Friday, April 29, 2011

NAHODHA WA SHEIN RANGERS AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA


Nahodha wa timu ya Shein Rangers ya Sinza (wa pili toka kulia walioinama)Godyfrey .I. Wambura akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa umri chini ya miaka 23 (U23) Manyara Stars. Timu ipo kambini kwa kujiaandaa kwa mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Uganda.

Thursday, April 28, 2011

KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE BINGWA EASTER CHALLENGE CUP 2011/12.


UONGOZI WA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE UNAYO FURAHA KUWAJULISHA WADAU WETU POPOTE MLIPO DUNIANI KUWA TIMU YETU IMEFANIKIWA KUCHUKUA UBINGWA WA KOMBE LA PASAKA 2011/12 BAADA YA KUIFUNGA TIMU YA KIJITONYAMA STAR FC KWA MAGOLI 2 KWA 0 MAGOLI YALIYOFUNGWA NA ALBERT KILIMBA D.K YA 16 NA RAMADHANI MZEE D.K YA 76 .

HIVYO KUJIPATIA ZAWADI YA SETI MOJA YA JEZI TOKA ZIZZOU FASSION NA KIKOMBE, TUNAWATUMIA BAADHI YA PICHA ZA AWALI NA BAADA YA HAPO UONGOZI UNAPANGA KUFANYA SHEREHE FUPI YA KUWAPONGEZA VIJANA WETU,TUNASHUKURU SANA KWA WADAU WALIOTUUNGA MKONO KWA HALI NA MALI WAKIONGOZWA NA BW,EVODIUS MTAWALA(KATIBU MKUU-SIMBA SPORTS CLUB) KWA SUPPORT KUBWA YA KUJA KUTUSHANGILIA,TUNASEMA ASANTENI SANA.

BY CHRIS FIDELIS (KATIBU MKUU MSAIDIZI) SIMU +255713481980.

TAARIFA HII IMETUMWA KWA NJIA YA MTANDAO NA UONGOZI WA KCSC

Sunday, April 24, 2011

MICHEZO YA PASAKA ZANZIBAR 2011

WACHEZAJI WA SHEIN RANGERS WAIBEBA KOMBAINI YA KINONDONI

Wachezaji wa timu ya Shein Rangers SC ya Sinza jijini Dar es salaam wameendelea kuonyesha uwezo mkubwa wa soka wakiwa na timu ya Kombaini ya Kinondoni huko Zanzibar katika michuano ya soka ya Pasaka.

Katika mchezo wa kwanza Kinondoni iliichapa Pita na Zako Rangers bao 1-0 bao lililofungwa na Mizza Abdallah (kutoka shein rangers). Na katika mchezo wa pili Kombaini ya Kinondoni iliichapa timu ngumu ya Coast Star bao 1 -0 mfungaji akiwa Jumanne Goa (kutoka shein rangers).

Michezo hiyo ya Pasaka imekuwa na msisimko mkubwa hufanyika kila mwaka, mwaka huu inafanyika Zanzibar katika uwanja wa Nungu uliopo Nungwi na kushirikisha timu tano amabazo ni Kombaini ya Kinondoni, Pita na Zako Rangers, Kaskazini A, Tumaini FC na Coast Star.

Wednesday, April 20, 2011

KIJITONYAMA CHIPUKIZI S.C YATINGA FAINALI EASTER CHALLENGE CUP 2010/11

WACHEZAJI WA KCSC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KABLA YA MCHEZO WAO WA NUSU FAINALI NA TIMU YA MWENGE SHOOTING,UWANJA WA BORA KIJITONYAMA.

UONGOZI WA KIJITONYAMA CHIPUKIZI SPORTS CENTRE UNAYO FURAHA KUWAJULISHA WADAU WETU POPOTE MLIPO DUNIANI KUWA TIMU YETU IMEFANIKIWA KUINGIA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA TIMU NGUMU YA MWENGE SHOOTING YA MWENGE KWA MAGOLI 4 KWA 2 .

