Tuesday, August 31, 2010

MWENYE POCHI APATIKANA

Habari njema! Hatimaye mwenye pochi yenye nyaraka muhimu iliyopotea na kutangazwa mwenyewe anatafutwa amepatikana. Pochi hiyo iloyookotwa maeneo ya Sinza Mori ikiwa na nyaraka muhimu za Esther Ibrahim Shedafa iliokotwa tarehe 29 Agost 2010. Na mwenyewe kuona katika mtandao anatafutwa aliwasiliana nasi na ameshapata pochi yake!

Monday, August 30, 2010

POCHI IMEOKOTWA MWENYEWE ANATAFUTWA

Pochi yenye nyaraka muhimu kama kadi ya Benki, kadi ya Hospitali na nyinginezo imeokotwa usiku wa tarehe 29 Agost 2010 na kondakta wa daladala iendayo Sinza/Kariakoo. Mtu yoyote mwenye kumfahamu mtu mwenye nyaraka hizo aitwaye ESTHER IBRAHIM SHEDAFA awasiliane na nasi kupitia e mail najuawajua@yahoo.com ili muhusika apate nyaraka zake muhimu.

Ama anaweza kuwasiliana kutumia blog hii au viongozi wa timu ya Shein Rangers Sports Club.

Saturday, August 28, 2010

BLOG YA SHEIN RANGERS NDANI YA FACEBOOK

Jiunge na kurasa maalum ya Shein Rangers Sports Club/Facebook

Blog yako ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB sasa inapatika katika mtandao maarufu unaounganisha watu wengi hapa duniani wa FACEBOOK.

Pia unaweza kupata habari, picha,kuchangia maoni na video za timu ya Shein Rangers katika ukurasa wake maalum unaopatikana ndani ya Facebook. Ili kujiunga na kurasa Shein Rangers Facebook bofya sehemu iliyoandika facebook hapo kulia.

Jiunge na ukurasa maalum wa Shein Rangers Sports Club ndani ya Facebook ili uiunge mkono timu yako!

Friday, August 27, 2010

KIKOSI CHA KWANZA


Kikosi cha kwanza Shein Rangers, katika moja ya michezo yake ya kifariki katika kituo cha TSA kilicho chini ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF.

Wednesday, August 25, 2010

TIMU YA WATOTO YA SHEIN RANGERS


Pichani kushoto ni kocha mkuu wa Shein Rangers SC Rashid Said, akiwa na timu ya watoto chini ya miaka 14 (U - 14) ya Shein Rangers.

Tuesday, August 24, 2010

SHEIN KUENDELEA NA MAZOEZI


Timu ya Shein Rangers Sports Club inaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa TP Afrika Sinza.

MABONDIA TANZANIA WAINGIA MITINI KATIKA MASHINDANO

Wale mabondia wa timu ya taifa ya Tanzania waliokuwa wanalalamikia ukata na lishe duni wameamua kuingia mitini kwenye ufunguzi wa michuano ya Bingwa wa Mabingwa Afrika Mashariki na Kati katika ukumbi wa DDC Mlimani Park jijini Dar es Salaam.

Mabondia hao ambao asubuhi walijitokeza kupima uzito na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mpambano walitoweka kwa kile kinachodhaniwa ni kutokubaliana na uamuzi wa viongozi wa kuwataka wao waende kula makwao huku wageni wakipewa chakula hotelini.Kwa kushindwa kutokea huko kwa mabondia wa Tanzania walitoa pointi za bure kwa wapinzani wao waliokuwa wakiingia ukumbini hapo na kusubiri kwa dakika tano kabla ya kupewa ushindi.

Monday, August 23, 2010

KIBADENI AWA MLEZI WA ABAJALO YA SINZA


Kocha maarufu na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania Abdallah Kibadeni (pichani juu)amekubali ombi la kuwa mlezi wa timu ya Abajalo FC (mnyama mkubwa) ya Sinza jijini Dar es salaam. Kibadeni ambaye ni mkazi wa Sinza amesema amekubali ombi la viongozi wa timu hiyo kuwa mlezi kiufundi na kisoka na amependa kuwasaidia vijana wenye vipaji vya soka ambao ni majirani zake.

Sunday, August 22, 2010

SHEIN RANGERS YAPIGA 10 - 0

Timu ya Shein Rangers imefanya mauaji ya kutisha baada ya kuichapa bila huruma timu ya Young Stars toka Mbezi Mwisho bao 10 - 0. Mchezo uliochezwa uwanja wa TP Africa Sinza.

Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja na magoli ya Shein Rangers yalifungwa na Maharaj Lal Bulu aliyefunga magoli matano peke yake, Thabit Mruta magoli mawili, Miza Abdalah goli moja, Adolph Mkebezi (Mwalala)goli moja na Nassoro Udulele goli moja.

Friday, August 20, 2010

LIGI KUU YA SOKA TANZANIA KUANZA


Ligi kuu ya soka ya Tanzania maarufu kwa ligi kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi tarehe 21 Agost 2010 katika viwanja mbalimbali hapa nchini na kushirikisha timu kumi na mbili. Timu hizo ni Polisi Dodoma,Yanga, AFC Arusha, Azam, Majimaji, Mtibwa, Simba, African Lyon, Toto Africa, Ruvu Shooting, JKT Ruvu na Kagera Sugar.

BONDIA WA KULIPWA TANZANIA ASAKA VIPAJI VIPYA

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Mada Maugo a.k.a mbuge mtarajiwa amesema yupo mbioni kuanza kusaka vipaji vya mabondia wapya kwa vijana wa umri wa miaka 18 - 20, kwa kuanzia ataanza Kanda ya ziwa.

Kwa sasa yupo katika taratibu za kufanikisha zoezi hilo pamoja na kutafuta wadhamini. Mchezo wa ngumi ni miongoni ya michezo iliyoipatia Tanzania sifa kwa kutoa mabondia bora miaka ya nyuma.

Wednesday, August 18, 2010

YANGA YAICHAPA SIMBA 3 - 1


Wana Yanga wakishangilia ushindi mkubwa wa bao 3 - 1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Simba. Kwa ushindi huo timu ya Yanga ndio mabingwa wa ngao ya hisani kwa mwaka 2010/2011.

YANGA YATWAA NGAO YA HISANI


Nahodha wa timu ya Yanga Fred Mbuna akipokea zawadi ya ngao ya hisani toka kwa rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Leodeger Tenga, baada ya kuifunga timu ya Simba bao 3 - 1 na kutwaa ngao hiyo katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa siku ya tarehe 18 Agost 2010.

Tuesday, August 17, 2010

MABONDIA TIMU YA TAIFA WAPUNGUA UZITO


Mabondia wa timu ya taifa ngumi (Ridhaa)wamepungua uzito kutokana na mazoezi magumu wanayopewa na kocha wao, pia ukosefu wa lishe ya kutosha umechangia kushusha uzito wa mabondia hao. Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) Eckland Mwafisi.

MARADONA ATAMANI KUWA KOCHA ASTON VILLA


Kocha mwenye vituko Diego Maradona amesema anatamani kuifundisha timu ya Aston Villa ya Uingereza ambayo inasaka kocha mpya baada ya kuondokewa na kocha wake aitwaye Martin O`Neill.

Sunday, August 15, 2010

BINGWA CHELSEA AANZA LIGI KWA KISHINDO


Mabingwa wa soka wa Uingereza Chelsea yaanza ligi kwa kishindo baada ya kuichapa West Brom bao 6 - 0.

Saturday, August 14, 2010

YANGA NA SIMBA KUGOMBEA NGAO YA HISANI


Kikosi cha Yanga kitakachopambana na Simba katika mchezo wa kugombea ngao ya Hisani siku ya tarehe 18 Agost 2010 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

SIMBA SPORTS CLUB


Kikosi cha Simba kitakachopambana na Yanga katika mchezo wa kuwania ngao ya Hisani siku ya tarehe 18 Agost 2010.

Wednesday, August 11, 2010

SHEIN YAICHAPA JUHUDI FC

Timu ya Shein Rangers SC, leo jioni tarehe 11 Agost 2010 imeichapa timu ya Juhudi FC toka Mabibo bao 6 - 2. Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa TP Afrika sinza ulikuwa wa kuvutia kutokana na uwezo ulioonyeshwa na timu zote mbili.
Magoli ya Shein Rangers katika mchezo huo yalifungwa na Maharaj Lal Bulu aliyefunga magoli matatu, na magoli mengine mawili yalifungwa na beki mwenye uwezo wa kupanda kwa kasi Timoth Emanuel na Ibrahimu Juma Kombo goli moja.

KUENDELEA NA MAZOEZI
Pamoja na kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, timu ya Shein Rangers itaendelea na mazoezi pamoja na michezo ya kirafiki kama kawaida.

APIGA BAO TATU


Mchezaji wa timu ya Shein Rangers SC, Maharaj Lal Bulu ambaye amefunga magoli matatu katika mchezo wa leo dhidi ya Juhudi FC.

