Tuesday, June 12, 2012

MABINGWA WA COPA COCA COLA KANDA YA UBUNGO

Timu ya Shein Rangers Sc chini ya miaka 17 (U 17) ambayo ndio mabingwa wa mashindano ya copa coca cola kwa kanda ya Ubungo kwa mwaka 2012. Mashindano ya copa coca cola yanafanyika kwa mwaka wa sita mfurulizo na ndio yanayoongoza kwa kuibua wacheza wengi vyota ambao ni chipukizi.

SHEIN RANGERS YAWA BINGWA WA COPA COCA COLA KANDA YA UBUNGO

FAINALI COPA COCA COLA KANDA YA UBUNGO: Timu ya Shein Rangers Sc ya Sinza imetwaa ubingwa wa copa coca cola kanda ya Ubungo baada ya kuichapa Home Team bao 1-0 katika mchezo wa fainali.

Goli pekee la Shein Rangers katika mchezo huo lilifungwa na Mnange,  pamoja na kuchukua ubingwa huo timu ya Shein Rangers imetoa wachezaji wawili wanaowakilisha mkoa wa Kinondoni katika mashindano ya copa coca cola taifa yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wednesday, June 6, 2012

SHEIN RANGERS NDANI YA CHAMAZI

Mchezaji wa Shein Rangers Miza Abdallah (kuchoto) akiwa na mchezaji wa Azam FC katika uwanja wa Chamazi unaomilikiwa na timu ya Azam. Hii ilikuwa baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Shein na Azam.

Tuesday, June 5, 2012

SHEIN RANGERS KUPAMBANA NA REAL TALLENT

SIKU YA ALHAMISI TAREHE 7 JUNE 2012 TIMU YA SHEIN RANGERS SC ITACHEZA MCHEZO WA KUJIPIMA NGUVU NA TIMU YA REAL TALLENT YA MIKOCHENI B. MCHEZO HUO UTACHEZWA SAA KUMI JIONI KATIKA UWANJA WA SHULE YA MSINGI USHINDI MIKOCHENI B. PIA TIMU YA SHEIN RANGERS INACHUKULIA MCHEZO HUO KAMA KIPIMO TOSHA KWA MAANDALIZI YA LIGI YA MSHIKAMANO MZUNGUKO WA PILI NA MAANDALIZI YA LIGI YA TFF.