Sunday, October 23, 2016

SHEIN RANGERS YAZAWADIWA VIFAA

Mdau wa michezo Sinza Ndugu Yahaya (kushoto) aizawadia timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB vifaa vya michezo. SHEIN ambao ndiyo mabingwa wa Wilaya ya Kinondoni, pichani juu akikabidhi jezi na mipira kwa mjumbe wa soka la vijana wa SHEIN ndugu Rashid Said hivi karibuni.

Tuesday, October 18, 2016

TAARIFA TOKA SHEIN RANGERS SPORTS CLUB

Uongozi wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB unapenda kutoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kupapamba na kujitoa kwao hadi kufikia lengo tulilojiwekea mwaka huu la kupanda daraja kwa msimu huu. Vilevile uongozi unatoa Shukurani za dhati kabisa kwa wadau na wanamichezo wote walioiunga mkono timu kwa wakati wote wa ligi daraja la tatu Wilaya ya Kinondoni na hatimaye timu kujenga historia mpya kwa kuwa mabingwa wa ligi daraja la tatu Wilaya ya Kinondoni kwa msimu wa 2015/16 uliomalizika hivi karibuni.

Hakuna cha kusema zaidi ya kusema Asante wanakinondoni kwa kutuunga mkono kwa wakati wote.

Kwa sasa timu inaendelea na maandalizi ya ligi ya Mkoa katika uwanja wa Sinza "E" Darajani, pamoja na maandalizi hayo ni kipindi cha kutengeneza Kikosi imara cha ushindani na benchi la ufundi linatumia nafasi hiyo kufanya usaili kwa wachezaji wapya wenye uwezo wa kuitumikia timu. Benchi la ufundi Shein Rangers linapenda kuwataarifu wachezaji wanaojiona wana uwezo wa kuitumikia timu kufika uwanjani hapo kwa ajili ya majaribio. Muda wa majaribio ni saa 10:00 jioni hadi saa 12:30 jioni kila siku ya Jumatatu hadi Jumatano, eneo uwanja wa Sinza "E" Darajani.

Friday, October 14, 2016

SHEIN RANGERS NDIO MABINGWA WA KINONDONITimu ya Shein Rangers Sc leo imedhiilisha kuwa haikuongoza kundi B kwa bahati baada ya kuichapa Ukwamani FC walioongoza kundi A katika mchezo mzuri wa fainali kusaka Klabu bingwa ya Wilaya ya Kinondoni kutamatisha ligi daraja la tatu wilaya. Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Kinesi umeamua nani bingwa wa wilaya kati ya timu mbili zitakazowakilisha Kinondoni katika ligi ya mkoa wa Dar es salaam.

Katika mchezo wa leo magoli yote ya Shein Rangers yalipatikana katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mkongwe Shomari Pengo na Muddy Vidal. Pamoja na ushindi huo Shein ilizawadiwa Kombe na Cheti cha ushiriki wa ligi daraja la tatu kwa msimu wa 2015/16 iliyomalizika hivi karibuni.

FAINALI YA KLABU BINGWA KINONDONI LEO

Ule mchezo wa fainali Klabu Bingwa Wilaya ya Kinondoni uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa kati ya timu ya Shein Rangers na Ukwamani FC utachezwa leo katika uwanja wa Kinesi saa kumi jioni.

Pamoja na mchezo huo vilabu vyote vilivyoshiriki ligi daraja la tatu msimu huu vitakabidhiwa vyeti uwanjani hapo kabla ya mchezo huo.

Wednesday, October 12, 2016

FAINALI UBINGWA WA WILAYA YA KINONDONI

Kesho Ijumaa tarehe 14 October 2016 timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB inatarajia kuandika Historia mpya katika mchezo wa soka kwa kuwania ubingwa wa Wilaya ya Kinondoni baada ya kuibuka kinara wa kundi B katika ligi daraja la tatu Kinondoni. Kwa matokeo hayo itacheza na kinara wa kundi A timu ya Ukwamani FC kutafuta bingwa wa Wilaya.

Mchezo huo wa fainali utachezwa katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam, muda wa saa 10:00 jioni. Vilevile pamoja na mchezo huo Chama Cha Mpira Kinondoni KIFA kinatarajia kutoa vyeti kwa timu zote shiriki ligi daraja la tatu iliyomalizika hivi karibuni, Viongozi wa vilabu mnatakiwa kudhuria tukio hilo litakalofanyika kabla ya mchezo wa fainali.

Mungu Ibariki Shein Rangers, Mshikamano Daima!!

Saturday, October 8, 2016

Wednesday, October 5, 2016

Shein Rangers Yaendelea na Mazoezi

Timu ya Shein Rangers inaendelea na mazoezi kujiandaa na fainali ya kutafuta bingwa wa Wilaya ya Kinondoni