Wednesday, June 22, 2011

SHEIN KATIKA MAZOEZITimu ya Shein Rangers SC, inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wake wa mwisho wa makundi katika ligi ya vijana mkoa wa Dar es salaam. Shein itapambana na timu ya Kombora FC ya Temeke siku ya tarehe 24 June 2011 katika uwanja wa Twalipo Camp Mgulani.

Monday, June 20, 2011

DAYOSA CUP 2011/2012 SHEIN YASHINDA TENA

LIGI YA SOKA VIJANA MKOA WA DAR ES SALAAM (DAYOSA)

Timu ya Shein Rangers SC ambayo ndio mabingwa wa Kinondoni katika ligi ya vijana (YOSO) imeendelea kuiwakilisha vizuri wilaya ya Kinondoni baada ya siku ya tarehe 18 June 2011 kuichapa timu ngumu ya Amadori toka wilaya ya Ilala bao 3 - 2 katika mchezo wa ligi ya soka kwa vijana ya mkoa wa Dar es salaam.

Magoli ya timu ya Shein Rangers katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mwananyamala 'B' yalifungwa na Said Issa (fela) Mrisho Juma (fuso) na George Harison. Mashindano hayo yameandaliwa na chama cha michezo kwa vijana mkoa wa Dar es salaam (DAYOSA) na kushirikisha timu bingwa toka wilaya zote za mkoa huo.

TIMU YA WATOTO SHEIN


Timu ya watoto ya chini ya miaka 12 na 14 ya Shein Rangers SC.

Sunday, June 12, 2011

DAYOSA CUP 2011/2012

Timu ya Shein Rangers SC yaichapa Nusra bao 2 - 0

Timu ya Shein Rangers SC ya Sinza imeichapa timu ya Nusra SC toka Temeke bao 2 - 0 katika mchezo wa ligi ya soka ya vijana mkoa wa Dar es salaam (DAYOSA)uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwananyamala "B". Mabao ya Shein Rangers (jezi bluu bahari) yalifungwa na Suleiman Waziri na Victor Wenslaus.

Mpaka sasa timu ya Shein Rangers imecheza michezo miwili, imetoka sare mchezo mmoja na kushinda mchezo mmoja, timu ya Shein Rangers imebakiza michezo miwili kuhitimisha michezo katika kundi lake.

WACHEZAJI WA AKIBA


Wachezaji wa akiba wa Shein Rangers wakifatilia mchezo wa Shein na River Herous katika uwanja wa Magereza Ukonga.

Wednesday, June 8, 2011

SHEIN RANGERS WAANZA LIGI KWA SARE


Timu ya Shein Rangers SC ya Sinza, imeanza mchezo wake wa kwanza wa ligi ya soka ya vijana mkoa wa Dar es salaam kwa kutoka sare ya bila kufungana na timu ya River Heroes ya Ilala. Mchezo huo uliochezwa siku ya tarehe 08 June 2011 katika uwanja wa Ukonga Magereza ulikuwa mzuri na wa kuvutia licha hali ya uwanja kuwa mbaya kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha uwanjani hapo.

Timu ya Shein Rangers watajilaumu wenyewe kwa kutotumia vizuri nafasi tatu za wazi ambapo wachezaji wake wangekuwa makini wangejipatia mabao ya mapema kabisa.

Sunday, June 5, 2011

IMAGE PROFESSION SPORTS CLUB YA NAMANGA


Timu ya Soka ya Image Profession toka Namanga jijini Dar es salaam, timu hii ni timu inayochipukia na yenye wachezaji wenye vipaji vya soka. IP Sports Club ni moja ya timu za vijana yenye kucheza soka la kuvutia, iwapo kuna timu yoyote itahitaji kucheza na timu hii wasiliana na blog hii.

Saturday, June 4, 2011

SHEIN YAICHAPA IP SPORST BAO 4 - 0


Timu ya soka ya Shein Rangers SC ya Sinza imeichapa timu ya soka ya IP Sports Club ya Namanga jijini Dar es salaam bao 4 - 0 katika mchezo safi na wakuvutia uliochezwa katika uwanja wa chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama siku ya tarehe 04 June 2011. Timu ya Shein Rangers ilitumia mchezo huo kama kipimo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa kwanza wa ligi ya mkoa wa Dar es salaam itakayoanza tarehe 08 June 2011, magoli ya Shein Rangers katika mchezo huo yalifungwa na
Said Isaa (Fela), George Halison (Mwape),Timoth Emmanuel na Richard Frank (Boko).

Thursday, June 2, 2011

SHEIN RANGERS WAKIJIFUA BEACH

Wachezaji wa timu ya Shein Rangers SC, wakijifua mchangani katika fukwe ya bahari ya Hindi ili kujenga stamina.