Friday, August 24, 2012

SIKU JESHI LA SHEIN LILIPOKUTANA NA JESHI LA YANGATimu ya Shein Rangers SC ya Sinza ilikuwa ni miongoni mwa timu za soka zilizojipima ubavu na Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) Yanga. Mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar wakati Yanga wakijiandaa na mashindano ya Kagame Cup, katika mchezo huo Yanga ilishinda bao 5 - 1.

SHEIN RANGERS YAANZA MAZOEZI YA UFUKWENI

Timu ya Shein Rangers SC imeanza mazoezi katika fukwe ya bahari ili kujiweka sawa na maandalizi ya ligi ya TFF wilaya ya Kinondoni inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Tuesday, August 21, 2012

SHEIN RANGERS YAWAKUMBUSHA WANAMICHEZO KUSHIRIKI SENSA

Kituo cha michezo cha SHEIN RANGERS SPORTS CENTRE ambacho kinamiliki timu ya soka ya Shein Rangers kinapenda kuwakumbusha wanamichezo wote nchini kushiriki katika zoezi la kuhesabiwa la Sensa.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603.