Friday, January 31, 2014

DEVELOPMENT PLAN

The Football Federation of Tanzania Technical Development
Plan sets out the Tanzanian framework for coaching and player
development from 2013- 2016 and includes complimentary
actions in refereeing, medical practice, administration and
training facility development.

Tuesday, January 28, 2014

MAANDALIZI YA MAZOEZI

Wachezaji wa Shein Rangers SC wakiwa katika maandalizi kabla ya kuanza  mazoezi, timu ya Shein iliyopo daraja la nne ipo katika maandalizi ya ligi daraja la nne wilaya ya Kinondoni.

RATIBA YA MECHI ZA KIRAFIKI WEEKEND HIII


Siku ya Ijumaa tarehe 31 Jan 2014 Shein Vs Lebanon
Saa kumi jioni katika uwanja wa Madoto Mburahati

Siku ya Jumamosi tarehe 01 Feb 2014 Shein Vs Kijitonyama Stars
Saa kumi jioni katika uwanja wa Bora Kijitonyama
Michezo yote hii ni maandalizi ya ligi daraja la nne Wilaya ya Kinondoni.

Sunday, January 26, 2014

MAANDALIZI YA LIGI DARAJA LA NNE WILAYA YA KINONDONI

MAANDALIZI YA LIGI DARAJA LA NNE WILAYA YA KINONDONI:- Timu ya Shein Rangers SC leo imeichapa timu  Juhudi FC ya Mabibo bao 3 - 1 katika mchezo mkali wa kirafiki  uliochezwa katika uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar.

Magoli ya Shein katika mchezo huo yalifungwa na Said Isaa fela (2) na Jumanne Goa (1), baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Shein Rangers  Rashid Said mokake aliuambia mtandao wa club kuwa ameridhishwa na kiwango cha vijana wake kwani walicheza soka safi sana.

Friday, January 24, 2014

NYOTA MPYA YATABILIWA SHEIN RANGERS

Mchezaji wa timu ya watoto ya Shein Rangers SC Goodluck Willlyhapton a.k.a Kibabu ni miongoni mwa wachezani vijana kabisa waliotokea timu ya watoto chini ya miaka 17 ya Shein Rangers na kufanikiwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Shein Rangers, mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji wa Shein wanaojiandaa na ligi daraja la nne na ni mategemeo yetu ni nyota mpya inakuja katika kulimwengu wa soka.

SHEIN YAICHAPA GONGA FC 5 - 1

Timu ya Shein Rangers imeichakaza timu ya Gonga FC bao 5 - 1 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Bora kijitonyama.

Wafungaji katika mchezo huo ni  Hassani Kapalata aliyefunga mabao matatu hat trick na Deogratius Kulwa aliyefunga mabao mawili timu ya Shein ipo katika maaandalizi ya ligi daraja la nne wilaya ya Kinondoni.

Thursday, January 16, 2014

SOKA NA KAZI: KUDO MASTER WA SHEIN RANGERS


Picha mbili tofauti zikionyesha mchezaji mahili wa Shein Rangers Kudo, maarufu kama Kudo Master akiwa mazoezini na nyingine kazini. Huu ni mfano kwa vijana wengine wa kitanzania kuwa tunaweza tukacheza soka huku tukawa tunakazania masomo ama kazi, vyote vinawezekana kama Kudo Master kaweza wewe kwa nini usiweze? Kudo Master alipata elimu yake ya Computer UCC iliyo chini ya chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kama UD.

AGOGO WA SHEIN RANGERS AKIJIFUA

Mchezaji wa Shein Rangers Victor Wenslaus Agogo akijifua kujiweka sawa kwa ajili ya ligi ya TFF inayotarajia kuanza hivi karibuni.

MCHEZAJI WA KIMATAIFA YANGA AVUTIWA NA KIUNGO CHIPUKIZI WA SHEIN RANGERS SC

Mchezaji wa kimataifa wa Yanga Haruna Niyonzima alivutiwa na kiwango cha mchezaji wa Shein Rangers Miza Abdallah ambaye naye anacheza nafasi ya kiungo, hii ilikuwa baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Shein Rangers SC katika uwanja wa shule ya Loyola.

Sunday, January 12, 2014

SHEIN YAJIANDAA NA LIGI DARAJA LA NNE

Timu ya Shein Rangers ipo katika maandalizi ya ligi daraja la nne kwa msimu wa mwaka 2014/15. Mdau wa michezo unaombwa mchango wako wa hali na mali ili kufanikisha malengo ya timu ya kupanda daraja.