Monday, November 29, 2010

SHEIN RANGERS YAINGIA FAINALI UKIMWI DAYTimu ya Shein Rangers SC chini ya miaka 17 (U17), imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya UKIMWI DAY inayoandaliwa na Taasisi ya Right to Play kwa kuichapa timu ya Msimamo ya Vingunguti bao 2 - 1. Magoli ya Shein Rangers yalifungwa na Miza Abdalah na Chris Alex (Messi). Mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa shule maalim ya walemavu Buguruni.

SHEIN YA WATOTO YATOLEWA NUSU FAINALITimu ya Shein Rangers (U14) jezi nyekundu na Msimamo jezi za njano wakiwa katika maandalizi ya mchezo wa nusu fainali katika michezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Right to Play.

WAKATI WA MAPUMZIKO


Timu ya watoto wa Shein Rangers SC, chini ya miaka 14 (U14) wakiwasikiliza walimu wao wakati wa mapumziko katika mchezo wa nusu fainali ya michezo maalum ya soka kwa vituo vya michezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Right to Play. Katika mchezo huo timu ya Shein Ranger na Msimamo ya Vingunguti zilitoka sale ya bao 1 - 1 ndipo ilipoingia hatua ya matuta na Msimamo kuibika washindi.

WENGINE WALIMWAGA MACHOZI


Baadhi ya wachezajiwa timu ya Shein Rangers ya watoto chini ya miaka 14 wakilia kwa uchungu baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali kwa njia ya matuta (penalti).

Wednesday, November 24, 2010

SHEIN RANGERS YATINGA ROBO FAINALI VIJANA CUP

Timu ya soka ya Shein Rangers SC "THE HAMMER" imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika ligi ya VIJANA CUP 2010/2011 baada ya kuichapa Tabata FC bao 1 - 0 katika hatua ya timu 16 bora katika ligi hiyo.

Katika mchezo huo mkali uliochezwa tarehe 20 Novemba 2010 katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam goli pekee la Shein Rangers lilifungwa na Jumanne Goa.

Saturday, November 20, 2010

VICTOR WENSLAUS ALIPOKUWA KATIKA COPA COCA COLA


Mchezaji wa Shein Rangers SC, Victor Wenslaus (wakwanza kushoto aliye juu) akifurahi na wenzake wakati alipokuwa akiiwakilisha timu ya Kinondoni katika michezo ya Copa Coca Cola na hatimaye kuwa mabingwa wa mashindano hayo kwa mwaka 2010/2011.

MABADILIKO YA RATIBA KOMBE LA RANGERS FAMILY 2010.

Uongozi wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre unaleta kwenu madiliko ya Ratiba ya Rangers Family Cup kama ifutavyo :-
Tarehe 24-11-2010 ni Kijitonyama Chipukizi na Eagle FC (small tiger)
Tarehe 07-12-2010 Kijitonyama Chipukizi na Mwananyamala Sports.
Tarehe 21-12-2010 ni Kijitonyama Chipukizi na Garden FC
Tarehe 30-12-2010 ni Kijitonyama Chipukizi na Mburahati All Star.

Ratiba hii imefuta ratiba zote za awali na ligi hii inaanza rasmi tarehe 17-11-2010 kati ya Yanga B na Yakuza.mechi zote zitachezwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B.Ratiba hii ni mujibu wa mratibu wa mashindano Bw, Abbas Ngau.