TIMU YETU NDOGO YA U-17 INAENDELEA VYEMA NA MECHI ZAKE ZA COPA COCA COLA 2011 TUNAWAKARIBISHA WADAU NA WAPENZI WOTE WA SOKA KUJA KUIONA TIMU YETU ITAKAPOPAMBANA NA TIMU YA KIJITONYAMA STAR SIKU YA JUMAPILI YA TAREHE 24/04/2011 AMBAYO NI KILELE CHA PASAKA KATIKA UWANJA WA BORA KIJITONYAMA JIRANI NA POLISI MABATINI,MECHI HIYO INATARAJIWA KUANZA SAA 10:15 JIONI.
HAKUNA KIINGILIO .

WENU KATIKA KUKUZA NA KUENDELEZA VIPAJI.

BY CHRIS FIDELIS (KATIBU MKUU MSAIDIZI) SIMU+255713481980.

TAARIFA HII IMETUMWA KWA NJIA YA MTANDAO NA UONGOZI WA KCSC

Sunday, April 17, 2011

SHEIN RANGERS YASHINDA 3 - 1

LIGI YA MSHIKAMANO CUP 2011/2012

Timu ya Shein Rangers SC leo tarehe 17 Aprili 2011 imeichapa timu ya Mabibo Boys bao 3 - 1 katika mchezo mkali wa ligi ya Mshikamano Cup, katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Kines mabao ya Shein yalifungwa na Mengi John na Yusuph Suleiman na goli moja walijinga wenyewe.

Ushindi huo ulichangiwa sana na uelewano wa wachezaji waandamizi wa timu ya Shein Rangers walioingia kipindi cha pili wachezaji hao ni Yusuph Suleiman, Murshid Rashid, Minyi na Miza Dula. Wachezaji hao walipoingia walibadilisha sura ya mchezo na kuleta matokeo yaliyokuwa yanangojewa na watu wengi waliokuwepo uwanjani hapo.

NAHODHA WA SHEIN RANGERS AKIWA NA TIMU YA TAIFA


Nahodha wa timu ya Shein Rangers SC ya Sinza Godyfrey .I. Wambura (wanne kutoka kushoto waliopiga goti)akiwa na kikosi cha timu ya taifa umri chini ya miaka 23 (U23) Manyara Stars walipokuwa nchini Uganda katika jiji la Kampala.

Monday, April 11, 2011

YANGA BINGWA 2010/2011


Timu ya Yanga ya Dar es salaam imetwaa ubingwa wa soka wa Tanzania bara kwa mwaka 2010/2011 baada ya kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Toto Afrika ya Mwanza bao 3 - 0 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

VIJANA WA TANZANIA WASONGAMBELE


Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 23 (U23) Manyara Stars wakifurahi kwa pamoja baada ya kuiondoa katika mashindano timu ya taifa ya Cameroon kwa penati 4 - 3.

Tuesday, April 5, 2011

NAHODHA SHEIN NA TIMU YA TAIFA YA VIJANA


Nahodha wa timu ya Shein Rangers SC ya Sinza Godyfrey Inocent (wa tatu kutoka kulia) kwa waliokaa viti vya mstari wa tatu toka mbele, akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania umri chini ya miaka 23 (U23) wakifatilia mchezo wa Simba na TP Mazembe katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Sunday, April 3, 2011

TEGEMEO LETU LA KESHO


Timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 (U20) ikiwa katika moja ya michezo yake nje ya nchi. Timu hii ndio tegemeo letu la kesho katika soka la Tanzania.

Saturday, April 2, 2011

MLINDA MLANGO WA SHEIN RANGERS


Kutana na Muntasir Dawood mlinda mlango wa kutumainiwa wa timu ya Shein Rangers Sports Club ya Sinza, siku za hivi karibuni kiwango cha mlinda mlango huyo kimekuwa kwa kasi sana na kuweza kuwavutia wadau wengi wa soka mitaa ya Sinza na nje ya sinza.