Sunday, October 31, 2010

RANGER FAMILY CUP 2010/11


UONGOZI NA WANACHAMA WA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE UNAYO FURAHA KUWAFAHAMISHA WADAU WETU WOTE WA SOKA KUWA TIMU YETU YA U-20 INATARAJIWA KUSHIRIKI LIGI YA RANGER FAMILY CUP 2010 INAYOTA RAJIWA KUANZA TAREHE 13 –NOVENBA -2010 KTK UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWANANYAMALA B,LIGI INAYOSHIRIKISHA IDADI YA TIMU 20 ZIKIWEMO TIMU ZA AZAM-B,SIMBA –B NA YANGA B.

WOTE MNAKARIBISHWA

CHRIS FIDELIS(KATIBU MKUU MSAIDIZI-KCSC)

Taarifa hii imetumwa kwa njia ya mtandao na uongozi wa KCSC.

MAZOEZI YA SHEIN RANGERS U14


Timu ya watoto chini ya umri wa miaka 14 (U 14) wakiwa katika mazoezi yao ya kila siku katika uwanja wa TP Afrika chini ya Mwalimu Loya.

Saturday, October 30, 2010

SOKA YA TANZANIA YAPATA PIGO KUBWA


Kocha wa soka maarufu na mazoefu nchini Tanzania Sylasaid Mziray 'SUPER COACH' (pichani kulia) ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam amefariki dunia leo alfajiri. Mziray, ambaye mpaka kifo kinamchukua alikuwa akimsaidia Kocha Phiri kuinoa timu ya Simba ya jijini Dar es salaam. Wapenzi na wadau wa soka wanasikitika kumpoteza mtu makini kama mziray. Marehemu alikuwa ni kocha pekee wa kizalendo aliyewahi kufundisha timu za Yanga na Simba kwa vipindi zaidi ya kimoja wakati wa uhai wake. Tunamtakia mapumziko mema amen!

Friday, October 29, 2010

MAZOEZI YANAENDELEA


Mazoezi ya timu ya Shein Rangers yanaendelea katika uwanja wa TP Sinza, pichani ni wachezaji wa Shein Rangers chini ya miaka 14 (U14) wakiwa mazoezini.

Wednesday, October 27, 2010

WATANZANIA ZIMESALIA SIKU NNE KUPIGA KURA

Timu ya soka ya Shein Rangers SC ya sinza inapenda kuwakumbusha wadau wote wa michezo na watanzania kwa ujumla kuwa zimesalia siku nne tu kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

MTANZANIA KUPIGA KURA NI HAKI YAKO YA MSINGI!

Monday, October 25, 2010

SAFARI ZA TIMU


Wachezaji na viongozi wa Shein Rangers wakiwa katika moja ya safari zao za kimichezo.

Saturday, October 23, 2010

ROONEY ABAKI MANCHESTER


Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney ameamua kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yake hiyo na kufuta tetesi za kuihama klabu yake.

Friday, October 22, 2010

SHEIN RANGERS YAICHAPA TENA TWIGA STARS 4 - 1

Mabingwa wa YOSSO wiliya ya Kinondoni 2010 timu ya Shein Rangers SC yenye maskani yake Sinza, imeichapa tena timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) bao 4 - 1 katika mchezo mkali na wa kuvutia uliochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam. Mchezo huo ni wa marudiano baada ya mchezo wa awali Shein Rangers kuichapa Twiga Stars bao 5 - 1, katika mchezo wa jana magoli ya Shein Rangers yalifungwa na Munil Abdul (2), Gaudens Abel (1) na Mbwana Eliasa (1) na goli la kufutia machozi kwa wawakilishi hao wa Tanzania katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake lilifungwa na mshambuliaji wao hatari Asha Rashid a.k.a mwalala.

TWIGA STARS KUONDOKA KESHO

Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) itaondoka nchini siku ya kesho Jumamosi kwenda nchini Botswana ikiwa njiani kuelekea Afrika Kusini. Timu hiyo ikiwa nchini Botswana itakweka kambi fupi ya siku tano na kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa na wenyeji wao kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini.

