Wednesday, June 30, 2010

TATHMINI YA MECHI ZA SHEIN RANGERS SC TOKA JANUARY MPAKA JUNE 2010

MECHI
Mechi zilizochezwa ni 29
Mechi ilizoshinda 23
Mechi ilizopoteza 3
Mechi za suluhu 3

MAGOLI
Magoli ya kufunga 97
Magoli ya kufungwa 45

Mchezaji anayeongoza kwa magoli
Victor Wensleaus magoli 22

Mchezaji aliyecheza mechi nyingi
Victor Wansleaus mechi 22

Friday, June 25, 2010

SHEIN WALIPOKUWA UFUKWENI


Timu ya SHEIN RANGERS SC, walipokwenda kutalii katika fukwe ya Kigamboni, safari hiyo ilijumuisha timu nzima.

Tuesday, June 22, 2010

PICHA YA KUMBUKUMBU


Picha ya kumbukumbu ya mwezi kama huu mwaka jana timu ya soka ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, ilitembelea na kutoa zawadi katika kituo cha watoto Yatima cha Sikitiko kilichopo Magomeni jijini Dar es salaam.

Monday, June 21, 2010

SHEIN YARUDI UWANJA WAKE

Timu ya SHEIN RANGERS SC,iliyokuwa nje ya uwanja wao wa mazoezi kwa kipindi kirefu kutokana na mvua zilizokuwa zinanyesha nchi nzima imerudi katika uwanja wanaotumia kwa mazoezi uliopo sinza wa TP Afrika.

MCHEZO WA KIRAFIKI
Mwishoni wa wiki iliyopita timu ya SHEIN RANGERS SC, iliichapa timu ya UDSM bao 9 - 2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa TP Afrika Sinza.

Sunday, June 20, 2010

WAWILI WA SHEIN WACHAGULIWA TIMU YA COPA COCA COLA MKOA WA KINONDONI


Ramadhani Issa (Dizana) mchezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SC, aliyechaguliwa katika timu ya mkoa wa Kinondoni kwa michuano ya copa coca cola na alicheza mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya mkoa wa mjini magharibi na mkoa wa Kinondoni kushinda bao 2 - 1.

VICTOR WENSLAUS


Mchezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SC, aliyechaguliwa katika timu ya mkoa wa Kinondoni kwa michuano ya copa coca cola na alicheza mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya mkoa wa mjini magharibi na mkoa wa Kinondoni kushinda bao 2 - 1.

Tuesday, June 15, 2010

GHANA YAWAFURAHISHA WAAFRIKA


Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana wakisheherekea goli baada ya kuichapa Serbia bao 1 - 1 katika mashindano ya Kombe la Dunia (FIFA World Cup 2010) nchini Afrika Kusini.

Sunday, June 13, 2010

MCHEZAJI WA ZAMANI SHEIN AFARIKI DUNIA


Mchezaji wa zamani wa Shein Rangers SC Daud Yusuf, amefariki dunia mwishoni wa wiki iliyopita na kuzikwa katika makaburi ya Tandale. Mchezaji huyo alizaliwa mwaka 1989 na alijiunga na Shein Rangers mwaka 2002 mpaka 2005. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen!

MAZISHI YA DAUDI YUSUF

Ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu wakijumuika na wanamichezo waliojitokeza katika mazishi.

Friday, June 11, 2010

Nelson Mandela Will Not Attend Opening Ceremony

Nelson Mandela will now not attend the opening ceremony of the World Cup following the tragic death of his great-granddaughter following a concert in Soweto on Thursday evening.

Zenani Mandela, 13, was killed in a car accident following the event held to mark the beginning of the tournament.

"Nelson Mandela this morning learned of the tragic death of his great-granddaughter, Zenani Mandela, in a car accident. It would therefore be inappropriate for him to personally attend the 2010 FIFA World Cup opening celebrations," a statement from the Nelson Madela Foundation reads.

"We are sure that South Africans and people all over the world will stand in solidarity with Mr Mandela and his family in the aftermath of this tragedy.

"We continue to believe that the 2010 FIFA World Cup is a momentous and historic occasion for South Africa and the continent and we are certain it will be a huge success. Madiba will be there with you in spirit today."

