Wednesday, September 26, 2012

SHEIN Vs YANGA


Wachezaji wa timu ya Yanga (pichani juu) wakipasha miili yao joto kujiandaa na pambano la kirafiki na timu ya Shein Rangers (pichani chini), mchezo huu ulichezwa siku chache kabla ya timu ya Yanga kwenda nchini Rwanda.

MECHI YA KIRAFIKI

Siku ya Jumamosi tarehe 29 Septemba 2012 timu ya Shein Rangers SC inajipima ubavu na timu kongwe ya SIFA POLITAN ya Temeke. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja maarufu wa chuo cha Bandari uliopo Tandika jijini Dar es salaam.

Kwa sasa timu ya Shein Rangers inaendelea na mazoezi katika uwanja wa TP Afrika uliopo Sinza muda wa asubuhi ikiwa ni maandalizi ya ligi ya TFF na Mashindano mengine yaliyopo mbele ikiwemo ligi ya vijana mkoa wa Dar es salaam.

Monday, September 24, 2012

MTAKATIFU TOM AKIWA NA WALIMU WA SHEIN

Kocha wa Yanga aliyesitishiwa mkataba wake Mtakatifu Tom (wa pili kutoka kushoto) akiwa na walimu wa timu ya Shein Rangers SC mara baada ya mchezo wa timu hizo.

Wednesday, September 19, 2012

SHEIN WAZIDI KUJIFUASHEIN WAZIDI KUJIFUA: Picha ya kwanza juu kocha mkuu wa Shein Rangers SC Rashid Said akiwa amatoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

BAADA YA MCHEZO NA YANGA

Mchezaji wa timu ya Shein Rangers Nassoro Almasi (kushoto) akiwa na mchezaji wa Yanga Steven Mwasyika mara baada ya mchezo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo mbili hivi karibuni.

Saturday, September 15, 2012

MAZOEZI YANAENDELEA KWA NGUVU

Mazoezi ya timu ya Shein Rangers SC yanaendelea kwa nguvu na morali ya hali ya juu katika uwanja wa TP, baada ya kumaliza program maalum katika fukwe ya bahari ya Hindi.

BAADA YA MAZOEZI

Baada ya mazoezi mazito ya asubuhi wachezaji wa timu ya Shein Rangers SC wakimsikiliza kocha wao Rashid Said "Sir Mokake" katika uwanja wa TP Sinza. Timu ya Shein ipo katika maandalizi ya ligi ya TFF msimu wa 2012/13.

Thursday, September 13, 2012

SHEIN RANGERS WAPIGA MAZOEZI MASAA MANNE
Timu ya Shein Rangers SC ambayo ipo katika maandalizi ya ligi ya TFF, inafanya mazoeni makali katika uwanja wa TP Sinza. Mazoezi hayo ambayo ufanyika mida ya asubuhi yamekuwa ni kivutio kwa wapenda soka wa ukanda wa huo, timu hiyo imekuwa ikifanya mazoezi yake kwa muda usiopungua masaa manne kwa siku.

TIMU YA WATOTO CHINI YA MIAKA 14 YAENDELEA NA MAZOEZI I

Wachezaji wa timu ya watoto chini ya miaka 14 wa Shein Rangers SC wakiwa na walimu wao baada ya mazoezi yao yanayoendelea kila siku jioni katika uwanja wa TP Sinza.

MCHEZAJI WA SHEIN YUPO KAMBINI TIMU YA TAIFA

Mchezaji wa timu ya Shein Rangers SC Miza Abdallah, ambaye amechaguliwa  timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 anaendelea vyema na kambi maalum ya mazoezi mkoani Mbeya.