Thursday, January 27, 2011

MCHEZAJI TANZANIA APATA TIMU ULAYA


Mchezaji wa kimataifa wa Tanzani Asha Rashid a.k.a Mwalala amepata timu barani ulaya nchini Uturuki. Habari zaidi za safari yake na timu yake mpya zitawajia baada ya mahojiano maalum kati yake na blog hii.

Monday, January 24, 2011

SHEIN KUIKARIBISHA MAKUMBUSHO TALENT NYUMBANI

LIGI YA YOUTH SUPER CUP 2011 (LIGI YA SOKA MKOA WA DAR ES SALAAM)

Siku ya Jumapili tarehe 30 January 2011 timu ya Shein Rangers SC ya Sinza itakuwa mwenyeji wa timu ya Makumbusho Talent katika mchezo wa ligi ya Youth Super Cup 2011 inayosimamiwa na Chama Cha Michezo Kwa Vijana Wilaya ya Kinondoni (KIDIYOSA) kwa upande wa wilaya ya Kinondoni. Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa TP Africa Sinza.

Mchezo huo utakuwa ni wa pili kwa timu ya Shein Rangers katika ligi hiyo baada ya mchezo wa kwanza kuichapa timu ya Kiungi ya Magomeni bao 1 - 0 huko huko kwake. Mchezo kati ya Shein Rangers na Makumbusho Talent unatarajiwa kuwa mgumu kwani mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kirafiki Shein Rangers ililala bao 4 - 2.

Sunday, January 23, 2011

SHEIN RANGERS YAANZA LIGI VIZURI


Timu ya Shein Rangers Sports Club ya Sinza jijini Dar es salaam (jezi za njano) imeanza vizuri mchezo wake wa kwanza wa ligi ya YOUTH SUPER CUP 2011 inayosimamiwa na chama cha michezo kwa vijana Wilaya ya Kinondoni (KIDIYOSA) kwa kushinda mchezo wa ugenini kwa kuicha Kiungi FC ya Magomeni bao 1 - 0. Bao la Shein Rangers lilifungwa na Daud Mfaume kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Munir.

Saturday, January 22, 2011

SHEIN RANGERS KATIKA MAANDALIZI YA MCHEZO WA KESHOTimu ya Shein Rangers Sports Club ikiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho na Kiungi FC ya Magomeni.

Friday, January 21, 2011

YOUTH SUPER CUP 2011

SHEIN RANGERS KUSHIRIKI LIGI YA YOUTH SUPER CUP

Ligi hiyo itakayoshirikisha timu sita bora toka Wilaya ya Kinondoni alafu nne za juu zitaungana na timu toka wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam, ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa mzunguko kwa mechi za nyumbani na ugenini.

Mchezo wa kwanza kwa Shein Rangers utacheza ugenini na timu ya Kiungi FC ya Magomeni siku ya Jumapili tarehe 23 January 2011, mchezo huo awali ulikuwa uchezwe tarehe 22 January 2011 kutokana na sababu zisizozuilika imesogezwa mbele kwa siku moja.

Thursday, January 20, 2011

CHIPUKIZI NA DEPO FC KUPAMBANA ROBO FAINALI RANGERS CUP

KIKOSI KIKOSI CHA TIMU YA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE KATIKA PICHA YA PAMOJA. KIKOSI HIKI KITAPAMBANA NA DEPO FC KATIKA MCHEZO WA ROBO FAINALI YA RANGERS CUP 2010/2011 KATIKA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWANANYAMALA B.

TAARIFA HIZI ZIMETUMWA KWA NJIA YA MTANDAO NA UONGOZI WA KCSC

Saturday, January 15, 2011

SHEIN WAKIJIFUA


Timu ya Shein Rangers SC wakijifua kwa ajili ya maandalizi ya fainali ya ligi ya VIJANA CUP 2010/2011.

WAKATI HUO HUO: Timu ya Shein Rangers imeichapa timu ya Police Oysterbay bao 6 - 1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika siku ya Jumamosi tarehe 15 January 2011 katika uwanja wa TP.

Thursday, January 13, 2011

SHEIN YAJIPANGA UPYA BAADA YA KUPOTEZA MCHEZO

Baada ya timu ya Shein Rangers kupoteza mchezo wake wa kirafiki katika uwanja wake wa nyumbani hivi karibu, timu hiyo imejipanga upya ili hali hiyo isijirudie tena.

Vile vile timu hiyo inajipanga kwa ajili ya mchezo wa fainali ya VIJANA CUP 2010/2011 dhidi ya timu ya Star Rangers ya Kimara. Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuwa mgumu kwa kuwa mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika fainali ya LIGI YA YOSSO 2010 mkoa wa Kinondoni na timu ya Shein Rangers SC, kuibuka mabingwa.