KILA LA HERI KWA TWIGA STARRS
Uongozi na wachezaji wa Shein Rangers SC, wanapenda kuchukua nafasi hii kuungana na watanzania wote kuwatakia kila la heri timu ya Twiga Star katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake itakayofanyika nchini Afrika Kusini kuanzia tarehe 31 Oktoba 2010.

Shein Rangers tunasema kuwa tuna imani na timu ya Twiga Stars kwa kuwa uwezo wenu tumeuona baada ya kupata bahati ya kujipima katika michezo miwili wakati wa maandalizi yenu, sisi wapenda michezo hatukuwa na mchango mkubwa kwenu zaidi ya mchango wetu wa kuwapa mazoezi katika mechi mbili, tuna imani mchango wetu huo kwenu utakuwa na manufaa kwa timu na taifa kwa ujumla.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TWIGA STARS

Tuesday, October 19, 2010

SHEIN RANGERS KURUDIANA TWIGA STARS


Timu ya Shein Rangers SC, kurudiana na timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) siku ya Alhamisi tarehe 21 Oktoba 2010 katika uwanja wa Karume saa 10 : 30 jioni. Katika mchezo wa kwanza Shein Rangers ilishinda bao 5 - 1.

Monday, October 18, 2010

SHEIN RANGERS NDANI YA KIPINDI CHA VIWANJANI WIKI HII CHA RADIO TIMES FM 100.5


Kocha mkuu wa timu ya Shein Rangers Sports Club, Rashid Said akiongea katika kipindi maarufu cha michezo cha VIWANJANI WIKI HII kinachorushwa kila mwisho wa wiki na RADIO TIMES FM 100.5.

BAADA YA KIPINDI


Viongozi wa timu ya Shein Ragers SC waliosimama, wakiwa na Shabani Kondo ambaye ni mtangazaji wa kipindi maarufu cha michezo kinachorushwa na Redio Times 100.5 cha VIWANJANI WIKI HII, baada ya kumalizika kwa kipindi hicho ambapo wageni wa wiki walikuwa viongozi wa SHEIN RANGERS SC.

Friday, October 15, 2010

SHEIN RANGERS YAICHAPA TWIGA STARS 5 - 1


Timu ya Shein Rangers SC imeichapa timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars bao 5 - 1 katika mchezo mzuri na wa kuvutia uliochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam. Mchezo huo uliokuwa maaluma kwa ajili ya kuipa mazoezi timu ya taifa ya Tanzania inayojiandaa na mashindano ya Afrika kwa wanawake na uliwafurahisha wapenzi wa soka waliojitokeza uwanjani hapo, magoli ya ya Shein Rangers yalifungwa na Maharaj Lal Bulu (3) Victor Wenslaus (1) na Timoth Emmanuel (1) goli la Twiga lilipatikana kipindi cha pili wakati beki wa Shein Rangers Mrisho Juma (fuso) alipojifunga alipokuwa akirudisha mpira kwa kipa wake, hata hivyo Twiga Stars watajilaumu kwa kukosa penati katika mchezo huo baada ya penati iliyopigwa na Fatuma Mustapha kugonga mwamba na kuokolewa na walinzi wa Shein Rangers. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri sana na ufundi kwa pande zote mbili. Pamoja na kupoteza mchezo huo Twiga Stars ilionyesha uwezo wa hali ya juu na kutoa matumaini kwa watanzania.

HONGERA KWA MCHEZO MZURI


Kocha wa Shein Rangers Rashid Saidi (mwenye jezi ya njano)akiongea na mchezaji wa Twiga Stars Eto Mlezi mara baada ya mchezo wa kujipima nguvu kati ya timu ya Taifa ya wanawake na Shein Rangers.

BAADA YA MECHI


Nahodha wa Twiga Stars Sophia Mwasikili na baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakiwa na baadhi ya viongozi na wachezaji wa Shein Rangers baada ya mchezo wa kirafiki.

