Tuesday, October 18, 2016

TAARIFA TOKA SHEIN RANGERS SPORTS CLUB

Uongozi wa timu ya SHEIN RANGERS SPORTS CLUB unapenda kutoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kupapamba na kujitoa kwao hadi kufikia lengo tulilojiwekea mwaka huu la kupanda daraja kwa msimu huu. Vilevile uongozi unatoa Shukurani za dhati kabisa kwa wadau na wanamichezo wote walioiunga mkono timu kwa wakati wote wa ligi daraja la tatu Wilaya ya Kinondoni na hatimaye timu kujenga historia mpya kwa kuwa mabingwa wa ligi daraja la tatu Wilaya ya Kinondoni kwa msimu wa 2015/16 uliomalizika hivi karibuni.

Hakuna cha kusema zaidi ya kusema Asante wanakinondoni kwa kutuunga mkono kwa wakati wote.

Kwa sasa timu inaendelea na maandalizi ya ligi ya Mkoa katika uwanja wa Sinza "E" Darajani, pamoja na maandalizi hayo ni kipindi cha kutengeneza Kikosi imara cha ushindani na benchi la ufundi linatumia nafasi hiyo kufanya usaili kwa wachezaji wapya wenye uwezo wa kuitumikia timu. Benchi la ufundi Shein Rangers linapenda kuwataarifu wachezaji wanaojiona wana uwezo wa kuitumikia timu kufika uwanjani hapo kwa ajili ya majaribio. Muda wa majaribio ni saa 10:00 jioni hadi saa 12:30 jioni kila siku ya Jumatatu hadi Jumatano, eneo uwanja wa Sinza "E" Darajani.

1 comment: