Tuesday, July 27, 2010

NYOTA WETU WIKI HII


Nyota wetu wiki hii imeangukia kwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutoa pasi za uhakika na si mungine ila ni Abdallah Kiumbo Shomari maarufu kwa jina la (Didigo). Mchezaji huyo mwenye tabia ya ukimya awapo uwanjani na nje ya uwanja ni kipenzi cha wachezaji wenzake na wadau wa soka kutokana tabia yake hiyo. Didigo ni mchezaji anayejituma sana katika mazoezi ya timu na hata katika mazoezi yake binafsi. mchezaji huyo aliyezaliwa mwaka 1995 jijini Dar es salaam alijiunga na timu ya SHEIN RANGERS SC mwaka 2005 na akiwa uwanjani anamudu kucheza namba 7, 11, 9 na 10. Mbali na soka mchezaji huyo ana kipaji cha mchezo wa ngumi pia, na alipata mafunzo ya mchezo huo hapa hapa jijini Dar es salaam.

Sunday, July 25, 2010

MICHEZO YA MWISHO YA WIKI

SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 24 JULY 2010
Timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, ilicheza na timu ya kituo cha michezo cha KIJITONYAMA CHIPUKIZI (KCSC)katika uwanja wa bora na timu ya Shein ilishinda bao 3 - 2. Magoli ya Shein yalifungwa na Victor Wenslaus (figo), Ibrahim Juma Kombo na Zola.

SIKU YA JUMAPILI TAREHE 25 JULY 2010
Saa 10 : 30 Jioni timu ya SHEIN RANGERS (U - 20) ilicheza na timu ya AL HADAD ya Bagamoyo (U - 20) na timu ya Shein ilishinda bao 1 - 0 goli lililofungwa na Maharaji bulu.

Kabla ya mechi hiyo saa 9 : 00 kulifanyika mchezo kati ya Shein (U-17) na AL HADAD (U - 17) na matokeo Shein ilishinda bao 2 - 1, magoli ya Shein yalifungwa na Lukinga Abdallah na Fuso.

Thursday, July 22, 2010

KCSC YAPATA ZAWADI TOKA BENK YA NMB


Kocha wa timu ya watoto ya kituo cha michezo cha KIJITONYAMA CHIPUKIZI akipokea zawadi ya Cones toka kwa meneja Benk ya NMB tawi la Mlimany City.

MAZOEZI YANAENDELEA

Baada ya mapumziko marefu kwa wachezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB, timu hiyo imeanza mazoezi katika uwanja wa TP AFRIKA uliopo sinza. Uongozi wa timu unapenda kuwataarifu wachezaji wote waliokuwa katika mapumziko kufika mazoeni kama kawaida.

MCHEZO WA KIRAFIKI
Siku ya Jumapili tarehe 25 July 2008 timu ya Shein Rangers itacheza mchezo wa kirafiki na timu kutoka Mkoa wa Pwani Bagamoyo. Mchezo huo utaanza majira ya saa tisa alasili, wapenzi wote wa soka mnakaribishwa kupata burudani safi ya soka.

Tuesday, July 13, 2010

KINONDONI MADUME WA COPA COCA COLA 2010


Wachezaji wa timu ya soka ya mkoa wa kisoka wa Kinondoni, wakipanda jukwaa la wageni wa heshima kupokea zawadi zao za ubingwa wa COPA COCA COLA 2010, pichani mbele nimchezaji wa Kinondoni Ramadhani Salim (jezi namba 10) muuwaji wa bao la pili dhidi ya Temeke. Katika fainali Kinondoni iliichapa timu ngumu ya Temeke bao 2 - 0.

FURAHA YA UBINGWA

Viongozi na wachezaji wa kinondoni wakiwa na furaha kubwa baada ya kuchukua kombe la copa coca cola kwa mwaka 2010, pichani (katikati) aliyebeba kombe ni kiongozi wa KCSC Chris Fidelis na wapili kutoka kulia ni Dizana Issa toka SHEIN RANGERS FC. Hii ilikuwa katika uwanja wa UHURU baada ya kuichapa Temeke bao 2 - 0 katika mchezo wa fainali.

KCSC YAPATA MLEZI MPYA


KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE IMEPATA MLEZI MPYA AMBAYE NI MHE: JORDAN RUGIMBANA (MKUU WA WILAYA YA KINONDONI) KUANZIA TAREHE 9-JULAI 2010. TAARIFA ZAIDI ZA KUMPOKEA NA KUSHIRIKIANA NAYE JUU YA MAENDELEO YA KCSC TUTAWAPATIA HAPO BAADAE.