MAKOCHA WA TWIGA NA SHEIN


Kocha wa Shein Rangers SC, Rashid Said (katikati) akiwa na makocha wa timu ya taifa ya soka ya wanawake Twiga Stars, kocha Adolf kushoto na kocha Mkwasa kulia baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Shein na Twiga Stars.

Thursday, October 14, 2010

SHEIN RANGERS YAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUMKUMBUKA MWL JK NYERERE


Wakurugenzi wa bodi, uongozi na wachezaji wa timu ya Shein Rangers Sports Club wanapenda kuungana na watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya kutimiza miaka kumi na moja (11) ya kifo cha baba wa taifa Mwl. Julius K. Nyerere.

MICHEZO NI FURAHA, MICHEZO NI AMANI
SHEIN RANGERS INASEMA UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU, SHEIN RANGERS MSHIKAMANO DAIMA

Wednesday, October 13, 2010

SHEIN RANGERS Vs TWIGA STARS


Kesho tarehe 14 Oktoba 2010 timu ya Shein Rangers SC mabingwa wa YOSSO Kinondoni 2010, watashuka uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kuonyeshana kazi na timu ya Taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars. Mchezo huo utaanza saa kumi na nusu jioni maalum kwa ajili ya kuipa mazoezi Twiga Stars ambao wanajiandaa na fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake nchini Afrika kusini.

Tuesday, October 12, 2010

BONDIA PENDO NJAU ANYAKUA MKANDA WA AFRIKA MASHARIKI


Bondia Pendo Njau (kushoto) amefanikiwa kunyakuwa mkanda wa Afrika mashariki baada ya kumchapa Rukia Nasilete wa nchini Kenya katika mchezo fainali wa michuano ya ligi ya Kick Boxing iliyoanza mwishoni mwa juma lililopita kwenye ukumbi wa Amana jijini Dar es Salaam.
Pendo Njau ambaye ametetea mkanda huo alimshinda mpinzani wake Rukia Rukia kwa Point tano.
Katika mapambano ya ngumi Kalama Nyalawila amemshinda Stam Kess kwa pointi na Venans Mponji alimchapa Saidi Zungu kwa pointi.

Monday, October 11, 2010

AFISA HABARI TFF ASIMAMISHWA KAZI

Shirikisho la soka hapa nchini TFF, limemsimamisha kazi Afisa habari wa Shirikisho hilo Frolian Kaijage kutokana na Fedheha ya kushindwa kutimiza itifaki muhimu ya kupiga nyimbo za taifa za timu husika, nyimbo ya taifa ya timu ya Morocco na nyimbo ya taifa ya Jamhri ya muungano ya Tanzania katika mchezo wa timu hizo mbili uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi iliyopita.
Mchezo wa Taifa Stars na Morocco uliochezwa jumamosi iliyopita ni wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za matiafa ya Afrika mwaka 2012 ambapo Stars walilala goli 1 - 0.

Rais wa shirikisho hilo Leodegar Chila Tenga amesema tukio hilo ni la aibu kwa Tanzania lilofanyika mbele ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na mbele ya halaiki ya watanzania pamoja na wageni.

SHEIN RANGERS KUCHEZA NA TWIGA STARS


Siku ya tarehe 14 Octoba 2010 kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) na mabingwa wa YOSSO Kinondoni 2010 timu ya Shein Rangers ya Sinza. Mchezo huo maalum kuipa mazoezi timu ya Twiga Stars inayojiandaa na mashindano ya Afrika kwa wanawake nchini Afrika Kusini utachezwa katika uwanja wa Karume saa kumi jioni.

CHIPUKIZI YAFANYA MAUAJI

Timu ya soka ya watoto chini ya miaka 14 ya Kijitonyama chipukizi imefanya mauaji baada ya kuichapa timu ya watoto chini ya miaka 14 ya Shein Rangers bao 6 - 0 katika mchezo wa soka uliochezwa siku ya Jumamosi tarehe 9 Oktoba 2010 katika uwanja wa TP Afrika Sinza.

