Friday, December 31, 2010

MAZOEZI YASHIKA KASI


Mazoezi ya timu ya Shein Rangers SC, yanaendelea kwa kasi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya VIJANA CUP 2010.

Wednesday, December 29, 2010

SHEIN RANGERS YATINGA NUSU FAINALI VIJANA CUP

Timu ya Shein Rangers SC, imeichapa timu ya Seba Football Club bao 8 - 3 katika mchezo mkali na wakuvutia wa robo fainali ya VIJANA CUP 2010.

Kwa matokeo hayo ya mchezo huo uliochezwa leo asubuhi katika uwanja wa Villa Squad timu ya Shein Rangers imetinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Magoli ya Shein yalifungwa na Victor Wenslaus 3, Jumanne Goa 2,Mbwana Eliasa 1,Timoth 1 na George Harison 1.

Tuesday, December 28, 2010

Monday, December 27, 2010

WACHEZAJI WAKIPATA MSOSI


Wachezaji wa timu ya Shein Rangers Sports Club wakipata chakula baada ya kuchukua ubingwa UKIMWI CUP 2010.

MAZOEZI KUENDELEA LEO

Baada ya mapumziko ya siku mbili kusheherekea sikukuu ya x mas, timu ya Shein Rangers itaendelea na mazoezi yake kama kawaida kuanzia leo.

Wachezaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa kuwahi mazoezini.

Thursday, December 23, 2010

MAPUMZIKO YA SIKUKUU X - MAS


Kutokana na sikukuu ya Christmas uongozi wa timu ya Shein Rangers Sports Club umetoa mapumziko ya siku mbili kwa wachezaji wake wote, wachezaji watapumzika tarehe 25 na 26 December 2010 na mazoezi yataendelea kama kawaida tarehe 27 December 2010.

Shein Rangers inawatakia watu wote sikukuu njema!

Tuesday, December 21, 2010

NAHODHA WA SHEIN RANGERS


Nahodha wa Shein Rangers SC, Godfrey Inocent (kushoto) akiwa na mchezaji mwenzake wa Shein Victor Wenslaus katika mashindano ya UKIMWI DAY 2010.

Monday, December 13, 2010

KILIMANJARO STARS WAPELEKA KOMBE IKULUWachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wamkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete kombe la ubingwa wa CECAFA. Shughuli hii ilifanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Pichani chini wachezaji na kocha wa Kilimanjaro Stars wakifurahia ubingwa wa CECAFA katika uwanja wa taifa jiji Dar.

Sunday, December 12, 2010

TANZANIA BARA BINGWA


Timu ya soka ya Tanzania Bara imefanikiwa kuchukua ubingwa wa CECAFA TUSKER CUP 2010/2011 kwa kuichapa timu ya Ivory Coast bao 1 - 0 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Saturday, December 11, 2010

WATOTO WA SHEIN


Timu ya watoto chini ya miaka 14 (U14) ya Shein Rangers wakipasha misuli moto kabla ya kuanza moja ya michezo yake.

Friday, December 10, 2010

MIAKA 49 YA UHURU


Viongozi na wachezaji wa timu ya Shein Rangers SC, wanawapongeza watanzania wote kwa kusheherekea miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) kwa utulivu na amani.

Thursday, December 9, 2010

TANZANIA BARA YAICHAPA RWANDA 1- 0


Timu ya soka ya Tanzania Bara Kill Stars imeichapa timu ya taifa ya Rwanda bao 1 - 0 katika mchezo wa robo fainali ya CECAFA Tusker Cup katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Robo fainali ya kwanza ilizikutanisha Uganda na Zanzibar ambapo Uganda walishinda kwa penati 5 - 3 baada ya kutoka sare ya 2 - 2 katika dakika 90 za mchezo.

MABINGWA WAKIPONGEZWA


Mabingwa wa kombe la UKIMWI DAY CUP 2010 timu ya Shein Rangers SC wakipongezwa na wawakilishi wa Taasisi ya Right to Play toka Canada baada ya kuibuka wababe wa michuano hiyo.

Wednesday, December 8, 2010

HAWA NDIO WALIOLETA UBINGWA WA UKIMWI DAY CUP


Wachezaji wa Shein Rangers SC, ambao ndio waliwakilisha siku ya fainali na kushinda bao 2 - 0 na hatimaye kutwaa kombe.

WAAMUZI


Hawa ndio waamuzi waliochezesha michezo ya fainali siku ya Ukimwi duniani.

Sunday, December 5, 2010

TIMU YA SOKA WASICHANA WALEMAVU WA KUSIKIA


Timu ya soka ya wasichana toka shule maalumu ya walemavu wa kusikia ya Buguruni Marapa pia ilishiriki mashindano ya soka kwa upande wa wanawake siku ya UKIMWI DUNIANI.

Saturday, December 4, 2010

ILIKUWA NI FURAHA


Ilikuwa ni furaha kwa wachezaji wa Shein Rangers SC na wanafunzi wa shule ya msingi Mashujaa ambao kwa pamoja waliiwakilisha Sinza katika michezo ya UKIMWI DAY 2010 na timu ya Shein Rangers kuibuka mabingwa katika mchezo wa soka.

MAZOEZINI


Wachezaji wa Shein Rangers SC, wakimsikiliza Mwalimu wao Rashid Said (wa kwanza kulia) kwa makini wakati wa mazoezi ya timu hiyo jijini Dar es salaam.

Wednesday, December 1, 2010

SHEIN RANGERS MABINGWA WA UKIMWI DAY CUP 2010
Timu ya Shein Rangers SC ambayo ndio mabingwa wa soka kwa mkoa wa Kinondoni ligi ya YOSSO imetwaa ubingwa wa UKIMWI DAY CUP baada ya kuichapa timu ya PASADA katika mchezo wa fainali bao 2 - 0. Bao la kwanza la Shein lilifungwa na Victor Wenslau na la pili lilifungwa na Miza Abdalah. Mchezo huo wa fainali ulivutia watu wengi ulichezwa katika uwanja wa Ismani vinguguti. Kwa picha zaidi za mchezo huo na michezo mingine ingia katika kurasa maalum ya Shein Rangers Sports Club katika facebook.
Vile vile timu ya Shein Rangers chini ya miaka 12 ulishika nafasi ya pili katika fainali yao ya umri wao.

For more picture visit our facebook page

SHULE YA MSINGI MASHUJAA YA SINZA WALIKUWEPO


Wanafunzi wa shule ya msingi mashujaa ya Sinza pia walishiriki michezo katika siku ya Ukimwi dunia, michezo hiyo ilifanyika Vingunguti katika uwanja wa Isman.

SIKU YA UKIMWI ILIADHIMISHWA KWA MICHEZO MBALIMBALI


Wanafunzi wa shule ya msingi mashujaa ya Sinza wakishirikiana na wachezaji wa timu ya Shein Rangers katika michezo mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani.

SHEIN CHINI YA MIAKA 12 WASHIKA NAFASI YA PILI


Mgeni rasmi akiikagua timu ya Shein Rangers umri chini ya miaka 12 (U12) ambayo ilishika nafasi ya pili UKIMWI DAY CUP kwa upande wa umri wao baada ya kufungwa kwa penalti 3 - 4.

TIMU YA SHEIN RANGERS NA MSIMAMO


Timu ya Shein Rangers SC chini ya miaka 12 (U12) jezi nyekundu wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya Msimamo ya Vingunguti chini ya miaka 12 (U12) wenye jezi njano, walipopiga picha ya pamoja na wageni toka makao makuu ya Right to Play.