Sunday, January 9, 2011

SHEIN RANGERS YACHAPWA 4 - 2


Timu ya Shein Rangers SC leo imechapwa kipigo cha aibu katika uwanja wake wa nyumbani na timu ya Makumbusho Talent bao 4 - 2 katika mchezo wa kirafiki.

Saturday, January 8, 2011

SHEIN YAINGIA FAINALI VIJANA CUP

Timu ya Shein Rangers SC ya Sinza, leo asubuhi imekata tiketi ya kuingia fainali ya VIJANA CUP 2010/2011 baada ya kuichapa timu ngumu ya Taifa toka Tandika bao 2 - 1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa katika uwanja wa Villa Squad Jangwani jijini Dar es salaam.

Magoli ya Shein Rangers yalifungwa na Miza Abdallah na Chris Alex (Messi). Kwa matokeo hayo Shein Rangers imetinga fainali na inangojea mshindi kati ya EMIMA na Star Rangers ambao watapambana kesho katika nusu fainali ya pili kwenye uwanja huo huo.

CHIPUKIZI YAINGIA ROBO FAINALI YA RANGER FAMILY CUP 2010/11

UONGOZI NA WANACHAMA WA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE UNAYO FURAHA KUWAFAHAMISHA WADAU WETU WOTE WA SOKA KUWA TIMU YETU YA U-20 IMEKUWA TIMU YA KWANZA KUTINGA HATUA YA ROBO FAINALI JANA BAADA YA TIMU YA MBURAHATI ALL STAR(MIRAMBO ) KUTOTOKEA UWANJANI NA HIVYO KCSC KUPEWA MAGOLI MATATU NA POINTI 3 NA KUFIKISHA JUMLA YA POINTI 8,BAADAE KCSC ILICHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI NA TIMU YA AMREF F.C NA KUISHINDA GOLI 7-0.KCSC INATEGEMEA KUKUTANA NA TIMU ZA SIMBA B,YANGA B AU AZAM B RATIBA YA ROBO FAINALI ITAKAPOTOLEWA.

TAARIFA HII IMETUMWA KWA NJIA YA MTANDAO NA:-

CHRIS FIDELIS(KATIBU MKUU MSAIDIZI-KCSC)

Friday, January 7, 2011

BLOG YA SHEIN RANGERS YATIMIZA MIAKA MIWILI LEO


Leo siku ya tarehe 7 January 2011 Blog hii inatimiaza miaka miwili toka kuanzishwa kwake.

Uongozi wa timu ya Shein Rangers Sports Club unapenda kutoa shukurani kwa wadau mbali mbali wanaotembelea blog hii na kutoa maoni yao, wapenzi wa michezo, blog mbali mbali marafiki na viongozi wa vilabu vya michezo marafiki na wadau wakubwa wa blog hii.

Kwa kipindi cha miaka miwili idadi ya wasomaji wa blog hii imeongezeka mara tatu zaidi ya mwaka jana na pia kwa sasa blog hii ina link na mitandao mbali mbali duniani ikiwemo mtandao maarufu duniani wa facebook.

Hapa chini tumeandaa picha na matukio muhimu yaliyoripotiwa na blog hii kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

ASANTE KWA KUICHAGUA SHEIN RANGERS SPORTS CLUB

Tuesday, January 4, 2011

MATUKIO MUHIMU YA SHEIN RANGERS KWA MWAKA 2010

Yafuatayo chini ni matukio muhimu, habari na picha za timu ya Shein Rangers Sports club kwa kipindi cha mwaka 2010 uliomalizika kwa mafanikio makubwa kimichezo kwa timu hiyo.

Uongozi wa timu ya Shein Rangers unapenda kutoa pongezi kwa wadau wote wa michezo kwa kutuunga mkono kwa kipindi cha mwaka 2010.

KOMBE LA SIKU YA UKIMWI 2010Mwaka 2010 timu ya Shein Rangers iliweza kutwaa ubingwa wa UKIMWI DAY CUP 2010 mashindano yaliyoshirikisha timu na vituo mbali mbali vya michezo vya mkoa wa Dar es salaam.

SIKU SHEIN ILIPOCHEZA NA TWIGA STARS


Ndani ya mwaka 2010 timu ya Shein Rangers ilicheza michezo miwili na timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars katika uwanja wa Karume.

SHEIN NA YANGA B


Siku timu za Shein Rangers na Yanga B zilipokutana katika uwanja wa Kaunda hii ilikuwa mwaka 2010.

TIMU YA SHEIN ILIPOTWAA UBINGWA WA KINDONDONI 2010Mwaka 2010 timu ya Shein Rangers ilitwaa ubingwa wa mkoa wa Kinondoni katika ligi ya vijana chini ya miaka 17 YOSSO.

WAGENI


Mwaka 2010 timu ya Shein Rangers ilipata wageni toka Japan na Canada waliokuja kuitembelea timu baada ya kupata habari zake kwa njia ya mtandao.

