Thursday, September 30, 2010

ILIVYOKUWA BAADA YA SHEIN RANGERS KUCHUKUA UBINGWA WA KINONDONI


Hivi ndio ilivyokuwa baada ya timu ya Shein Rangers kuchukua ubingwa wa YOSSO mkoa wa Kinondoni, ilikuwa ni furaha tupu uwanjani hapo.

Tuesday, September 28, 2010

WAKATI WA MAANDALIZI YA FAINALI


Wachezaji wa timu ya Shein Rangers wakiwa katika maandalizi siku ya mchezo wa Fainali ligi ya YOSSO Kinondoni.

Monday, September 27, 2010

SALAM MAALUM TOKA KWA MWALIMU


Mwalimu mkuu wa timu ya Shein Rangers SC, Rashidi Said wa kwanza kulia mwenye flana ya kijani ametoa salam maalum za pongezi kwa wachezaji, viongozi na wapenzi wa Shein Rangers kwa mshikamano na ushirikiano wao kwa kipindi chote cha mashindano mpaka kuwa mabingwa wapya wa Kinondoni.

Pia amewaomba wachezaji wake kutojiona kuwa ndio wameshafika kwa kuwa mabingwa, na kinachotakiwa ni kuongeza bidii ya mazoezi ili kuonyesha umma kuwa kweli wao ni mabingwa wa Kinondoni.

UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU, SHEIN RANGERS MSHIKAMANO DAIMA

Sunday, September 26, 2010

SHEIN RANGERS YAWA MABINGWA WAPYA WA KINONDONITimu ya Shein Rangers SC, leo asubuhi wameweza kutwaa ubingwa wa soka mkoa wa Kinondoni kwa vijana wadogo baada ya kuichapa timu ya Star Rangers ya kimara kwa penati 4 - 3. Mchezo huo uliokuwa na kasi na wa kuvutia ulifanyika katika uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam, mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1 - 1.

Saturday, September 25, 2010

FAINALI IPO PALE PALE

Ile fainali ya kusaka bingwa wa soka mkoa wa Kinondoni kwa vijana hatimaye imewadia, mchezo huo wa fainali ambao hapo awali ulihairishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa waandaaji sasa itapigwa Jumapili ya kesho tarehe 26 Septemba 2010 katika uwanja wa Kinesi kuanzia saa 3:00 Asubuhi.

Mchezo huo utakutanisha bingwa mtetezi Star Rangers ya Kimara na Shein Rangers ya Sinza, timu hizo zilikuwa kundi moja katika michezo ya awali ambapo katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa ligi zilipokutana zilitoka sare ya bao 1 - 1.

MAMBO YA FAINALI YANAENDA VIZURI


Mwalimu wa timu ya Shein Rangers akiwa katika hatua za mwisho mwisho kuandaa kikosi chake kitakachocheza kesho fainali ligi ya YOSSO kusaka bingwa wa soka mkoa wa Kinondoni kwa vijana.

Friday, September 24, 2010

MAANDALIZI YA FAINALI YAPAMBA MOTO

Maandalizi ya mchezo wa fainali kusaka bingwa wa soka mkoa wa Kinondoni yamepamba moto kwa upande wa Shein Rangers. Kwa mujibu wa mwalimu wa timu hiyo Rashid Said mpaka sasa kila kitu kinaenda sawa.

Wednesday, September 22, 2010

MAANDALIZI YA FAINALIWachezaji wa timu ya Shein Rangers wakiwa katika maandalizi ya mchezo wa fainali ligi ya Wilaya ya Kinondoni itakayochezwa siku ya tarehe 26 Septemba 2010.

SHEIN RANGERS KUCHEZA FAINALI LIGI YA WILAYA YA KINONDONI

Siku ya Jumapili tarehe 26 Septemba 2010 kutafanyika mchezo wa fainali ligi ya YOSSO Wilaya ya Kinondoni. Mchezo huo utakutanisha bingwa mtetezi Star Rangers ya Kimara na timu ya Shein Rangers ya Sinza.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo Chama Cha Michezo Kwa Vijana Wilaya ya Kinondoni, mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Kinesi Urafiki, na kama kutakuwa na mabadiliko ya uwanja taarifa zitatolewa mapema.

Tuesday, September 21, 2010

VIJANA WA TWALIPO CAMP


Wachezaji wa timu ya Twalipo Camp wakimsikiliza mwalimu wao wakati wa mapumziko walipocheza na timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars katika uwanja wa Karume.

Monday, September 20, 2010

TIMU YA KCSC ILIPOPATA UGENI MZITOMkuu wa wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana (wa pili kutoka kushoto waliosimama katika picha ya juu ) akiwa na wageni wengine waalikwa, pamoja na viongozi na wachezaji wa kikosi cha pili cha timu ya soka ya Kituo cha Michezo cha Kijitonyama Chipukizi katika moja ya shughuli za kimichezo kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama. Katika picha ya chini ni Kocha wa Kijitonyama Chipukizi Jastin Ngwaya (wa pili kutoka kulia waliosimama) akiwa na wachezaji wa kikosi cha pili.

Saturday, September 18, 2010

TWIGA STARS WAJARIBU NA TWALIPO CAMPTimu ya Taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) jioni ya leo imepimana ubavu na timu ya Twalipo Camp (kituo cha soka kinachomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania) katika mchezo mzuri na wa kuvutia uliochezwa katika uwanja wa Karume ikiwa ni sahemu ya maandalizi kwa timu ya Twiga kwa ajili ya fainali za Afrika kwa wanawake nchini Afrika Kusini. Katika mchezo huo timu ya Twalipo ilishinda bao 4 - 0,pamoja na Twiga Stars kupoteza mchezo huo ilionyesha mchezo mzuri na wa ushindani.

