Wednesday, March 30, 2011

SHEIN KUENDELEA NA MAZOEZI

Baada ya timu ya soka ya Shein Rangers kutoka sare ya bao 1 - 1 na timu ya Kilimani FC katika mashindano ya Mshikamamo, timu hiyo inaendelea na mazoezi yake kama kawaida kujiwinda na michezo ya Pasaka. Shein ndio bingwa wa mashindano ya pasaka kwa mwaka 2010.

Friday, March 25, 2011

MSHIKAMANO CUP 2011/2012

Timu ya Shein Rangers Sports Club leo inashuka dimba la uwanja wa Mkombozi saa kumi jioni kucheza mchezo wake wa pili wa ligi ya Mshikamano 2011/2012.

Timu ya Shein Rangers wawakilishi pekee wa timu za Sinza Uzuri imeahidi ushindi na mchezo mzuri.

Tuesday, March 22, 2011

EVANCE THOMAS UNATAKIWA

Mchezaji aliyejitambulisha kwa jina la Evance Thomas aliyeomba kujiunga na timu ya Shein Rangers Sports Club kupitia njia ya mtandao anatakiwa kuripoti katika mazoezi ya Shein Ranger Sports Club saa kumi na nusu jioni katika uwanja wa TP Afrika Sinza. Kwa maelezo zaidi wasiliana na mwalimu wa Shein Rangers SC kwa simu namba 0717 294876.

Tuesday, March 15, 2011

NAHODHA WA TIMU YA SHEIN RANGERS ACHAGULIWA TIMU YA TAIFA CHINI YA MIAKA 23Mchezaji mwandamizi na nahodha wa timu ya Shein Rangers ya Sinza Godyfrey Inocent wa kushoto katika picha ya juu na wa kwanza kulia (waliosimama) picha ya chini amechaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa chini ya miaka 23(Ngorongoro) kinachojiandaa kucheza na Camerun, hii ni mara ya pili kwa timu ya Shein Rangers kutoa mchezaji timu ya taifa, baada mwaka 2009 kumtoa Murshid Ally timu ya taifa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).

Viongozi na wachezaji wa Shein Rangers wanampongeza kwa kuchaguliwa kwake timu ya taifa na wanamtakia kila la heri balozi wa Shein Ranger katika timu ya taifa.

Wednesday, March 2, 2011

KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C YATINGA NUSU FAINALI RANGERS FAMILY CUP 2010/11


WACHEZAJI WA TIMU YA KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C WALIPOKUWA WANAJIAANDAA NA MOJA YA MECHI ZA KIRAFIKI UWANJA WA TAIFA,DAR ES SALAAM.

UONGOZI WA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE UNAYO FURAHA KUWAJULISHA WADAU WETU POPOTE MLIPO DUNIANI KUWA TIMU YETU IMEFANIKIWA KUINGIA NUSU FAINALI BAADA YA MIZENGWE YA WAANDAAJI WA KOMBE HILO LUCKY RANGERS KUTAKA KUIBEBA TIMU YA DEPO F.C KUSHINDIKANA,LEO TAREHE 27-02-2011 KTK UWANJA WA S/M MWANANYAMALA B, KCSC IMEWEZA KUIFUNGA TENA TIMU YA DEPO FC KWA MAGOLI 3 KWA 1 MAGOLI YA KCSC YALIFUNGWA NA ADAM MWINGIRA DK YA 28 NA RAMADHANI SALIM DK YA 47 NA DK YA 59,KCSC ILIKUWA TIMU YA KWANZA TOKA AWALI KUINGIA NUSU FAINALI.

BY CHRIS FIDELIS (KATIBU MKUUMSAIDIZI) SIMU+255713481980.