TAARIFA HII IMETUMWA KWA NJIA YA MTANDAO TOKA KCSC
NA: CHRIS FIDELIS kny KCSC

Friday, July 9, 2010

KINONDONI KUCHEZA FAINALI COPA COCA COLA NA TEMEKE

TIMU ya vijana ya Copa Coca-Cola wenye umri wa miaka 17 ya Temeke, imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Kigoma bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na sasa itakutana na Kinondoni kwenye mechi ya fainali itakayopigwa Jumamosi.

Katika mechi hiyo, Temeke ilizidiwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha kwanza ambapo, dakika ya 33 Kigoma ilikosa penalti baada ya Najim Benjamin kupaisha mpira juu.

Hata hivyo Temeke ilizinduka katika kipindi cha pili, baada ya kufanya mashambuizi ya nguvu langoni mwa wapinzani wao ambapo dakika ya 58, timu hiyo ilipata ambayo hata hivyo Selemani Bofu alishindwa kutumbuiza mpira kimiani.

Temeke baada ya kukosa penalti hiyo, ilizidisha mashambulizi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika ya 88, lililowekwa kimiani na Makarani Ally.

Timu hiyo inakutana Kinondoni ambayo, juzi ilifanikiwa kutinga fainali, baada ya kuwafunga bao 1-0 mabingwa watetezi, Mjini Magharibi katika mechi pia iliyochezwa Uwanja wa Uhuru.

Sunday, July 4, 2010

KINONDONI YATINGA NUSU FAINALI COPA COCA COLA 2010


Timu za Kinondoni na Mbeya zikiingia uwanjani katika mchezo wa robo fainali copa coca cola 2010 uliofanyika uwanja wa Uhuru na Kinondoni kuibuka washindi kwa bao 3- 0 na kutinga hatua ya nusu fainali.

WACHEZAJI KCSC WATAMBA COPA COCA COLA

WACHEZAJI WA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE WAZIDI KUNGAA KATIKA TIMU YA MKOA WA KINONDONI HUKU BW RASHID ESMAIL AKIONGOZA KWA IDADI YA MAGOLI 7 NA KUPATA MIPIRA AINA YA JABURANI MIWILI NA RAMADHANI MZEE MWENGE MAGOLI 6 AKIWA NA MPIRA MMOJA WA JABURANI BILA KUMSAHAU GOLIKIPA NAMBA MOJA WA KCSC BW ABUBAKARI MAYALLA ALIFUNGWA MAGOLI MATATU TU TO MWAZO WA MASHIDANO MPAKA SASA.

NDUGU WADAU KWA SASA MECHI HIZI ZINAONESHWA LIVE NA KITUO CHA ITV SAA 10:00 JIONI KILA SIKU NA HII TIMU YETU ITACHEZA NUSU FAINALI SIKU YA J/4 TAREHE 6 KTK UWANJA WA UHURU.

NDUGU WADAU TUNAWAPA BAADHI YA PICHA MUHIMU YA TIMU YETU YA KINONDONI. PICHA ZOTE KWA HISANI YA KCSC

CHRIS FIDELIS KNY KCSC.

VIONGOZI KCSC WAKIFATILIA PAMBANO


Baadhi ya wachezaji na viongozi wa Kituo cha Michezo cha Kijitonyama Chipukizi wakifatilia kwa makini mchezo kati ya Kinondoni na Mbeya katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. KCSC ni miongoni mwa timu za Kinondoni zilizotoa wachezaji mahili wanaotamba na kuipaisha timu hiyo kutinga nusu fainali ya Copa Coca Cola 2010.

WACHEZAJI WA KCSC NA SHEIN RANGERS WATAMBA NA KINONDONI KATIKA COPA COCA COLA


Timu ya Mkoa wa kisoka ya Kinondoni, siku ilipoichapa Mbeya bao 3 - 1. Wa kwanza toka kushoto ni golikipa namba moja wa Kinondoni anayetoka Kijitonyama Chipukizi Abubakari Mayalla na watatu kutoka kushoto ni mchezaji wa Kinondoni Ramadhani Issa (Dizana) anayetoka timu ya Shein Rangers.

Friday, July 2, 2010

SHEIN RANGERS WAKIWA KARUME STADIUM


Wachezaji wa timu ya SHEIN RANGERS SC, wakiwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam katika moja ya michezo yake ya kirafiki.