Taarifa hii imetumwa kwa njia ya mtandao na uongozi wa KCSC

SHEIN RANGERS YAINGIA 16 BORA LIGI VIJANA CUP 2010/2011

Timu ya Shein Rangers SC, ambayo ndio bingwa wa soka mkoa wa Kinondoni katika ligi ya YOSSO imefanikiwa kuingia katika timu 16 bora za ligi ya VIJANA CUP inayochezwa katika viwanja tofauti jijini Dar es salaam. Timu ya Shein Ranger ilimaliza mechi zake za makundi (kundi C) ikiwa inaongoza kundi hilo baada ya kucheza michezo mitatu, kushinda miwili na kutoka sare mmoja. Katika mchezo wa ufunguzi Shein Rangers iliichapa Friends Rangers ya Magomeni bao 2 – 1 katika uwanja wa Shule ya msingi Mwalimu Nyerere Magomeni, magoli ya Shein Rangers yalifungwa na Jumanne Goa na Victor Wenslaus, mchezo uliofata Shein Rangers ilitoka sare na Vijana Muslim ya Kinondoni bao 2 – 2 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Muslim kinondoni na magoli yote ya Shein Rangers yalifungwa na Nassoro Udulele. Mchezo wa mwisho ulikutanisha timu ya Shein Rangers na Juhudi FC ya Mabibo katika uwanja wa Juhudi huko Mabibo na Shein Rangers kushinda bao 3 – 1, magoli ya Shein katika mchezo huo yalifungwa na Said Issa (fela)2 na Victor Wenslaus 1.

Thursday, November 18, 2010

MAZOEZI YANAENDELEA SHEIN RANGES SC


Baada ya mapumziko ya sikukuu ya Eid El Haj, timu ya Shein Rangers SC inaendelea na mazoezi yake kama kawaida kujiandaa kwa ajili ya michezo iliyosalia katika ligi ya VIJANA CUP 2010/2011.

Tuesday, November 16, 2010

EID EL HAJ NJEMA

Viongozi na wachezaji wa Shein Rangers Sports Club, wanawatakia waislam wote nchini na duniani kote sikukuu njema ya Eid El Haj.

Tunapenda watu wote washeherekee kwa amani na upendo.

Sunday, November 14, 2010

MAZOENI


Shein Rangers mazoezini, kwa sasa timu ya Shein Rangers inashiriki ligi ya Vijana Cup 2010/2011.

Thursday, November 11, 2010

TIMU YA SOKA YA VIJANA TANZANIA


Pichani ni wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ya Vijana umri chini ya miaka 20 (U20) wakiwa katika moja ya michezo yao ya nje ya nchi.

Sunday, November 7, 2010

KOCHA GERARD HOULLIER AMPONDA MCHEZAJI WAKE


Kocha wa timu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza Garard Houllier amemponda mchezaji wa timu yake John Carew kwa kumwita mpumbavu baada ya mchezaji huyo kudai mkataba mpya. Mkataba wa mchezaji huyo unafikia kikomo mwishoni mwa mwaka huu na kocha amemtaka Carew kuonyesha uwezo uwanjani kwanza ndio kudai mkataba mpya.

Wednesday, November 3, 2010

PONGEZI KWA KUAPISHWA DR SHEIN


Timu ya Shein Rangers Sports Club inapenda kutoa salam za pongezi kwa Dr Ally Mohamed Shein kwa kuapishwa kwake kuwa rais mpya na wa awamu ya saba wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Timu ya Shein Rangers SC, inamtakia kila la heri katika kazi yake mpya.

HAPA NDIPO ALIPOAPISHIWA DR SHEIN


Jukwaa hili dogo (kibanda) lililojengwa maalum kwa ajili ya kumuapishia rais mpya wa Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein katika uwanja wa Amani mjini Unguja.

Monday, November 1, 2010

SHEIN RANGERS YAANZA VIZURI VIJANA CUP 2010/2011


Timu ya Shein Rangers ambayo ndio mabingwa wa soka wa Kinondoni 2010 imeanza vizuri mashindano ya soka kwa vijana umri chini ya miaka 17 (U17) kwa kuichapa timu ngumu ya Friends Rangers bao 2 - 1 katika mchezo wa ligi ya VIJANA CUP 2010/2011 uliochezwa siku ya leo tarehe 01 Novemba 2010 katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam. Magoli ya Shein Rangers yaliwekwa kimiani na Victor Wenslaus na Jumanne Goa.