Saturday, July 30, 2011

SHEIN RANGERS KATIKA PENATI


Wachezaji wa timu ya Shein Rangers SC ambao ndio mabingwa wa YOSSO wilaya ya Kinondoni mwaka 2010 wakifatilia kwa makini wakati wenzao wakipiga penati katika mchezo wa nusu fainali ligi ya vijana mkoa wa Dar es salaam.

Thursday, July 28, 2011

FIGO WA SHEIN RANGERS


Mchezaji Victor Wenslau (figo) akipokea maelekezo toka kwa Mwalimu wake Rashid Said katika moja ya michezo ya ligi ya vijana mkoa wa Dar es salaam.

SHEIN NDANI YA TFF


Timu ya Soka ya Shein Rangers SC, wakiwa jikoni mwa soka la Tanzania katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.

Tuesday, July 26, 2011

SHEIN RANGERS SC YAISHIA NUSU FAINALI


Timu ya Shein Rangers imetolewa katika hatua ya nusu fainali ligi ya vijana mkoa wa Dar es salaam kwa penati 10 - 9 na timu ya Mapambano ya Temeke baada ya kutoa sare ya bao 1 - 1 katika muda wa kawaida.

Wednesday, July 20, 2011

TAARIFA TOKA BLOG YA SHEIN RANGERS

Blog hii inapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi wasomaji wake na wadau wake wote kwa kutokuwa hewani kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 22 June 2011, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.

Tunapenda kuwafahamisha wadau wetu kuwa tutakuwa hewani kama kawaida kuanzia tarehe 23 July 2011. Kwa habari zaidi za Shein Rangers Sports Club tembelea facebook Page ya Shein Rangers Sports Club. Pia wadau wote mnakumbushwa kutuma habari zenu za michezo katika blog hii.

Asanteni sana by: Shein Rangers Sports Club