Picha ya juu wachezaji wa timu zote mbili wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo na picha ya chini ni wachezaji wa Twiga Stars baada ya mchezo huo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TWIGA STARS

WAAMUZI WA MCHEZO HUO WALIKUWA NI WATOTOPicha ya juu ni mwenyekiti wa chama cha soka cha wanawake Lina Mhando (kulia mwenye miwani) akiwapongeza waamuzi hao watoto baada ya kumudu vyema pambano hilo. Na picha ya chini ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) Charles Mkwasa akisalimiana na waamuzi hao kabla ya mchezo. Waamuzi hao watoto walikuwa kivutio kwa wadau wa soka waliojitokeza katika uwanja wa karume jijini Dar es salaam.

SASA UNAWEZA KUCHANGIA MADA NDANI YA KURASA MAALUM YA SHEIN RANGERS KATIKA FACEBOOK

Blog ya Shein Rangers inapenda kuwataarifu wadau wake kuwa pamoja na kuanzisha kurasa yake maalum katika mtandao mkubwa na maarufu duniani wa Facebook, pia imeanzisha sehemu maalum ndani ya ukurasa huo ambayo wadau wa michezo wataweza kuchangia mada mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu na michezo mingine nchini Tanzania.

Jinsi ya kuweza kuchangia mada mbalimbali ukishaingia katika ukurasa maalum wa Shein Rangers katika mtandao wa Facebook. Utaenda sehemu iliyoandikwa DISCUSSIONS na ukiingia hapo utakuta mada (topic) ya siku na utaweza kushiriki nasi kwa kuchangia mada husika kwa wakati huo.

UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU, SHEIN RANGERS MSHIKAMANO DAIMA

Thursday, September 16, 2010

Wednesday, September 15, 2010

MTIBWA 1 YANGA 1


Ligi kuu ya soka Tanzania bara iliendelea jana katika viwanja mbalimbali, pichani anaonekana kipa wa Mtibwa Shaban Kado akiwa makini golini kwake katika mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Yanga, mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo uliisha kwa sare ya 1 - 1. Mjini mwanza Simba iliichapa Ruvu Shooting ya Pwani bao 2 - 1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba na Azam ikalala kwa Kagera Sugar bao 1 - 0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Tuesday, September 14, 2010

SHEIN RANGERS KUJIPANGA UPYA


Baada ya kutofaya mazoezi ya uhakika kutokana na kuwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, timu ya Shein Rangers SC imeanza kujipanga upya ili kujiweka katika hali ya kawaida kimichezo. Wachezaji wote ambao walikuwa hawajaripoti mazoezini wanatakiwa kufika mara moja kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya kirafiki na mchezo wa fainali ligi ya YOSSO wilaya ya Kinondoni.

Monday, September 13, 2010

SIKU SHEIN RANGERS WALIPOKIPIGA NA AZAM FC


Hii ni picha ya kumbukumbu siku timu ya Shein Rangers SC (jezi za njano) ilipokipiga na Azam FC katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Sunday, September 12, 2010

MISS TANZANIA 2010


Mrembo Geneviene Emanuel (katikati pichani) usiku wa kuamkia leo ametawazwa kuwa Miss Vodacom Tanzania 2010.

MAZOEZI KUENDELEA KESHO


Mazoezi ya timu ya Shein Rangers kuendelea kesho baada ya kusimama kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Iddi. Pichani ni kocha mkuu wa Shein Rangers akiwa na vijana wa chini ya miaka 14 mazoezini.

Thursday, September 9, 2010

IDDI NJEMA

Uongozi na wachezaji wa timu ya Shein Rangers unawatakia waislam na watu wote dunia sikukuu njema yenye upendo na amani. EID MUBARAK!!

Mapumziko
Kipindi chote cha sikukuu uongozi wa timu ya Shein Rangers umetoa mapumziko kwa wachezaji wote hadi siku ya Jumatatu tarehe 13 Septemba 2010, siku ambayo mazoezi yataanza rasmi.

Tuesday, September 7, 2010

HAPA ILIKUWA WAKATI WA MAPUMZIKO


Kocha mkuu wa timu ya Shein Rangers Sports Club, Rashid Said akitoa maelekezo kwa wachezaji wake katika mmoja ya michezo yake katika uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam.

Sunday, September 5, 2010

SHEIN RANGERS 1 STAR RANGERS 0

Timu ya Shein Rangers, imeichapa timu ngumu ya Star Rangers ya Kimara bao 1 - 0 katika mchezo mkali wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa TP Afrika Sinza siku ya tarehe 04 Septemba 2010.

Bao pekee la Shein Rangers lilitiwa kimiani na mshambuliaji wake hatari Maharaj Lal bulu, katika mchezo huo mkali nyota wa mchezo alikuwa golikipa wa Shein Rangers Muntasir Dawood baada ya kufanya kazi kubwa ya kuokoa michomo ya wachezaji wa Star Rangers.

Thursday, September 2, 2010

SIKU SHEIN ILIPOICHAPA MIDIZINI 3 - 0


Picha hii ni ya siku za nyuma siku timu ya Shein Rangers ilipoichapa timu ya Midizini FC bao 3 - 0, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Urafiki.