Uongozi wa timu ya Shein Rangers Sports Club unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza siku ya mchezo huo kwa viongozi na wachezaji wa timu Kijitonyama Chipukizi.

Sunday, October 10, 2010

TIMU YA SHEIN RANGERS YASHINDA MCHEZO WA BAGAMOYOTimu ya Shein Rangers SC, imeendelea kuitambia timu ya AL Hadad ya mjini Bagamoyo baada ya kuichapa bao 3 - 2 katika mchezo mkali uliofanyika mjini humo. Timu hizi zilikutana mara ya kwanza tarehe 25 July 2010 katika uwanja wa TP Afrika Sinza na timu ya Shein kuibuka washindi wa bao 1 - 0.

Saturday, October 9, 2010

SHEIN YACHAPWA 2 - 1 NA YANGATimu ya Shein Rangers jana tarehe 8 Oktoba 2010 ilichapwa bao 2 - 1 na Yanga 'B' katika mchezo safi na wa kuvutia uliofanyika katika uwanja wa Kaunda yalipo makao makuu ya klabu ya Yanga. Magoli yote katika mchezo huo yalipatikana kipindi cha pili, magoli ya Yanga yalifungwa na Jacob na Hamadi na goli la Shein Rangers lilifungwa na Mahalaji Lal Bulu.

HAWA NDIO WALIKUWA WAAMUZI KATIKA MECHI HIYO


Mechi hiyo ilichezeshwa na waamuzi watoto ambao walionyesha umahili mkubwa. Waamuzi hao wamejipatia umaarufu kwa kufanya kazi yao kwa umakini mkubwa katika michezo mbali mbali ya soka wanayochezesha.

Thursday, October 7, 2010

SHEIN YAENDELEA NA MAANDALIZI YA MECHI NA YANGA


Wachezaji wa timu ya Shein Rangers wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Yanga 'B' katika uwanja wa Kaunda uliopo makao makuu ya Yanga.

Wednesday, October 6, 2010

SHEIN RANGERS KUJIPIMA NA YANGA

Siku ya Ijumaa tarehe 8 Oktoba 2010 kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Mabingwa wa YOSSO Kinondoni timu ya Shein Rangers na timu ya Yanga kikosi cha pili, mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Kaunda uliopo katika klabu ya Yanga saa kumi jioni.

Wapenzi wa soka na wadau wa Shein Rangers SC, mnaombwa kuhudhuria kwa wingi kushuhudia vijana wenu wa Shein wakipepetana na Yanga "B".

Tuesday, October 5, 2010

SHEIN RANGERS YAALIKWA BAGAMOYOMabingwa wa ligi ya YOSSO Kinondoni 2010 timu ya Shein Rangers imealikwa kwenda Bagamoyo Mkoani Pwani kwa michezo ya kirafiki siku ya tarehe 10 Oktoba 2010. Taarifa zaidi juu ya safari hiyo zitatolewa baadae.

STAR RANGERS WASHINDI WA PILI KINONDONI


Timu ya Star Rangers ya Kimara ambao ni washindi wa pili wa ligi ya YOSSO Kinondoni, wakati wa mchezo wa fainali ya ligi hiyo wakisubiri hatua ya kupigiana penati.

Monday, October 4, 2010

SHEIN YAICHAPA TENA JUHUDI FC


Timu ya Shein Rangers SC, imeendeleza tena ubabe wake baada ya kuichapa timu ya Juhudi FC toka Mabibo bao 1 - 0. Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa TP Sinza siku ya Jumamosi tarehe 2 Oktoba 2010.

Friday, October 1, 2010

MCHEZO WA KIRAFIKI

Siku ya Jumamosi tarehe 02 Oktoba 2010 saa kumi jioni kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Juhudi FC na Shein Rangers SC, katika uwanja wa TP Afrika Sinza. Mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mgumu na wa kuvutia kutokana na uwezo wa kisoka wa timu zote mbili.

Timu ya Juhudi FC inatoka Mabibo jijini Dar es salaam, mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kirafiki timu ya Shein Rangers ilishinda bao 6 - 2.