Wednesday, May 25, 2011

SHEIN RANGERS WAKIJIFUATimu ya Shein Rangers SC, wakijifua katika uwanja wa TP Afrika sinza. Timu hii ambayo ni mabingwa wa YOSSO wilaya ya Kinondoni 2010/2011 inatarajiwa kushiriki mashindano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam kama bingwa toka Kinondoni.

Sunday, May 22, 2011

SHEIN RANGERS KAZINI


Kocha mkuu wa timu ya soka ya Shein Rangers Sports Club, Rashid Said akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa moja ya michezo yake.

Monday, May 16, 2011

MCHEZAJI NYOTA WA SHEIN RANGERS ATAMBA MJINI LONDON


Mchezaji nyota wa timu ya Shein Rangers SC ya Sinza Maharaj Lal Bulu (anayepokea kikombe) ambaye ana rekodi ya pekee ya kufunga mabao mengi katika timu hiyo amehamishia makali yake nchini Uingereza katika jiji la London baada ya kuiogoza timu ya Stratford Juniour kuichapa timu ya Inter Moore na kutwaa ubingwa wa East London siku ya terehe 15 May 2011. Picha zaidi za fainali hiyo hapa chini.

MAHARAJI WAKATI WA MCHEZO WA FAINALI

Saturday, May 14, 2011

NAHODHA WA SHEIN AWA MCHEZAJI BORA WA MECHI


Nahodha wa timu ya Shein Rangers SC ya Sinza, Godfrey Wambula ambaye anachezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 katika mashindano ya soka ambayo ni makubwa kuliko yote nchini ya taifa cup amekuwa mchezaji bora wa mechi kati ya timu Arusha na timu ya taifa ya vijana ya Tanzania. Pichani Wambula akipokea zawadi ya mchezaji bora wa mechi shilingi laki moja ya kitanzania katika uwanja wa chuo cha Ushirika Moshi.

Thursday, May 12, 2011

TAARIFA YA MKUTANO

Siku ya Jumapili tarehe 15 May 2011 kutafanyika mkutano wa kujadili maendeleo ya timu ya Shein Rangers SC na ushiriki wa ligi.

Mkutano huo utafanyika kuanzia saa nne kamili asubuhi katika shule ya msingi uzuri maeneo ya sinza darajani. Wanachama, wachezaji, wapenzi na wadau wote wa Shein Rangers. Wajumbe wote mnaombwa kufika bila kukosa na kuzingatia muda kwa ajili ya maendelea ya timu yetu.

Taarifa hii imetolewa na uongozi wa timu ya Shein Rangers Sports Club.

Saturday, May 7, 2011

MSHIKAMANO CUP: SHEIN YATINGA ROBO FAINALI

Timu ya Shein Rangers SC ya Sinza imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya Mshikamano Cup 2011/2012.

Timu ya Shein Rangers SC, ilijihakikishia kuingia robo fainali baada ya kuichapa timu ya African People ya Mabibo bao 3 - 1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kinesi leo tarehe 7 Mei 2011. Magoli ya Shein katika mchezo huo yalifungwa na Victor Wenslaus, Munir Abdul na Jumanne Goa.

Pamoja na kucheza vizuri katika mchezo huo timu ya Shein Rangers ilipoteza nafasi nyingi za kufunga, katika mashindano hayo timu ya Shein Rangers imecheza mechi nne na kushinda tatu na kutoka sare mchezo mmoja, kwa matokeo hayo ndio timu inaongoza kundi lake.