SHEIN ILIPOTWAA UBINGWA WA PASAKA 2010


Shein Rangers wakifurahia baada ya kukabidhiwa ubingwa wa PASAKA 2010 mashindano yaliyoshirikisha timu za Kinonzoni na Zanzibar.

AZAM NA SHEIN RANGERS ZILIPOKUTANASiku timu ya Azam ilipocheza na Shein Rangers katika uwanja wa chuo kikuu cha DSM na kurudiana katika uwanja wa Uhuru hii ilikuwa mwaka 2010

SHEIN WALIPOPOKEA ZAWADI TOKA FAMILIA YA COLONEL SEIF


Wachezaji wa Shein Rangers wakipokea zawadi ya vifaa vya michezo toka kwa wawakilishi wa familia ya marehemu Col Seif wa Mikocheni Regent Estate. Familia iliwakilishwa wajukuu wa Col Seif.

SHEIN RANGERS ILIPOZINDUA JEZI ZA 2010Shein Rangers SC, siku walipozindua jezi mpya kwa matumizi ya msimu wa mwaka 2010 hii ilikuwa mwaka 2010.

Monday, January 3, 2011

MATUKIO MUHIMU YA SHEIN RANGERS KWA MWAKA 2009

Yafuatayo chini ni matukio muhimu na picha vilivyojitokeza ndani ya kipindi cha mwaka 2009 katika timu ya Shein Rangers Sports Club.

Uongozi wa Shein Rangers unatoa shukurani kwa wadau wake wote na wapenda michezo kwa ujumla kwa ushirikiano wenu katika masuala mbali mbali.

SHEIN WALIPOCHEZA NA TSASiku timu ya Shein Rangers ilipocheza na timu ya TANZANIA SOCCER ACADEMY (TSA) inayomilikuwa na Shirikisho la Soka nchini TFF. Ilikuwa mwaka 2009.

TIMU TA SHEIN WALIPOTEMBELEA UFUKWENIWachezaji na viongozi wa timu ya Shein Rangers SC, walipokuwa katika mapumziko kwenye fukwe ya bahari ya hindi huko kingamboni mwaka 2009.

SHEIN WALIPOCHEZA NA TWALIPO


Manahodha wa timu ya (TYSF) na Shein Rangers chini ya miaka 12 wakiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo wao, nahodha wa Shein Rangers Moses Leonald (jezi bluu bahari) na nahodha wa (TYSF) Mussa Bakari (jezi yenye mistari ya bluu na nyekundu).

UBINGWA MAMA HIDAYA CUP 2009


Nahodha wa Shein Rangers Amme Mohamed akipokeza zawadi ya jezi baada ya timu ya Shein Rangers kutwaa ubingwa wa MAMA HIDAYA CUP 2009 huko Mburahati.

SHEIN RANGERS ILIPOANDAA MASHINDANO MAALUM YA KUTAFUTA WATOTO WENYE VIPAJITimu ya Shein Rangers mwaka 2009 iliandaa mashindano maalum yaliyoshirikisha watoto chini ya miaka 12 na 14 wapatao 70 kusaka watoto wenye vipaji.

SHEIN ILIPOTOA ZAWADI KWA WATOTO YATIMAWacheza na viongozi wa timu ya Shein Rangers walipotembelea kituo cha kulelea watoto yatima na kutoa zawadi katika kituo cha Sikitiko Magomeni Mikumi.

SHUJAA WA AFRIKA 2009


Mchezaji wa Shein Rangers Murshi Rashid ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji nane bora wa Afrika walioteuliwa kutengeneza video ya mashujaa wa Afrika. Wachezaji hao waliteuliwa toka katika mashindano ya copa coca cola nchini Afrika Kusini.

HII NAYO NI MWAKA 2009 WAKATI WA KUTENGENEZA VIDEO


Waandaaji wa video inayoonyesha mashujaa wa Afrika wa mashindano ya vijana wa copa coca cola nchini Afrika Kusini, video hiyo ilishirikisha wachezaji wote wa Shein Rangers.

HII ILIKUWA SINZA CUP 2009


Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh Iddi Azzan akimkabidhi nahodha wa timu ya Shein Rangers SC, Godfrey Inocent Wambura zawadi ya jezi baada ya kutwaa ubingwa wa SINZA (DIWANI) CUP 2009 mashindano yaliyoshirikisha timu toka kata mbalimbali za kinondoni.

Sunday, January 2, 2011

HERI YA MWAKA MPYA

Timu ya Shein Rangers SC, inawatakia wadau wake wote na wanamichezo wote duniani heri ya mwaka mpya 2011.

Ni imani yetu mwaka mpya wa 2011 utakuwa wa mafanikio kwa wanamichezo na ni mwaka wa kupiga hatua katika mabadiliko ya michezo nchini.

HAPPY NEW YEAR 2011