Friday, May 16, 2014

SHEIN YAMALIZA MICHEZO YAKE YA MZUNGUKO WA KWANZA

SHEIN YAMALIZA MICHEZO YAKE YA MZUNGUKO WA KWANZA
Timu ya Shein Rangers Sports Club imemaliza michezo yake ya mzunguko wa kwanza ya ligi Daraja la nne wilaya ya  Kinondoni mapema wiki iliyopita. Katika mzunguko wa kwanza ilicheza michezo mitano na kushinda mitatu na sare miwili, imefunga magoli 17 na kufungwa matatu. 

Kwa sasa timu hiyo imesitisha mapumziko kwa wachezaji wake wote waliopewa mapumziko kwa ajili ya kujiandaa kikamilifu na mzunguko ujao, nia ya Shein Rangers SC ni kupanda daraja msimu huu.