Wednesday, September 28, 2011

BONANZA LA SOKA KILA JUMAPILI

Timu ya Shein Rangers Sports Club, itashiriki bonanza la soka linalifanyika kila siku ya Jumapili katika uwanjwa wa TP Afrika Sinza na kushirikisha timu mbali mbali za jijini Dar es salaam.

Bonanza hilo la soka ambalo upambwa na bendi mbali mbali toka jijini lilivutia sana wapenzi wa soka na muziki wakati wa ufunguzi wake Jumapili iliyopita na kunogeshwa na bendi ya Extra Bongo chini ya Ally Choki. Mgeni rasmi siku ya ufunguzi alikuwa mbunge wa Kinondoni Mh Iddi Azan. Na timu ya Shein Rangers ilishika nafasi ya tatu.