Sunday, August 8, 2010

SHEIN YAICHAPA MADINGI TEMU FC

Timu ya Shein Rangers Sc, imeichapa timu ya Madingi Temu toka kiwalami bao 5 - 0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika siku ya tarehe 08 Agost 2010 katika uwanja wa TP Afrika.
Mabao ya Shein katika mchezo huo yalifungwa na Maharaji Bulu magoli matatu, Jumanne Goa na Victor Wenslaus kila mmoja goli moja.

Mchezo ulikuwa wa kuvutia na ufundi mkubwa toka wa vijana wa Shein Rangers SC.

WALIMU WA SHEIN RANGERS


Pichani kutoka kulia ni mwalimu mkuu wa Shein Rangers Rashid Said na msaidizi wake Godfrey Loya, picha hii walipiga siku timu yao ilipotinga fainali ligi wa wilaya ya Kinondoni.

Saturday, August 7, 2010

FAINALI YA YOSSO YAAHIRISHWA

Mchezo wa fainali ya ligi ya YOSSO wilaya ya Kinondoni uliyokuwa uchezwe siku ya kesho tarehe 08 July 2010 kati ya timu ya SHEIN RANGERS SC na STAR RANGERS imehairishwa mpaka hapo itakapotangazwa.

Habari za kuahirishwa mchezo huo zilipatikana jioni ya leo kupitia kwa katibu mkuu wa chama cha michezo kwa vijana wilaya ya kinondoni mzee Mwinyimadi Tambaza.

Kwa taarifa hii uongozi wa SHEIN RANGERS SC, unaomba radhi kwa wapenzi na mashabiki wake kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na kuahirishwa kwa mchezo huo.

Thursday, August 5, 2010

KIKOSI CHA PILI CHA SIMBA


Timu ya simba kikosi cha pili (simba B) walipokuwa katika mashindano ya soka ya kimataifa huko Arusha na kuibuka mabingwa. Mapema mwaka huu.

Tuesday, August 3, 2010

SHEIN KUCHEZA FAINALI NA STAR RANGERS


Timu ya Shein Rangers SC, siku ya Jumapili tarehe 08 Agost 2010 itacheza fainali ya ligi ya YOSSO mkoa wa kisoka wa Kinondoni na bingwa mtetezi wa ligi hiyo timu ya Star Rangers. Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Kinesi Urafiki saa tatu asubuhi.

HAWA NDIO STAR RANGERS


Timu ya Star Rangers ambayo itapambana na timu ya Shein Rangers katika mchezo wa fainali ligi ya YOSSO mkoa wa Kinondoni. Star Rangers ndio bingwa wa ligi hiyo kwa mwaka jana.

Monday, August 2, 2010

MSIBA KITUO CHA MICHEZO CHA KCSC

Kwa Niaba ya Bw Peter Msuya (Mshauri Mkuu na Mweka Hazina Msaidizi)wa timu ya KCSC nawajulisha wadau wetu wote kuwa mtajwa hapo juu amefiwa na mkewe na mazishi yamefanyika jana tarehe 01 Agost 2010 katika makaburi ya magomeni,Sote tumeshitushwa na taarifa za msiba wa mama huyu ambaye kwa kushirikiana na Mme wake alisaidia sana maendeleo ya ya kituo chetu,Tunasikitika kwa kifo chake na tutamkumbuka sana. Mungu amlaze mahali pema peponi Amina.


AHMADI MATUNDA kny KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE

HABARI HIZI ZIMETUMWA KWA NJA YA MTANDAO TOKA KCSC

Sunday, August 1, 2010

RIADHA TANZANIA


Wanariadha watano pekee toka nchini Tanzania ndio wamefikisha viwango vya kushiriki michezo ya jumuia ya madola itakayofanyika nchini India katika jiji la New Delhi, mwezi Octoba mwaka huu. Wanariadha hao ni Samson Ramadhani, Msenduki Mohamed, Sipe Andrea, Patrick Nyangero na Oswald Revelian.

KOCHA MZIRAY ARUDI TENA SIMBA SPORTS CLUB


Kocha mkongwe nchini Tanzania Sylarsaid Mziray (kushoto) ambaye ana sifa ya kipee nchini kwa kuwa kocha wa kwanza mzalendo kufundisha timu kongwe nchini Simba na Yanga. Kocha huyo amekuwa mwalimu wa timu hizo kwa nyakati tofauti zaidi ya mara moja. Kwa sasa kocha huyo ametua tena kuinoa timu ya Simba na anasema mkataba wake ni siri yake na Simba.