Monday, December 12, 2011

TAARIFA KWA WADAU TOKA BONDE FC

Timu ya Bonde Fc inawatangazia mashabiki wake kuwa imeamua kujitoa katika michuano ya DAYOSA kutokana na ukiritimba na ufisadi unaofanywa na katibu wa chama hicho ndugu Mwinyimaji Tambaza kwa kitendo chake cha kuzifungia timu za Shein Rangers na Bonde fc zisishiriki michuano ya aina yoyote inayoandaliwa na chama hicho na hata kutotakiwa kucheza mechi za kirafiki na timu yeyote unayoshiriki michuano inayoandaliwa na chama hicho sasa tunajiuliza hivi huyu jamaa kazi yake kuendeleza soka au kuua vipaji vya vijana.kwani alikwisha wahi kumshawishi ndugu Ibrahimu Tewa kuifuta Shein katika michuano ya TEWA CUP baada ya shein kugoma kushiriki michuano ya DAYOSA inayoendelea kutokana na ukilitimba wa kiongozi huyu.

TAARIFA HII KWA MUJIBU WA MTANDAO WA BONDE FC

Friday, December 9, 2011

SHEIN YATINGA FAINALI TEWA CUP

Timu ya watoto chini ya miaka 14 ya Shein Rangers SC imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya TEWA CUP, baada ya kuichapa timu ya Baruti FC bao 1 - 0.

Kwa matokeo hayo timu ya Shein Rangers itacheza mchezo wa fainali na timu ya Bonde FC siku ya Jumapili katika uwanja wa shule ya msingi Somanga.

Thursday, December 8, 2011

MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA


Timu ya Shein Rangers SC ya Sinza inaungana na wanamichezo na watanzania wote nchini na nje ya nchi katika kusheherekea MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA.

Shein Rangers SC inawatakia sherehe zenye amani na upendo.