Tuesday, June 8, 2010

BRAZIL YAICHAPA TANZANIA 5 - 1


Timu ya Taifa ya Soka ya Brazil imeichapa Tanzania bao 5 - 1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa nchini Tanzania tarehe 07 Juni 2010 jijini Dar es salaam. Pamoja na Tanzania kuchapwa bao tano ilionyesha kukomaa kiuchezaji na kuvunja rekodi ya Brazil kutoruhusu vyavu zake kuguswa toka Oktoba 2009.

NIZAR Vs KAKA


Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Nizar Halfan akikabana na mchezaji wa kimataifa wa Brazil Kaka katika mchezo wa kirafiki uliofanyija jijini Dar es salaam na Brazil kushinda bao 5 - 1.

Saturday, June 5, 2010

KOMBE LA DUNIA LABAKISHA SIKU TANO KUANZA


Mashindano makubwa kabisa ya soka dunia maarufu kama kombe la dunia la FIFA yamebakiza siku tano kuanza nchini Afrika Kusini, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika katika bara la Afrika.

SHEIN WAUNGA MKONO SIKU YA MAZINGIRA


Timu ya SHEIN RANGERS SC, imesheherekea siku ya mazingira duniani kwa kufanya usafi katika uwanja wao wa mazoezi na maeneo yanayozunguruka uwanja huo, ikiwa ni kuunga mkono siku ya mazingira duniani.

Thursday, June 3, 2010

KOMBE LA DUNIA

Kombe la Dunia la FIFA ni mchuano wa kimataifa wa mchezo wa soka wa wanaume. Kombe hili hutambulika pia kama kombe la dunia la soka, kombe la dunia la mpira wa miguu au Kombe la Dunia. Kombe hili hushindaniwa na nchi wanachama wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA - Fédération Internationale de Football Association). Mashindano haya hutazamwa na watu wengi zaidi duniani kuliko mashindano yoyote yale. Mashindano ya mwaka 2002 watu wapatao bilioni 1.1 walitazama.

Baada ya hatua za mwanzo za kugombea kushirikia katika mchuano huu, nchi 32 hushiriki katika mchuano ambao hufanyika katika nchi inayoandaa/zinazoandaa mashindano hayo.

Hadi sasa ni nchi saba tu ambazo zimeweza kuchukua kombe hili toka lilipoanza kushindaniwa hapo mwaka 1930. Mashindano haya hufanyika kila baada ya miaka minne. Mwaka 1942 na 1946 hakukuwa na Kombe la Dunia kutokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Brazili ndio nchi pekee ambayo imeweza kutwaa kombe hili mara tano mfululizo. Ujerumani na Italia zimelitwaa mara tatu. Nchi nyingine ambazo zimewahi kulitwaa ni Uruguay, Ufaransa, Argentina, na Uingereza.

Ujerumani ndio nchi iliyoandaa Kombe la Dunia 2006 kati ya Juni 9 hadi July 9. Bingwa wa sasa wa kombe hilo, Brazili, imetolewa kwenye mashindano hayo kwa kufungwa 1-0 na Ufaransa. Kombe la Dunia 2010 litafanyika katika bara la Afrika kwa mara ya kwanza katika nchi ya Afrika Kusini.

Wednesday, June 2, 2010

SHEIN YACHAPWA NA KOMBAINI YA KINONDONI

Timu ya Mkoa wa Kinondoni inayojiandaa na mashindano ya Copa Coca Cola leo tarehe 02 Juni 2010 imeichapa timu ya Shein Rangers bao 5 - 1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Tanganyika uliopo Kawe.

Tuesday, June 1, 2010

SHEIN RANGERS KUPIMANA NA TIMU YA KINONDONI

Siku ya tarehe 02 Juni 2010 timu ya SHEIN RANGERS SC, itapimana ubavu na timu ya soka ya Mkoa wa Kisoka wa Kinondoni inayojiandaa na mashindano ya Copa Coca Cola yanayoshirikisha timu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani. Na timu ya Shein ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa fainali ligi ya Wilaya ya Kinondoni ambayo kisoka inatambuliwa kama mkoa. Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Tanganyika uliopo Kawe jijini Dar, saa kumi jioni.