Sunday, February 27, 2011

SHEIN RANGERS YAICHAPA ABAJALO 3 - 2


Timu ya Shein Rangers SC, imeichapa timu ya Abajalo FC ya Sinza bao 3 -2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika tarehe 27 February 2011 katika uwanjwa wa TP Afrika Sinza.

Friday, February 25, 2011

MSHIKAMANO CUP 2011/2012

SHEIN RANGERS SPORTS CLUB YAANZA VIZURI

Timu ya Shein Rangers imeanza vizuri mchezo wake wa kwanza wa ligi ya Mshikamano Cup kwa kuichapa timu ya Palianda FC bao 2 - 1 katika uwanja wa Mkombozi.

Magoli ya Shein Rangers katika mchezo huo uliokuwa mgumu kwa pande zote yalifungwa na Victor Wenslaus na Ibrahimu Kombo.

Thursday, February 24, 2011

KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C KUCHEZA ROBO FAINALI YA TATU KIAINA

Uongozi wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre unawaomba radhi wadau wetu wote kwa kimya kutokana na ushiriki wao kombe la rangers kimsingi tulikuwa timu ya kwanza kuingia nusu fainali lakini kutokana na mizengwe ya waandaaji imeamuliwa kurudiwa kwa mchezo huo baada ya kcsc kupeleka malalamiko KIFA na wao kuamua jinsi walivyotaka,tunasema baada ya mashindano haya tutatoa tamko rasmi na ikibidi kuzishauri mamlaka husika jinsi mashindano ya watu binafsi yanavyotakiwa kuwa tunategemea support ya kutosha siku ya jumapili na tunasema tutakabiliana na kila hujuma ili mradi tumalizie mashindano haya nadhani mtu yeyote anayeishi mwananyamala anaelewa tulivyofanyiwa tunatoa rai kwa wakazi wote wa kijitonyama kuja kuona mechi hii ya 3 kama wenye mashindano walivyotaka na tunawahakikishia tutalinda heshima ya wakazi wote wa kijitonyama na wadau wetu wote.

By chris fidelis – katibu mkuu msaidizi

Friday, February 11, 2011

SHEIN RANGERS KATIKA MAANDALIZI YA MECHITimu ya Shein Rangers ikiwa katika maandalizi ya mchezo wake wa ligi ya Youth Super Cup 2011 dhidi ya timu ya Kiungi ya Magomeni siku ya Jumapili tarehe 13 February 2011.

Wednesday, February 9, 2011

LIGI YA YOUTH SUPER CUP 2011

TIMU YA SHEIN RANGERS SC KUIKARIBISHA KIUNGI FC

Siku ya tarehe 13 February 2011 timu ya Shein Rangers SC itakuwa mwenyeji wa timu ya Kiungi FC ya Magomeni katika mchezo wa ligi soka vijana mkoa wa Dar es salaam. Mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa TP Afrika sinza utakuwa wa marudiano baada ya Shein kushinda bao 1 - 0 katika mechi ya kwanza.

Sunday, February 6, 2011

MAZOEZI

MAANDALIZI KWA AJILI YA MECHI
Timu ya Shein Rangers inaendelea na mazoezi yake kama kawaida katika uwanja wa TP Sinza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa fainali ya Vijana Cup 2010/2011 dhidi ya Star Rangers ya Kimara na michezo yake ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam Youth Super Cup 2011 inayoendelea katika viwanja tofauti jijini.

LIGI YA YOUTH SUPER CUP 2011
Mchezo wa kwanza Shein Rangers imeichapa timu ya Kiungi ya Mangomeni bao 1 - 0.
Mchezo wa pili Shein Rangers imeichapa timu ya Makumbusho Talent bao 3 - 0.

Ligi hiyo inasimamiwa na Chama Cha Michezo Kwa Vijana Wadogo Wilaya Ya Kinondoni (KIDIYOSA) kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni.

Tuesday, February 1, 2011

KIJITONYAMA CHIPUKIZI NDANI YA UWANJA WA TAIFA
Timu ya Kijitonyama Chipukizi wakiwa katika picha tofauti siku walipocheza mchezo wa kirafiki na timu ya Simba B katika uwanja wa Taifa (Uwanja mpya).

SHEIN RANGERS YAICHAPA MAKUMBUSHO 3 - 0

LIGI YA YOUTH SUPER CUP 2011 (LIGI SOKA YA VIJANA MKOA WA DAR ES SALAAM)

Timu ya Shein Rangers Sports Club ya Sinza jiji Dar es salaam imeendeleza ubabe wake kwa kuichapa timu ngumu ya Makumbusho Talent bao 3 - 0 katika mchezo wa ligi ya Youth Super Cup 2011, mchezo huo uliojaa ufundi na kasi ulichezwa katika uwanja wa TP Afrika sinza siku ya Jumapili tarehe 30 January 2011.

Ligi hiyo inayosimamiwa na chama cha kuendeleza vijana wadogo wilaya ya Kinondoni (KIDIYOSA) inachezwa katika mtindo wa nyumbani na ugenini, huu ni mchezo wa pili kwa Shein kuibuka na ushindi katika ligi hiyo katika mechi mbili ilizocheza.