawe na nidhamu nje na ndani ya uwanja na pia aliwasisitizia kuwahi mazoezini ili kwenda sambamba na programu ya mwalimu.

KIDUME NAE ALIKUWEPO


Yule mtoto mwenye vituko katika timu ya Shein, Bwana kidume pia alikuwepo siku timu yake ilipotembelewa na wageni.

MWALIMU AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAGENI


Wageni wa timu ya SHEIN RANGERS SC, wakiongea na kocha mkuu wa Shein Rashid Said (katikati)kulia kwake ni Gelard Luzangi toka Canada na kushoto ni Hisami kutoka Japan.

PICHA YA PAMOJA


Picha ya pamoja ya wachezaji wa SHEIN RANGERS SC, viongozi pamoja na wageni wao mara baada ya kumaliza kikao cha kuweka mikakati ya maendeleo ya timu na mchezaji binasfi kwa siku zijazo.

Saturday, May 8, 2010

BONGOYO YACHAPWA NA SHEIN 3 - 1

Timu kongwe ya soka ya BONGOYO FC ya Msasani leo tarehe 8 May 2010 imepata kichapo kutoka kwa timu ya SHEIN RANGERS SC kwa kulala kwa bao 3 - 1. Mabao ya SHEIN yaliwekwa kimiani na nyota wake Mbwana Eliasa na Munil. Mchezo huo wa kuvutia ulichezwa katika uwanja wa Shule ya Msingi Mashujaa Sinza,

Friday, May 7, 2010

SHEIN DARASANI


Mwalimu wa SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, Rashid Said akiendesha kipindi cha darasani kwa wachezaji wake.

Wednesday, May 5, 2010

SHEIN KUENDELEA NA MAZOEZI

Timu ya soka ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Shule ya Msingi Mashujaa uliyopo Sinza kwa ushirikiano na timu ya ABAJALO FC ya Sinza.

Timu ya SHEIN ipo katika maandali ya mchezo wa nusu fainali ligi ya YOSSO Wilaya ya Kinondoni.

Tuesday, May 4, 2010

KIJITONYAMA CHIPUKIZI YAINGIA HATUA YA PILI LIGI YA COPA COCA COLA 2010

KATIBU MKUU,
SIMU:+255-732-587839,
DAR ES SALAAM.

TAREHE: 03/05/2010
KWA WADAU WOTE WA SOKA,
POPOTE MLIPO.

Ndugu,
YAH:MATOKEO YA MCHEZO WA JANA TAREHE 02-05-2010 KATIKA UWANJA WA MWL,NYERERE KATI YA KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C NA TIMU YA MSAKO F.C LIGI YA COPACOCACOLA 2010.
Husika na kichwa cha habari hapo juu.
Kwenu wadau wa soka,timu ya Kijitonyama Chipukizi S.C imefanikiwa kuingia kwa kishindo ligi ya copa cocacola hatua ya pili kwa kufanikiwa kuifunga timu ya Msako f.c kwa magoli 4 kwa 1,magoli yaliyofungwa na Rashid Esmail(magoli mawili) Abubakari Ngane goli moja na Mzackiru Mohamed goli 1,hivyo kuifanya timu ya KCSC kuwa na pointi 9, magoli ya kufunga 13 na goli la kufungwa 1 katika mechi 3 ilizocheza na hivyo moja kwa moja kuingia ligi hatua ya pili ya kumtafuta bingwa wa mkoa wa kinondoni,Ligi hatua ya pili itaanza mara baada ya timu zote kumalizika mwishoni mwa wiki hii na timu zilizoongoza katika makundi kupangiwa ratiba itakayozikutanisha timu 3 kwa kila jimbo yaani kinondoni,kawe na ubungo kumpata bingwa wa mkoa wa kinondoni.

MAFANIKIO KWA WACHEZAJI KWA HATUA YA KWANZA.

Timu yetu imefanikiwa kutoa wachezaji watatu kwa ajili ya timu ya mkoa wa kinondoni copa cocacola2010 nao ni Golikipa Abubakari Mayallah, Rashid Esmail na Daudi Yohana na kwa upande wa kombaini ya KIFA tumefanikiwa kutoa wachezaji Daudi Yohana na Abubakari Ngane.

Tunatoa shukrani kwa wadau wetu wote kwa ushirikiano waliotupatia.


Taarifa hii imetumwa kwa njia ya mtandao na:-
CHRIS FIDELIS kny KCSC

KIKOSI CHA KCSC COPA COCA COLA 2010


Pichani ni kikosi cha timu ya KIJITONYAMA CHIPUKIZI kilichowakilisha vyema katika mashindano ya COPA COCA COLA Wilaya ya Kinondoni.

Sunday, May 2, 2010

TANZANIA 1 RWANDA 1


Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imetoka sare na timu ya Taifa ya Rwanda kwa kufungana bao 1 - 1 katika mchezo wa kwanza kuwania kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.

SHEIN KUENDELEA NA MAZOEZI

Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, inaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Shule ya Msingi Mashujaa Sinza, baada ya uwanja wake wa mazoezi wa TP Afrika kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote kwa wakati huu.