Tuesday, August 30, 2011

EID NJEMA

Viongozi na wachezaji wa timu ya Shein Rangers ya Sinza wanawatakia wadau wake wote sikukuu njema ya Eid.

Kutokana na sikukuu hiyo timu ya Shein Rangers imetoa mapumziko kwa wachezaji wake mpaka siku ya Jumatatu tarehe 05 Septemba 2011.

Eid Mubarak.........

MAHARAJ BULU BALOZI WA SHEIN UGAIBUNI


Mchezaji wa timu ya Shein Rangers SC ya Sinza Maharaj Bulu (wa kwanza kulia) anaendelea kuwakilisha vizuri soka la Shein Rangers na Tanzania kwa ujumla nchini Uingereza katika jiji la London akiwa na timu ya Stratford Juniour.

Tuesday, August 2, 2011

AZAM FC YALETA MAPINDUZI YA SOKA BONGO


Timu ya Azam FC imeleta mapinduzi ya mchezo wa soka nchini kwa kuwa na timu imara yenye mwalimu bora pamoja na kumiliki uwanja wa soka wa kisasa kwa ajili ya mazoezi na michezo ya ligi kuu.

Monday, August 1, 2011

SIKU SHEIN ILIPOCHUKUA UBINGWA WA KINONDONI LIGI YA YOSSO


Wapenzi wa soka na wachezaji wa Shein Rangers SC wakimpongeza kocha wa timu hiyo baada ya kuichapa Star Rangers ya Kimara katika mchezo wa fainali ligi ya YOSSO 2010 wilaya ya kinondoni katika uwanja wa Kinesi.