Wednesday, June 4, 2014

SHEIN RANGERS KUANDIKISHA WANACHAMA WAPYA

Mkutano mkuu wa Dharula uliofanyika siku ya tarehe 01 Jun 2014 umejadili mambo mbalimbali kuhusuana na maendeleo ya timu katika ligi daraja la nne na swala la kubadirisha kadi za Uanachama na uandikishaji wa wanachana wapya.

Kutokana na kubadirika kwa mfumo wa uandikishaji uanachama na kadi utalazimika kujaza fomu maalum ya maombi ya uanachama. Pia uongozi unatoa taarifa kwa wanachama wake na watu wengine wanaopenda kuwa wanachama kuwa fomu hizo zinaanza kutolewa siku ya Jumapili tarehe 08 Jun 2014 makao makuu ya timu Sinza Uzuri (Lombo) kwa "Chid" . Fomu hizo zitauzwa Tshs 2000/= tu.

Taarifa hii imetolewa na:-
Ramadhan .R. Sunga
Katibu